Serikali imesitisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la Tanzania Daima kwa kukithiri, kujirudia makosa yanayokiuka sheria za nchi na maadili ya uandishi wa habari licha ya kuwaonya, kuwaeleza na kuwakumbusha wahariri wa gazeti hilo.
Leo Jumanne tarehe 23 Juni 2020, Patrick Kipangula, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ametangaza kusitishwa leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti hilo, kuanzia kesho Jumatano tarehe 24 Juni 2020.
Kipangula amedai, uamuzi huo umechukuliwa baada ya wahariri wa gazeti hilo kukiuka masharti ya leseni waliyopewa, licha ya kuonywa mara kadhaa.
“Umma unataarifiwa kuwa Gazeti la Tanzania Daima halitaruhusiwa kuchapishwa wala kusambazwa popote nchini au nje ya nchi, klufuatia uamuzi wa kusitisha leseni ya gazeti hilo. Uamuzi huu unatokana na kukithiri na kujirudia kwa makosa yanayokiuka sheria za nchi
“Juhudi za kuwaonya, kuwaelekeza na kuwakumbusha wahariri wa gazeti hilo, kufuata masharti ya leseni kwa muda wa mwaka mmoja sasa, zimeshindwa kuzaa matudna kutokana na ukaidi.”- Amesema
0 comments:
Post a Comment