Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaoongozwa na Askofu Josephat Gwajima wakiwa nje ya geti la kiongozi huyo.
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajim.
POLISI wanaotajwa kuvaa nguo za
kiraia (askari kanzu), wanadaiwa kuzingira nyumba ya Askofu wa Kanisa
la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Salasala nje kidogo ya jijini Dar
es Salaam majira ya saa nane mchana.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vinadai
kuwa askari hao walifika nyumbani kwa askofu huyo mchana huo ambapo
ilielezwa kuwa baada ya kufika kwa kiongozi huyo wa kiroho waligonga
geti lakini halikuweza kufunguliwa na kuamua kuweka kambi kwa muda wa
saa mbili.
Ilielezwa kuwa mlinzi wa geti hilo hakuweza kufungua wala kutoka ndani hadi askari hao walipoondoka eneo hilo.
Mwandishi wa mtandao huu alifika eneo la
tukio na hakukuta askari hao kwani walikuwa wameshaondoka japokuwa
kulikuwa na waumuni wa kanisa hilo nje ya geti.
Hata hivyo walipoulizwa juu ya uwepo wa askari walisema hawajui lolote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa
Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa na mwandishi wetu
kuhusiana na madai hayo alikiri kuwa askari wake walikwenda kwa Gwajima.
“Askari wangu walikwenda kumuona Gwajima
lakini hawakumkuta, hivyo wakarudi ofisini,” alisema kamanda Fuime bila
kufafanua nia ya kumfuata kiongozi huyo wa kiroho.
0 comments:
Post a Comment