WATU wanane wameuawa baada ya kupigwa risasi na mwanajeshi ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye iliyopo mjini Kampala nchini Uganda.
Msemaji wa Jeshi la Uganda, Meja Edward Birungi, ameeleza kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe.
Mwanajeshi huyo anaripotiwa kuwa mlevi na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi kiholela akimtafuta mkewe ambaye alifanikiwa kutoroka.
Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi waliuawa katika tukio hilo.
Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu.
Mwanajeshi huyo naye aliuawa kwa kupigwa risasi.
0 comments:
Post a Comment