Saturday, 23 May 2020

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Tanzania na Kenya kuhusu madereva wa malori

...
Mawaziri wa Sekta ya Uchukuzi kutoka Tanzania na Kenya wamekutana katika Mpaka wa Namanga Upande wa Tanzania kutatua changamoto ya kibiashara na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili katika kuvuka mpaka wa nchi moja kwenda nyingine.

Kufuatia majadiliano yaliyofanyika, pande hizo mbili zimefikia makubaliano kuwa utaifa wa madereva watakaokutwa na maambukizi ya virusi vya corona hautawekwa wazi.

Taarifa ambayo imesainiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania na yule wa Kenya, Issack Kamwele na James Macharia, inaeleza kuwa taarifa hizo zitawasilishwa kwa mamlaka husika kupitia njia za kidiplomasia kwa ajili ya hatua zaidi.

“Watendaji wa malori watapimwa afya zao kabla ya kuanza safari kwa kuzingatia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO), na watapatiwa vyeti vitakavyodumu kwa siku 14 kuonesha kuwa hawana maambukizi ya Covid-19. Kazi hiyo itafanywa na mamlaka itakayotambulika na pande zote mbili,” viongozi hao wamesema.

Kila gari (lori) litaruhusiwa kuwa na watu wasiozidi watatu, na kila nchi itaainisha maeneo ambapo madereva hao wataruhusiwa kusimama na kulala.

Aidha, Wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika pande mbili za nchi hizo wataendelea na shughuli zao kwa sharti la kutambulika na mamlaka za serikali ikiwa ni pamoja na idara za uhamiaji na polisi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger