Monday, 1 June 2020

Maandamano kutokana na kifo cha George Floyd yaendelea katika miji mbalimbali nchini Marekani

...
Waandamanaji wanaopinga ubaguzi kwa mara nyingine  tena wameingia  mitaani katika miji nchini Marekani jana Jumapili kupaza sauti  zao za hasira dhidi ya ukatili wa polisi.

Wakati  huo huo utawala wa rais Donald Trump  uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika  katika  usiku wa  siku  tano  kuwa  ni  magaidi wa ndani. 

Rais Trump  aliwapongeza wanajeshi wa kikosi cha  ulinzi wa taifa kwa  kusema, "pongezi kwa  walinzi  wetu  wa  taifa kwa  kazi  nzuri waliyofanya  mara  walipowasili Minneapolis , Minesota, usiku  wa jana," alisema  hayo  katika  ukurasa wa  Twitter

Waandamanaji  walichoma  moto  karibu  na  Ikulu ya  Marekani  ya White House wakati hali  ya  wasi  wasi  na  polisi  ilipopanda wakati  wa  siku  ya  tatu  mfululizo ya  maandamano  ya  usiku yaliyofanyika  kujibu kifo cha  George Floyd mikononi mwa  polisi mjini  huko Minesota. 

Waandamanaji pia walikusanya  vibao vya alama  za  barabarani  na vizuwizi  vya  plastiki  na  kuchoma moto  katikakti ya  mtaa  H. ..Baadhi  walishusha  bendera  ya  marekani  kutoka  katika  jengo  la karibu  na  kuitupa  katika  moto.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger