Friday, 29 November 2024

CHAUMMA YAPATA KITI KIMOJA SERIKALI ZA MITAA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimepata kiti kimoja katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa wenyeviti wa mitaa katika uchaguzi uliofanyika jana Novemba 27, 2024.

Mchengerwa amesema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo akikitaja Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuongoza kwa kupata jumla ya viti 4,213 sawa na asilimia 98.83 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikishika nafasi ya pili kwa kupata viti 36 sawa na asilimia 0.84.

Mapema akizungumzia kwa upande wa wenyeviti wa vijiji, Mchengerwa amesema huko pia CCM imeongoza asilimia 99.01 ( viti 12,150) huku Chadema ikipata asilimia 0.79 (viti 97).

Share:

Thursday, 28 November 2024

MKURANGA WAHAMASISHWA MALIPO YA HUDUMA ZA MAJI

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma Mkuranga inaendelea na zoezi la kuhamasisha ulipaji wa ankara za majisafi kwa wateja wa eneo la Mwanambaya, kata ya Mipeko Wilaya ya Mkuranga.

Zoezi hilo limeenda sambamba na kutoa wito kwa wateja kulipa bili zao kwa wakati ili waendelee kupata huduma za majisafi na kuwezesha Mamlaka kuboresha zaidi huduma zake.

Zoezi hili linaendelea katika kata zote nane, ambazo ni Mkuranga, Mipeko,Vikindu Vianzi,Kiparang'anda,Mwandege,Tambani na Tengerea.
Share:

WAZIRI KOMBO AWASILI MAKAO MAKUU YA EAC ARUSHA KUSHIRIKI MKUTANO WA 46 WA MAWAZIRI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thatib Kombo akiwasili katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha leo tarehe 28 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 46 wakawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo.

Mkutano wa Mawaziri unafanyika kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC utakaofanyika tarehe 29 na 30 Novemba 2024.

Mhe. Balozi Kombo anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa Mawaziri.
Share:

MBOWE, LISSU WATUACHIE CHAMA CHETU

 


SINGIDA-Mpasuko ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeendelea kutamalaki huku chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni viongozi wakuu wa chama hicho kuyapa kisogo majukumu na vipaumbele vya chama huku wakiangalia fursa za kushibisha matumbo yao.

Hali hiyo, inatajwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwa chanzo kikuu cha wao kukosa mwelekeo na kupoteza matumaini kuanzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi Uchaguzi Mkuu ujao.

Miongoni mwa viongozi ambao wanatajwa kutotabirika ni Makamu Mwenyekiti wa chama Bara, Tundu Lissu ambaye imedaiwa ni hodari wa kulalamika, lakini uwezo wa kutenda ni sufuri.

"Wakati Taifa linajiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, Tundu Lissu alikuwa Ulaya.

"Wakati wa kampeni, alikuwa bize kutuambia ukweli kwamba chama chake hakikujipanga.

"Leo, siku ya uchaguzi, hayupo.Hodari wa kulalamika, lakini bingwa wa kutotenda. Huu ndio udhaifu wa uongozi wa CHADEMA.

"Wameshindwa kutekeleza ahadi zao, lakini wanaendelea kutoa maneno tupu, tunahitaji viongozi wanaotenda, si walalamikaji," amesisitiza mmoja wa wanachama.

Aidha, kwa nyakati tofauti mkoani Singida ambako ni nyumbani kwa Tundu Lissu baadhi ya wanachama wa chama hicho wamesema,hawana imani na Lissu katika siasa.

"Lissu siasa imemshinda na hata chama chetu bila uongozi mpya hakuna mwelekeo tena.

"Ni vema, Lissu akarejea kwenye taaluma yake, huku kwenye siasa hakumfai, siasa ya kisasa inahitaji umakini na utafiti, si uropokaji.

"Kama vipi Lissu na kina Mbowe watuachie chama chetu tukijenge upya, chama kimechoshwa hadi kimetuchosha wanachama wenyewe.

"Kwa mwelekeo wa sasa, hatuna matarajio ya kufanya vema tena, pengine tumewapa njia ya ushindi wa kishindo CCM katika chaguzi zote,"amesema Said ambaye ni mwanachama wa chama hicho na mkazi wa Ikungi.
Share:

Wednesday, 27 November 2024

DC MUHEZA ATOA WITO KWA WANANCHI KUTIMIZA HAKI YAO YA MSINGI KUCHAGUA VIONGOZI

 




Na Oscar Assenga, MUHEZA.

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Zainab Abdallah Issa amewataka wananchi wilayani humo kutimiza haki yao ya msingi kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo hapa nchini.

DC Zainab aliyasema hayo leo mara baada ya kushiriki zoezi la kupiga kura katika Ofisi ya Mtendaji Kata Mbaramo wilayani humo huku akisisitiza kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kupigia kura.

Alisema zoezi la kupiga kura ni haki ya kila mwananchi ambaye alijiandikisha hivyo uwepo wa ulinzi na usalama kwenye vituo vya kupigia kura unawapa nafasi wananchi kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Alisema kwamba ni muhimu wananchi kujitokeza mapema kupiga kura kutokana na kuwa zoezi hilo ni la muda mfupi wanapofika kwenye vituo wana hakiki majina na kuingia kwenye mchakato wa kupiga kura

“Nitoe wito kwa wana Muheza na Watanzania kujitokeza kwa wingi tutimize haki yetu ya msingi kuwachagua viongozi ambao tunawakata kwa maslahi ya maendeleo ya maeneo yetu kwa miaka mitano ijayo”Alisema

“Niwaombe leo ni siku ya mapumziko huna sababu ya kusubiri mpaka saa 10 jioni twendeni tukapige kura hali ya usalama kila mahali imeimarishwa na mungu atatujalia mpaka tutakapofunga tutafunga kwa usalama”Alisema DC Zainab.

Hata hivyo aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo waliojitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uandikishaji huku akieleza kwamba katika zoezi hilo la upigaji kura wataendelee kuhamasishana.
“Pale ulipojiandikisha ndio utakapopiga kura imani yangu wana Muheza 187,000 kama walivyojiandikisha tutapiga kura na tutahakikisha zoezi linakamilika salama.

Awali akizungumza mara baada ya kupiga kura kwenye kituo hicho cha kupigia kura Mkazi wa Mbaramo wilayani Muheza Martha Joseph alisema wanamshukuru mungu wameanza kupiga kura saa mbili asubuhi na mpaka sasa zoezi linaendelea vizuri na hivyo wanaamini litamalizika salama.
Share:

RAIS SAMIA AMLILIA DKT. NGUGULILE

  


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024.


Rais Samia ametoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kufuatia Msiba huu Mzito.


Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen



Share:

TANZIA: DKT. NDUGULILE AFARIKI DUNIA

Share:

Tuesday, 26 November 2024

WAHAMIAJI HARAMU WAVAMIA SHINYANGA, JESHI LA POLISI LAKAMATA SABA, LATAKA USALAMA WAKATI WA UCHAGUZI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeendelea kufanya doria na operesheni kubwa za kukabiliana na uhalifu na wahamiaji haramu, ambapo katika operesheni za hivi karibuni, wahamiaji haramu saba kutoka nchini Burundi wamekamatwa, hatua inayosemekana kuwa ni moja ya mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya uhamiaji haramu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Novemba 26,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema mnamo Novemba 13, 2024, wahamiaji watatu walikamatwa huko Kijiji cha Mseki, Kata ya Bulungwa, Wilaya ya Ushetu, wakiwa wameingia nchini kinyume cha sheria. 

Aidha, Novemba 17, 2024, wahamiaji wanne walikamatwa katika Kijiji cha Nyamilangano, Wilaya ya Ushetu, ambapo walikamatwa kwa kosa la kuingia nchini bila kibali cha mamlaka ya uhamiaji.

 "Wahamiaji wote saba ni raia wa Burundi na wamepelekwa katika ofisi za uhamiaji kwa hatua zaidi",amesema. 

Polisi Yakamata Wahalifu na Vifaa vya Wizi Kishapu

Huku operesheni za kudhibiti wahamiaji haramu zikiendelea, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga pia limefanikiwa kukamata wahalifu katika Wilaya ya Kishapu, wakituhumiwa kwa wizi wa mbegu za pamba na bidhaa zingine za Serikali.

Kamanda Magomi ameeleza kuwa Mnamo Novemba 15, 2024, huko Kijiji cha Mwamishoni, Kata ya Bubiki, Polisi walikamata gari moja aina ya Fuso lilikokuwa limebeba mbegu za pamba 210, ambapo mifuko 107 ya pamba iliibiwa kutoka katika chama cha AMCOSS Mwamishoni. Aidha, mnamo Novemba 23, 2024, mtuhumiwa mmoja alikamatwa huko Kijiji cha Maganzo kwa kuuza mbegu za pamba za ruzuku kwa mtu ambaye bado anatafutwa na Polisi.

Mafanikio Makubwa Katika Kudhibiti Uhalifu na Ulinzi Barabarani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema kuwa kuanzia Oktoba 24, 2024 hadi Novemba 25, 2024, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata jumla ya wahalifu 51 pamoja na vielelezo mbalimbali, vikiwemo Bhangi kilo 10, Pikipiki 09, Pombe ya moshi lita 15, Godoro 04, Container 02 za bati, Mashine 03 za Bonanza, Gari aina ya FUSO ikiwa na Nondo 130, Binding wire 11, Mifuko ya Saruji 100 vitu vinavyo dhaniwa kuwa vya wizi pamoja, Gari 01 aina ya Toyota Noah iliyotumika kubeba vitu vya wizi, Simu 02, Redio 07, Kabati 01, Fridge 01, na Kitanda 01 cha mbao.

Pia, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata makosa 7,920 ya uendeshaji wa magari na vyombo vya usafiri, ambapo wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.

Katika upande wa kesi za uhalifu, amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kuona hatua kubwa katika mfumo wa haki, ambapo washtakiwa kadhaa wamehukumiwa vifungo vizito. 

Kesi mbalimbali zimepata mafanikio, ikiwemo Mshtakiwa mmoja katika kesi ya kulawiti amepewa kifungo cha maisha jela, Washtakiwa watatu katika kesi za kubaka wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja na Washtakiwa wawili katika kesi za ukatili dhidi ya watoto na kusafirisha madawa ya kulevya wamehukumiwa kifungo cha miaka 5 kila mmoja.

Uhamasishaji wa Jamii na Usalama wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kamanda Magomi amesisitiza umuhimu wa usalama katika uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa, akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchaguzi na kwamba Polisi wamejipanga kuhakikisha usalama wa raia kutoka majumbani hadi kwenye vituo vya kupiga kura na kurudi majumbani kwao.

Share:

NLD YAHIMITISHA KAMPENI KWA KISHINDO HANDENI YAWAOMBA WANANCHI KUWAPA RIDHAA WAGOMBEA WAO ILI WAWAPE MAENDELEO



Na Oscar Assenga,HANDENI.

CHAMA cha The National League For Democracy (NLD) kimehitimisha kampeni kwa wagombea ambao wanawania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu huku wakiwawataka wananchi kuwapa ridhaa ili waweze kuwapa maendeleo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni wa kuhitimisha kampeni hizo katika viwanja vya soko la Misima wilayani Handeni,Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassani Doyo alisema kwamba chama hicho kimejipanga kuhakikisha wanatatua kero za wananchi zinazowakabili kwa muda mrefu.

Alisema kwamba wagombea ambao wamewasimamisha kwenye maeneo yote wanauwezo mkubwa wa kuweza kuwatumikia wananchi na kuwasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili kutokana na kwamba wanatosha na uwezo wa kuwaongoza.

“Sisi katika uchaguzi huu tumewasimamisha wagombea wasiokuwa na njaa lakini pia wenye uwezo wa kutoa ajira kwa wengine kupitia fursa tulizonazo na wengi wametoa ajira kwenye jamii zinazowazunguka”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Doyo aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo kwa baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.

“Haiwezekani mgombea anachukua fomu ya kugombea anaijaza halafu akairudisha alafu leo unaambiwa kajitoa hii ni rushwa ya wazi wazi kabisa kwa hiyo tunaiomba Takukuru iingilie kati haraka iwezekanavyo “Alisema

Share:

BOSI ANATAKA NIMPE PENZI NDIO ANIPANDISHE CHEO

Jina langu ni Jesca kutokea Mwanza, Tanzania, naweza kusema itanichukua miaka mingi sana kuja kusahau kitendo cha Bosi wangu niliyekuwa namuheshimu sana alipoaniambia ili kupanda cheo kazini basi ni lazima nilale na angalau mara kadhaa.

Nilikataa mara moja kwani uwezo wa kazi ninao mzuri na isitoshe nimesoma vizuri na vyeti vya kitaaluma ninavyo. Nikajisema kimoyo moyo kama vipi nitaacha hii kazi akiendelea kunisumbua kuhusu jambo hilo.

Baada ya kumkatalia Bosi, haukuisha mwezi rafiki yangu wa kike ambaye alinikuta kazini nikiwa na miaka mitatu aliweza kupandishwa cheo pamoja na mshahara huku mimi nikisalia mtupu.

Nilijua fika ni hasira za Bosi dhidi yangu na asingeza kunifukuza kutokana mkataba wangu ulikuwa na kipengele iwapo nitafukuzwa wanilipe fidia kwa muda wote uliosalia.

Jambo hilo liliniacha na msongo sana wa mawazo, niliamua kumpigia rafiki yangu simu aliyepo jijini Kagera na kumuuliza kama naweza kuhamia huko kikazi maana maisha ya Mwanza yamenishinda.

Aliniuliza tatizo ni nini hasa?, nikamwambia mkasa wangu wote na Bosi wangu akanioneka sana huruma.

Akaniambia yeye alishapandishwa cheo zaidi ya mwaka mmoja uliyopita, nilimuuliza kama alilala na Bosi ndipo akapata fursa hiyo ambayo nimekuwa nikiipigania kwa miaka mingi.

Alinijibu hapana, bali ni mtu aliyemsaidia, nikamuuliza ni nani huyo?, ndipo alipomtaja Dr Bokko.

Basi akanitumia namba zake ambazo ni +255618536050, nilimpigia Dr Bokko na kuongea naye kwa undani zaidi kuhusu changamoto yangu, naye hakusita kunipa uhakika wa suluhisho.

Aliniambia ningoje ndani ya saa 48 nitakuwa nimepata majibu ya jambo hilo ila kabla hata ya saa 24 nilipigiwa simu na HR wa ofisi kwetu na kuniambia kuna barua ipo kwake kutoka kwa Bosi niende kuichukua.

Nilipofika na kukabidhiwa ile barua nilifungua na kukuta ni taarifa ya kuwa nimepandishwa cheo, ndani yake kulikuwa na mkataba mpya wa kazi ambao nilitakiwa kuusaini ili nianze kulipwa mshahara wa juu zaidi.

Nilisaini mara moja mkataba ule na kuurudisha kwa HR na kurudi nyumbani kupumzika kwani wiki inayofuata ningeanza majukumu mengine tofauti na yale ya awali.

Sasa ni takribani miezi 10 napokea mshahara mzuri katika cheo changu kipya na wala sijalala na Bosi kama alivyokuwa anataka yeye. Mpigie Dr Bokko kwa namba +255618536050.



Share:

Monday, 25 November 2024

WAANDISHI WA HABARI MANYARA NA UTPC WAANDAMANA UZINDUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI

WAANDISHI wa habari wa Mkoa wa Manyara na wafanyakazi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) wameongoza maandamano ya uzinduzi wa kampeni maalum ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Katika maandamano hayo yaliyoanza saa 2 asubuhi Novemba 25 mwaka 2024 katika kituo cha magari cha zamani Babati na kupita mitaa mbalimbali yalishirikisha pia makundi mbalimbali ikiwemo madereva wa bodaboda, wakulima, wafugaji, wanafunzi wa chuo cha Veta Manyara.

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari wa mkoa wa Manyara (NRPC) Jaliwason Jasson amesema maandamano hayo yakiongozwa na waandishi wa habari yamepitia maeneo ya barabara ya Arusha, Oysterbay, Ngarenaro na kumalizikia White Rose hoteli ili kusikiliza mada mbalimbali zitakazotolewa.

"Nawashukuru waandishi wa habari na wadau mbalimbali waliotuunga mkono katika kushiriki wakiwemo askari polisi wa kikosi cha usalama barabara waliosimamia ulinzi na usalama ili kusitokee ajali," amesema

Share:

TANI 2.2 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA TANGA, DAR ES SALAAM

Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo
Dawa za kulevya aina ya Skanka
Dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine



***
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 2,207.56 za dawa za kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Novemba 25, 2024, na Kamishina Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, miongoni mwa dawa zilizokamatwa ni skanka, methamphetamine, heroin, na dawa tiba aina ya Fentanyl. 

Amesema Dawa hizo zilipatikana katika operesheni maalum zilizofanyika katika maeneo tofauti na kwamba Watuhumiwa saba wanashikiliwa kuhusiana na dawa hizo.


 Ameongeza kuwa , Kati ya dawa zilizokamatwa, skanka ni kilogramu 1,500.6, methamphetamine kilogramu 687.76, heroin kilogramu 19.20, na chupa 10 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl. 

"Tarehe 14 Novemba, 2024, jijini Dar es Salaam, katika wilaya ya Kigamboni, mtaa wa Nyangwale, watuhumiwa Mohamed Suleiman Bakar (40) na Sullesh Said Mhailoh (36), wote wakazi wa Mabibo, Dar es Salaam, walikamatwa wakiwa na kilogramu 1,350.4 za dawa za kulevya aina ya skanka. 

Dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya nyumba aliyopanga mtuhumiwa Mohamed, ambayo aliitumia kama ghala la kuhifadhi dawa hizo. Aidha, dawa nyingine zilipatikana ndani ya gari aina ya Nissan Juke yenye namba za usajili T 534 EJC, zikiwa tayari kwa kusambazwa",ameeleza.

" Tarehe hiyo hiyo, katika mtaa wa Pweza Sinza E, wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, mtuhumiwa Iddy Mohamed Iddy (46), mkazi wa Chanika Buyuni, alikamatwa akiwa na kilogramu 150.2 za skanka, zilizokuwa zimefichwa katika maboksi ya sabuni na baadhi ya dawa hizo zikiwa zimefichwa kwenye boksi lililotengenezwa kwa bati ngumu na kupachikwa kwenye chassis ya gari aina ya Scania lenye namba za usajili wa Afrika Kusini LN87XJGP, ambalo limekuwa likitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi",ameongeza. 

Ameeleza kuwa vilevile, tarehe 17 Novemba, 2024, katika jiji la Tanga, watuhumiwa Ally Kassim Ally (52) na Fahadi Ally Kassim (36) walikamatwa mtaa wa Mwakibila wakiwa na kilogramu 706.96 za dawa aina ya heroin na methamphetamine. 

Baadhi ya dawa hizo zilipatikana ndani ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 714 EGX, huku nyingine zikibainika kufichwa kwenye nyumba aliyopanga mtuhumiwa. 

  Tarehe 19 Novemba, 2024, katika mtaa wa Kipata na Nyamwezi Kariakoo jijini Dar es Salaam, watuhumiwa Michael Dona Mziwanda (28) mkazi wa Tabata Segerea, na Tumpale Benard Mwasakila (32) mkazi wa Temeke Mikoroshini, walikamatwa wakiwa na chupa kumi za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl wakiwa nazo katika duka la M-PESA. 

Aidha, katika operesheni hizi zilizofanyika, jumla ya magari matatu na boti moja vilivyohusika katika uhalifu huo vinashikiliwa.

 Dawa zilizokamatwa ni nyingi na zingeweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii na taifa ikiwa zingeingia mitaani. 

Dawa hizi haziathiri tu wale waliokwisha anza matumizi ya dawa za kulevya, bali pia wafanyabiashara hawa hulenga watu wengine ambao hawajaanza matumizi ili kutanua masoko yao. Walengwa wapya wanaweza kuwa mtu yeyote katika jamii au familia za Kitanzania. 

Hivyo, ni dhahiri kuwa jamii nzima inakabiliwa na hatari ya dawa za kulevya. Kadhalika, Mamlaka imebaini kuwa wahusika wa biashara haramu ya dawa za kulevya hutumia mbinu ya kupanga nyumba ambazo zinageuzwa kuwa maghala ya kuhifadhi dawa za kulevya, huku wao wakiishi katika maeneo mengine. 

Mamlaka inatoa rai kwa wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyumba zao, kwani nyumba inayotumika kwa shughuli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa.

 Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95, imeweka katazo kwa mmiliki au msimamizi wa nyumba, msimamizi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike kwa lengo la kutengeneza, kuvuta, kujidunga, kuuza au kununua dawa za kulevya. 

Aidha, mmiliki anapojua kuwa kosa linatendeka kwenye eneo lake, anajukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka. 

Kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai, na akitiwa hatiani, adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia shilingi milioni tano hadi milioni hamsini, au kifungo cha miaka mitano hadi miaka thelathini jela, au vyote kwa pamoja. Mamlakaya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inatoa shukrani kwa wananchi wanaotoa ushirikiano kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na tunawahimiza wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini matukio yanayohusiana na biashara haramu ya dawa za kulevya. 






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger