Tuesday, 2 June 2020

Jarida la Billboard lawataka wasanii wa nje kujifunza kutoka kwa Daimond

...
Billboard wameachia makala wakielezea namna ya kupata mafanikio kimataifa kwa kutumia mtandao wa Youtube huku wakimtolea mfano star wa muziki wa Tanzania Diamond Platnumz
.
Makala hiyo imeandikwa "Wanamuziki wa Marekani wanatafuta njia za kutoboa kwenye Youtube, Wanapaswa kusoma mikakati ya kufanya na kuachia video kutoka kwa wasanii wa Kiafrika

"Wasanii wa Magharibi wanaweza kujifunza kutoka kwa kile wanachokifanya wasanii wa Kiafrika haswa wale ambao wamefanikiwa kimataifa," Amezungumza meneja wa 'Youtube Music Trends' Kevin Meenan, ambaye anasimamia ukusanyaji na uchambuzi wa data za chati za Muziki za YouTube

Ameelezea kuwa alivutiwa sana na mbinu pamoja na ubunifu ambao anautumia msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz kwenye chaneli yake ya YouTube na sehemu moja tu ya mkakati wa ujasiriamali ambao unajumuisha kituo cha redio ya FM pamoja na TV na usimamizi wa kampuni ya WCB Wasafi.

Kevin Meenan amesema Ukubwa wa Diamond kwenye Youtube ni wa kustaajabisha akiwa na Subscribers Millioni 3.6 na zaidi ya jumla ya views Millioni 980 huku 80% ya watamazaji wakiwa wanatokea nje ya Tanzania kutoka Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020

Meenan anasema kwamba, kimataifa Diamond alitazamwa zaidi na watu wa Nchini Kenya ikifuatiwa na Tanzania na Marekani.

Billboard wameeleza kuwa Msimamizi huyo wa Youtube Trending alishangazwa kukuta Diamond ameweka zaidi ya video 600 kwenye mtandao wa Youtube "Kwa kweli ilibidi nichunguze mara tatu ili kuhakikisha kuwa ilikuwa sawa," Alielezea

Wamesifia kuwa Diamond anaweza kuweka hadi video 20 akitangaza Official video moja tu huku wakitolea mfano wa wimbo wa Jeje ambapo ukiachana na Official video, kuna dance video, cartoon video, lyrics video pamoja na official audio.

Kwenye Makala hiyo Billboard wameelezea kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kufikisha subscribers zaidi ya Million 1 basi huwa wanatazamwa zaidi na watu wa nje ya nchi zao

Credit: Bongo5


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger