Tuesday, 30 May 2023

WAZIRI GWAJIMA AMUAGA ALIYEKUWA MUWAKILISHI MKAZI WA UNICEF BI.SHALINI BAHUGUNA JIJINI DODOMA




Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameiongoza Menejimenti ya wizara hiyo kumuaga aliyekuwa muwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Shalini Bahuguna katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Waziri Dkt. Gwajima amemshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Wizara kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka 2023 alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika kuhakikisha ustawi na Maendeleo ya watoto Nchini.

Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametumia fursa hiyo kumkabidhi Bi. Shalini zawadi mbalimbali ikiwemo cheti cha kuthamini na kutambua mchango wake.

Kwa upande wake Bi. Shalin licha ya kuishukuru Wizara kwa ushirikiano, ameipongeza kwa utendaji, Ubunifu na uendeshaji wa weledi wa kwenye programu za mbalimbali katika kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la UNICEF Tanzania.

Share:

TUMIENI NJIA SAHIHI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI- PROF. MSHANDETE




Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa. Antony Mshandete akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati akifungua baraza hilo 26 Mei,2023 jijini Arusha.


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Suzana Augustino akifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa baraza la wafanyakazi lililofanyika 26 Mei, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo.


Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia wakiimbi wimbo wa mshikamano wakati wa uzinduzi wa baraza hilo tarehe 26 Mei,2023 Jijini Arusha.


Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Utafiti na Ubunifu Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa. Antony Mshandete ametoa wito kwa wajumbe wa wakilishi wa wafanyakazi katika baraza la wafanyakazi kutumia njia sahihi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Profesa Mshandete ameyasema hayo wakati akifungua na kuendesha mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Arusha.

"Rai yangu kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi ni kubuni njia zitakasaidia katika kuibua bunifu mbalimbali ili kuongeza mapato kupitia rasilimali zinazopatikana katika taasisi yetu" anasema Profesa Mshandete

Anaongeza kwa kueleza kauli mbiu ya chuo chetu ni Taaluma kwa Jamii na viwanda naamini wote tunaisimamia hii katika kuhakikisha tunatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii

Naye Mwakilishi wa Kamishina wa Kazi, Bw. Mussa Msami alisema ushirikiswaji wa wafanyakazi katika mambo yanayoendelea kufanywa na uongozi huleta umoja na hamasa mahala pa kazi hivyo kuchangia kuongeza ari ya ufanyaji kazi.


Aliongeza kwa kuaainisha majukumu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi ikiwemo utendaji kazi, uvumilivu, nidhamu na ubunifu kusaidia uongozi katika utendaji na kusisitiza taasisi itajengwa na watu wenye utu na ari.

Aidha Bw. Mussa ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela kwa kutenga siku maalumu ya uzinduzi wa baraza hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa THTU Taifa Bw. Paul Loisulie amewaasa wajumbe wa baraza hilo kuzingatia utunzaji wa siri za taasisi na kuepuka kutoa au kupokea taarifa kutoka kwenye vyombo visivyo rasmi.
Share:

WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI KAZI NA AJIRA SADC




Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameshiriki Kikao cha Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC kilichoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Gilbert F. Houngbo.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Mei, 2023 kwa njia ya mtandao ambapo kupitia kikao hicho wameweza kujadili baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na Bodi ya Magavana wa ILO mnamo mwezi Machi 2023 ambayo yatawasilishwa katika mkutano mkuu wa Shirika la Kazi Duniani utakaofanyika Juni 5 hadi 16, 2023 Geneva, Uswiss.

Masuala yaliyojadiliwa ni programu ya bajeti ya ILO kwa mwaka 2024/2025, hoja ya mabadiliko ya katiba ya ILO ili kuongeza demokrasia katika shirika hilo, ushirikishwaji wa wadau katika uendeshaji wa ILO kwa lengo ya kuongeza haki ya jamii na mapendekezo ya namna ya kuendesha vikao vya ILO vya kikanda.
Share:

KLABU YA KWANZA YA MKONGE YAZINDULIWA



Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) kwa kushirikiana na Shule ya Sekondari ya Coastal ya jijini Tanga, zimezindua Klabu ya Mkonge kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo imelenga kuwafundisha vijana kuhusu kilimo cha Mkonge na Sekta ya Mkonge kwa ujumla hatua itakayowawezesha kujiajiri baada ya kumaliza masomo.

Akizindua klabu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TSB, Saddy Kambona amesema wazo la kuanzisha klabu hiyo lilizaliwa kwenye Mahafali ya kidato ya shule hiyo Machi mwaka huu, lakini baadaye ikaonekana isiwe klabu kwa ajili ya Shule ya Coastal pekee bali ianzishwe klabu itakayoshirikisha shule zote za Tanga na vizazi vinavyokuja kushiriki kwenye uchumi huu wa mkonge.

Amesema kwa muda mrefu imezoelekea kwamba elimu yetu haimuandai mwanafunzi kwenda kujitegemea anapomaliza shule, wengi wamekuwa na mtazamo kuwa kazi ya kuajiririwa ndiyo inafaa.

“Kwa hiyo sisi tulitazama wazo la kuwa na klabu za Mkonge kwa maana kama tunasema Mkonge ni Tanga na Tanga ni Mkonge, basi tunataka mtu akifika Tanga aone kweli kama Mkonge ni Tanga, tunategemea aone kwamba Mkonge ndiyo zao kuu la kibiashara.

“Yaani kuanzia anatua uwanja wa ndege anapotua anaona bidhaa za Mkonge barabarani hadi anapofika hotelini anakutana na mazuria ya Mkonge na bidhaa nyingine. Sasa sehemu ya kuanzia ni kuwa na klabu za kuhamasisha si tu kilimo cha Mkonge bali  pia kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Mkonge lakini pia kushiriki kwenye kuzalisha hizo bidhaa.

“Baada ya hayo sasa Bodi inakuwezesha kupata elimu, utaalamu kuanzia shambani kulima Mkonge na uongezaji wa thamani, wataalamu wetu watatoa ujuzi huo kwa vijana wa Tanga na nje ya Tanga ili wanapomaliza shule huko wanakokwenda wakawafundishe na wengine,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Zao la Mkonge na Masoko, Olivo Mtung’e akizungumzia faida za Mkonge na somo la kuhamasisha wanachama wa klabu hiyo alisema mahitaji ya Mkonge kwa sasa yameongezeka ndiyo maana wanahamasisha wakulima kulima zao hilo.

“Nchi nyingi sasa zinahitaji Mkonge lakini kiasi ambacho tunakilima kwa sasa ni kidogo ndiyo maana baada ya kuingia kwenye kilimo cha wakulima wadogo sasa tunahamasisha na sisi kwenye familia zetu wenye mashamba ya eka moja hadi tatu walime Mkonge kwa sababu kwa sasa hali ya hewa inatusukuma kuelekea huko kwani zao la Mkonge linahimili hali za hew azote ili kuimarisha uchumi wa familia,” amesema.

Mkurugenzi Mtung’e anasema kutokana na hali hiyo, wahitimu hawana haja ya kutafuta ajira kwa sababu Mkonge wenyewe ni ajira kwani ukishapanda baada ya miaka mitatu unaanza kuvuna hadi kwa muda wa miaka 18.

Kwa upande wake mwanafunzi wa shule hiyo na mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, Fatuma Mshashi amesema klabu hiyo yenye wanachama 50 ambao kati yao wavulana ni 23 na wasichana 27, inatekeleza malengo mbalimbali ikiwamo kufanya tafiti kuhusu kilimo cha zao la Mkonge ili kuona faida zake, kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu, wadau wa elimu kuhusu umuhimu wa zao hilo, kuhamasisha jamii kutumia bidhaa za mkonge, kuwaandaa wanafunzi ili kuja kuwa wataalamu wazuri na wabobevu katika zao la Mkonge na nyingine nyingi.

“Ili kufanikisha malengo katika Klabu ya Mkonge katika shule yetu, tunaomba ofisi yako kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwalimu Mkuu itusaidie kukutanishwa na wataalamu wa zao la Mkonge ili kupata elimu na ujuzi wa zao hili, kuwezeshwa klabu kuwa na shamba darasa ambalo litakuwa la kujifunzia hatua zote za uandaaji hadi uvunaji ambapo shamba hilo mlitakuwa mradi wa klabu,” amesema.
Share:

Video Mpya : KISIMA - MAISHA

 

Share:

Monday, 29 May 2023

WADAU WA USAFIRI WA MAJINI KIBITI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA, ULINZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 




Na Mwandishi Wetu,Pwani

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania  (TASAC) limetoa elimu ya Usafiri Salama Majini kwa wadau mbalimbali wa wilaya ya Kibiti katika mialo ya Nyamisati Mkoani Pwani Mei 25 mwaka huu

Elimu hiyo iliyotolewa katika mialo iliyozunguka Nyamasati iliwajumuisha wavuvi, manahodha wa vyombo, wamiliki wa vyombo, wafanyabiashara na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri majini.

Katika utaoji wa elimu hiyo watoa  mada mbalimbali kutoka TASAC, TPA na BMU walitoa elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vya uokoaji pindi inapotokea dharura au ajali majini;  utumiaji vifaa vya uokoaji pamoja na matumizi ya kizimia moto (fire extinguisher) na umuhimu wa kuwa na kifaa hicho kwenye vyombo vidogo vya majini.

TASAC imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri majini kutoa elimu katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha wamiliki wa vyombo kuweka vifaa vya kujiokolea lakini pia manahodha na wavuvi kuvaa jaketi okozi wakati wote wawapo safarini au kuendesha shughuli za uvuvi.

Share:

WANANCHI WAHIMIZWA KUNUNUA BIDHAA ZILIZOTHIBITISHWA UBORA NA TBS

Afisa Udhibiti Ubora - Mwandamizi (TBS) Bw. Hamisi Simoni Seleleko, akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali waliotembelea banda la TBS katika Maonesho ya Sita (6) ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea Mkoani Kigoma.

********************

WANANCHI wamehimizwa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na kuhakikisha bidhaa wanazotumia hazijaisha muda wake wa matumizi.

Ushauri huo ulitolewa na Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa TBS, Bw.Hamis Seleleko, wakati wa Maonesho ya Sita ya Mifuko na Program za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yaliyofanyika mkoani Kigoma katika viwanja wa Mwanga Community Centre kuanzia Mei 21 hadi 28, mwaka huu.

Mbali na kuhimizwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo, wananchi waliohudhuria maonesho hayo wametahadharishwa kuhusiana na matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimepigwa marufuku kutumika nchini.

Aidha wananchi waliobahatika kufika kwenye banda la TBS kwenye maonesho hayo, walioneshwa mfano wa vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimekuwa na madhara ya kiafya kwa watumiaji.

"Wananchi wanapofika kwenye sehemu ambazo vipodozi vyenye viambata vya sumu vinauzwa wasisitize kutoa taarifa TBS, kwani watumiaji ndiyo wanaoathirika zaidi ." Amesema Bw.Seleleko

Pamoja na hayo Bw.Seleleko amesema kupitia maenesho hayo walipata nafasi ya kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia siku maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye maonesho hayo.

" Wajasiriamali walielimishwa kuhusu taratibu za kupata alama ya ubora ya TBS na mpango wa Serikali wa kuthibitisha ubora wa bidhaa kwa wajasiriamali hao bure kwa muda wa miaka mitatu," Amesema

Amesema TBS iliweza kufika kwenye mabanda ya washiriki wa maonesho hayo na kuzungumza nao na wale ambao wamethibitisha bidhaa zao na wale ambao bado ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kuwakwamisha kuthibitisha bidhaa zao.

"Lakini tumewapata taarifa kuhusiana na uwepo ofisi za shirika letu katika Kanda ya Magharibi ambayo ipo Kigoma, hivyo wakiwa na shida ni rahisi kufika hapo na kuweza kuhudumiwa," alisema.
Afisa Udhibiti Ubora - Mwandamizi (TBS) Bw. Hamisi Simoni Seleleko, akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali waliotembelea banda la TBS katika Maonesho ya Sita (6) ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea Mkoani Kigoma .
Mkurugenzi Mkuu (TBS)Dkt. Athuman Y. Ngenya ( wa Pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Meneja wa TBS kanda ya Magharibi Bw. Rodney Alananga (Watatu kushoto) pamoja na maafisa wa TBS alipotembelea maonesho ya 6 ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mwanga Community Center, Kigoma.
Share:

MCHENGERWA, WANANCHI WA VIJIJI VYENYE MIGOGORO YA MIPAKA HIFADHI YA SERENGETI WAYAJENGA, WAIPONGEZA SERIKALI, WATAKA USHIRIKISHWAJI.



Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya vikao na wananchi wa vijiji vyenye migogoro ya mipaka na Hifadhi ya Serengeti na kuutaka uongozi wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kuimarisha program za ujirani mwema na kuwashirikisha wananchi wanaozunguka hifadhi wakati wa kupanga mipango yao ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu kwenye uhifadhi wa raslimali hizo na kupunguza migogoro isiyo ya lazima.

Waziri Mchengerwa ametoa kauli hiyo Mei 28, 2023 wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Tarime na kufanya mikutano kwenye vijiji vyote vinavyozunguka Hifadhi ya Serengeti vilivyokuwa na migogoro na mipaka katika zoezi la uwekaji wa vigingi vya mipaka ambapo wananchi wa maeneo hao wamepongeza kwa hatua hiyo ya Serikali ya kuja na kuwasikiliza na kuahidi kushirikiana na Serikali kwenye uhifadhi.

Mhe. Mchengerwa aliambatana Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake Anderson Mutatembwa na Kamishna wa TANAPA, Afande William Mwakilema na kupokewa na uongozi wa Mkoa wa Mara, uongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime na Mbunge wa Tarime vijijini Mhe. Mwita Waitara ambapo katika mikutano hiyo yote Mhe. Mchengerwa aliongoza vikao hivyo kwa kuwapa wasaa wa wananchi kutoa maoni na mawazo yao na mwisho alitolea ufafanuzi wa hoja hizo na nyingine kuzichukua kwa hatua zaidi.

Wananchi wamepongeza hatua hiyo ya Waziri Mchengerwa kwenda na kuwasikiliza huku wakieleza kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mdogo na kuiomba Serikali kupanga kwa pamoja ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

Diwani wa kata ya Nyanungu Tiboche Richard amesema kuwa wananchi wa Kata yake wapo tayari kushirikiana na Serikali kwenye kila jambo endapo watashirikishwa na hifadhi.

“Mhe. Waziri napenda kukuhakikishia kuwa leo unatufanya tulale usingizi maana umetumwa na Mhe. Rais wetu kuja kutujengea mahusiano mazuri, na sisi hiki ndicho tulichokuwa tunakikosa.” Amesisitiza diwani Richard

Akiwa kwenye mkutano katika Kijiji cha Karakatonga wilayani Tarime, Mhe. Mchengerwa ameutaka uongozi wa TANAPA kushuka chini kwa wananchi na kwenda kuzungumza nao kwa kuwa hifadhi hizo ni za wananchi na wananchi ndiyo wahifadhi namba moja.
Aidha, amesema wazo la uhifadhi wa raslimali katika taifa la Tanzania limeasisiwa miaka mingi ambapo uongozi katika awamu zote toka enzi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Samia Suluhu Hassan limezingatiwa kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

Akiwa kwenye Kijiji cha Kegonga, Mhe. Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi hao kushirikiana na uongozi wa Serikali wakati wote na kuacha tabia za kugomea kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanachochea migogoro.
“Kwa hiyo wanapokuja viongozi wa Serikali kuja kujadili mpango wa matumizi bora ya ardhi wasikilizeni msikatae kusikiliza, shaurini tufanye nini.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Amewataka kutambua kuwa wahifadhi ni sehemu ya jamii yao kwa kuwa baadhi ya watumishi hao ni sehemu ya familia zao na watoto wao.
Share:

AMUUA BABA YAKE KISHA KUMPIKA KAMA MBOGA


Mwanaume mmoja kutoka kijiji cha Giankaja, kaunti ya Tharaka Nithi alitiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumuua baba yake na kupika sehemu za mwili wake.

Mwanamume huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya.

Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha wakisema mwathiriwa ambaye ni mzee mwenye umri wa miaka 70, aliripotiwa kutoweka kwa siku tatu. Msako ulifanyika katika kijiji kizima na wakazi wa eneo hilo katika juhudi za kumtafuta mzee huyo.

Baada ya saa kadhaa za msako, upekuzi wao uliwaelekeza kwenye mtaro wenye kina kirefu ambapo waliupata mwili wa marehemu ambao tayari ulikuwa umeshaanza kuoza. 

Marehemu alikuwa amekatwa kichwa na sehemu za mwili wake kukatwa na miguu yake ikiwa kando ya mwili wake. Walikimbia haraka kwa chifu wa eneo hilo ili kumjulisha kuwa wamempata mtu aliyepotea. Hata hivyo, waliporejea kwenye mtaro, mwili huo haukuonekana.

Wakiwa wamechanganyikiwa na jinsi mambo yalivyobadilika, wenyeji hao katika udadisi wao pamoja na polisi na chifu walitafuta ndani zaidi ya mtaro. 

Walizunguka kwenye mtaro wa kina kirefu uliowaelekeza kwenye nyumba ambayo polisi wanasema huenda ilikuwa ya mshukiwa.

 Walipofika katika nyumba hiyo, walishangaa kupata chungu cha kupikia kimejaa nyama na mboga.

 Katika eneo la tukio, kulikuwa na fuvu la kichwa cha binadamu na nguo zilizojaa damu pamoja na viatu vya marehemu. 

Polisi walimhoji mshukiwa huyo kuhusu aliko baba yake lakini alibaini kuwa pia alikuwa hafahamu kwa kuwa anaendelea kumtafuta.

Sehemu nyingine za mwili zilizopotea ambazo ziligunduliwa kwanza na wenyeji zilipatikana zikiwa zimetupwa kwenye gunia na kufunikwa kwa mawe ndani ya Mto Nithi.

 Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye alidai kuwa mshukiwa huyo alianza kuchimba mtaro huo mwaka 2017, alieleza kuwa mshukiwa na mwathiriwa wake walizozana kuhusu hali ya mtaro huo kabla ya kupotea.

 "Wawili hao walizozana baada ya mwanaume huyo kumzuia babake kukata nyasi za Napier kuzunguka mtaro," Johnson Mutembei mkazi aliambia jarida moja la eneo hilo.

Kwa sasa mshukiwa yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Chanzo- Tuko News
Share:

DAWA SAHIHI YA SHINIKIZO LA DAMU NA SUKARI


Isingekuwa shida sisi kama familia tusingemjua daktari bingwa BAKONGWA aliyemtibia baba yetu ugonjwa wa sukari ya kupanda na shinikizo la damu ambalo kwa hakika hospitali walituhakikishia kuwa baba yetu asingeweza kuishi zaidi ya miezi kumi kisha kufariki.

Familia yetu yenye kulelewa na baba aliyekuwa akifanya kazi serikalini haikuzijua shida wala njaa kama wengi walivyopitia changamoto.

Hali hii ilibadilika ghafla tulipo pata taarifa za baba kuanguka na kushindwa kufanya majukumu yake ya kila siku huko ofisini kwake Jijini Dar es salaam.Watoaji wa huduma za kwanza hapo kazini walimpeleka hospitali mara mmoja na kumpa huduma kisha vipimo vilifuata vilivyoonesha kuwa baba anashida ya sukari na shinikizo la damu la muda mrefu.

Haya yote baba aliyajua lakini aliyafanya siri akihofia kuwa tungeyajua mapema nguzo ya familia ingedondoka, alichokihofia sasa kilikuwa kimefika ugonjwa ule ulimsumbua baba kwa muda wa miaka nane bila ya kumfahamisha yeyote pale nyumbani.

Madaktari bingwa wa muhimbili walisisitiza kuwa hakuna cha kufanya zadi ya mionzi ya chemo na vidonge baadhi vya kumpa nguvu akingoja miezi hiyo kumi na kufariki.

Tulihangaika sana kubadili madaktari kila kona kwa muda wa miezi saba ikiwa ni miezi mitatu tu imebaki baba atutoke kama walivyosema madaktari lakini bado hatukupata msaada.

Mtumishi mmoja wa serikalini Bugando aliiona hofu ya familia yetu kumpoteza baba na kutuambia kuwa tujaribu njia nyingine kwa kuwa hizi za kiofisi tayari zimekuwa na kikomo cha muda.

Alitupatia nambari za whatsapp +243990627777 na tovuti zake pia https://bakongwadoctors.com na kusisitiza tumtafute.Tulifanya hilo mapema sana kwa kuhofia kumpoteza baba na mara tulipompata daktari akatuanzishia dawa iliyomtaka baba atumie siku mbili mfululizo.

Mara baada ya kutumia dawa jambo la ajabu sana tulishangaa kuona baba ameanza kutembea na kurejea kwenye shughuli zake za kila siku.Tunashukuru sana daktari kwa msaada wa kumponya baba yetu mpendwa.


Share:

ALIYEMPIGA NA KUMNG'OA JINO, KUMTOBOA JICHO MKEWE AKAMATWA ARUSHA



Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha Mei 27, 2023 limefanikiwa kumtamata mtuhumiwa aitwaye Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mke wake aitwaye Jackline Mkonyi (38) mkazi wa Sombetini jijini humo.

Akitoa taarifa hiyo  Mei 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa huko katika maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na wanaendelea kumhoji na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.

Lakini pia amewaomba wananchi popote walipo wasifumbie macho vitendo viovu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao ili kukomesha matukio hayo katika jamii.

Share:

MAJERUHI 18 WAMERUHUSIWA HOSPITALI YA TEMEKE KUFUATIA AJALI UWANJA WA MKAPA



Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewajulia hali majeruhi 10 wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya Temeke waliojeruhiwa kutokana na tukio la kukanyagana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wakijiandaa kuingia kutazama mechi kati ya Yanga na USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa Kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliochezwa Mei 28, 2023.

Mhe. Chana alipokea taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Gasper Kimaro kwamba, walipokea majeruhi 30 ambapo wanaume walikua 18, Wanawake 10 na mtoto Mmoja ambapo mgonjwa mmoja alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.

Ameeleza kuwa mpaka sasa wamebakiwa na wagonjwa 10 na wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.


Mhe. Chana katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu, Bw. Saidi Yakubu, Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwanahamisi Munkunda.
Share:

Sunday, 28 May 2023

Video : MAMA USHAURI - MAGEREZA

Share:

Video : MAMA USHAURI - CAROLINA

Share:

YANGA SC YACHAPWA 2-1NA USM ALGER FAINALI YA KWANZA CAFCC



*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wao USM Alger ya nchini Algeria baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali ya kwanza CAFCC ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Licha Yanga kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza waliruhusu bao la mapema kupitia kwa mshambuliaji Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo,bao ambalo liliwapeleka mpumziko USM Alger wakiwa mbele 1-0.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutengeneza nafasi nyingi kwaajili ya kusawazisha bao bila mafanikio hivyo kocha akalazimika kufanya mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwa kuwaingiza baadhi ya wachezaji wakiwemo Morisson, Salum Aboubakar, Djuma Shaban na Lomalisa Mutambala ambapowaliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele, goli likitengenezwa na Morisson dakika ya 82.

Baada ya Yanga kupata bao, USM Alger waliweza kuongeza bao dakika mbili mbele kupitia kwa nyota wao Islam Merili dakika ya 84.
Share:

PROF. NDALICHAKO : BILIONI 3 ZIMETOLEWA KUJENGA VYUO VITATU VYA WATU WENYE ULEMAVU 




Na Mwandishi Wetu, Kasulu 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako amesema Sh.Bilioni tatu zimetolewa na serikali kwa ajili ya kujenga vyuo vitatu vya watu wenye ulemavu na utegamano. Vyuo hivyo vinajengwa na serikali kupitia Ofisi hiyo kwenye Mikoa ya Songwe, Ruvuma na Kigoma na tayari kila chuo kimepewa Sh.Bilioni moja ili kujenga madarasa, mabweni na nyumba za walimu. Akizungumza Mei 27, 2023 alipokagua ujenzi wa chuo kinachojengwa eneo la Nyumbigwa, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambacho ni miongoni mwa vyuo hivyo, Prof.Ndalichako amesema kujengwa kwa vyuo hivyo ni msisitizo wa serikali kwenye mafunzo ya ujuzi kwa watu wenye ulemavu.

“Nimshukuru kwa dhati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kusogeza huduma kwa jamii katika maeneo muhimu. Tuna chuo cha mazoezi Kabanga kina wanafunzi wengi wenye ulemavu,”amesema.

Share:

SEHEMU ZANGU ZA SIRI ZIMEVIMBA BAADA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Hapo Januari mwaka huu, kuna familia ilihamia karibu na mahali nilipokuwa naishi, ghafla nikagundua mke wa jirani yangu yule ni mrembo sana, mtoto ni kisu kweli kweli, unaweza kutokwa na udenda, kidume yoyote yule ni lazima tu angemtamani.

Mume wake ni Afisa wa Polisi na mwanamke huyo ni mfanyakazi katika bandari ya Mombasa, basi tukaanza urafiki kama majirani, wote walinichukulia kama ndugu yao na mara kadhaa nilienda nyumbani kwao kwa ajili ya maongezi.

Nilizoeana na mke wa bwana yule hadi ikafikia hatua ambayo nilianza kupika chakula kila nilipoenda kwenye nyumba yao, haikuchukua muda mimi na mwanamke yule tukaanza kutamaniana kimapenzi.

Tulibadilishana namba za simu na hapo tukaanza kutumiana jumbe za kimapenzi kila mara kwani mapenzi yalikua yamenoga baina yetu, huku mume wake akiwa hajui lolote.

Alhamisi moja bwana mwenye nyumba alitumwa katika maeneo ya Msambweni kwa ajili usalama, ilikuwa ni fursa nzuri kwangu kwenda katika nyumba yake ile kupiga stori na mke wake kama ilivyokua kawaida yangu. Nilipofika ndani ya nyumba ile, nilimkuta mke yule amevalia nguo za kulalia, hapo mwili wangu ukawaka sana hisia.

Tulizungumza kwa muda wa dakika 20 hivi kisha akanza kunipapasa kwa mikono yake iliyolainika, nilifahamu kuwa maishani fursa kama hiyo huwa inakuja mara moja tu, hivyo nikaamua kumega tunda la mwenzangu kwa raha zangu mwenyewe.

Jumamosi asubuhi nilishtushwa usingizini na maumivu niliyokuwa nahisi katika sehemu zangu za siri, nilisema labda maumivu yale yanatokana na nguvu nyingi ambazo nilitumia katika tendo lile na jirani yangu.

Lakini siku zilivyozidi kwenda maumivu nayo yalizidi kuwa makali, hapo ndipo nilipogundua kuwa mume wake alikua ametumia dawa ya kumkinga mke wake asiweze kufanya mapenzi na mwanaume mwingine yoyote yule nje ya ndoa yao.

Nilishindwa hata kutembea kwani sehemu zangu za siri zilikuwa zimevimba sana huku maumivu yakiwa yakutisha, niliamua kuwasiliana na African Doctors kuomba msaada, akaniambia kuwa mume wa mwanamke yule alikuwa amemkinga mke wake na yeye ndiye aliyemuokea kinga hiyo!. 

Alinishauri niende kwa bwana yule ambaye anaitwa Rashid ili nimuombe msamaha kwa yale niliyafanya kwani yeye African Doctors kama mtaalam ndiye alikuwa mshauri wake wa jambo hilo.

Nilikumbwa na msongo wa mawazo na hapo nikachanganyikiwa nikifikiria naanzaje kwenda kuomba msamaha, wakati ule sikuwa hata na uwezo wa kutembea kwani sehemu zangu za siri zilikua zimevimba sana.

Nilipiga moyo konde na kwenda kuomba msamaha kwa bwana Rashid, nashukuru alinisamehe ila aliniamuru nimpigie African Doctors kwanza, nilizungumza naye na kunitoza Ksh30,000 kama faini ya kosa lile na siku iliyofuata mambo yakarudi kama ilivyokuwa kawaida. 

African Doctors anatibu kaswende, kifua kikuu, pia anasuluhisha migogoro ya ndoa, kuinua biashara, kukusaidia kupata kazi, kupanda cheo kazini, kuongezwa mshahara na mengine mengi.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger