Friday, 30 August 2019

MTOTO MWINGINE ALIYEANGUKIWA NA BOMBA LA MAJI AFARIKI DUNIA


Mfano wa Bomba lililomwangukia mtoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Brnabas Mwakalukwa, amesema kuwa mtoto aliyeangukiwa na bomba kubwa la maji mkoani humo, amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kiyungi iliyopo Manispaa ya Tabora, alipata majeraha siku ya Agosti 28 baada ya kuangukiwa na bomba kubwa la kupitisha maji, walipokuwa wakicheza na wenzao hali iliyopelekea mtoto mwenzake kufariki muda huo huo.

''Yule mtoto aliyelazwa ICU walifanya utaratibu wa kumpeleka Bugando lakini bahati mbaya akafariki njiani maeneo ya Nzega, na daktari akathibitisha kufariki kwake'' amesema ACP Mwakalukwa.

Mabomba yaliyosababisha madhira hayo ni ya mradi mpya wa usambazaji wa maji mkoani humo kutoka Ziwa Victoria, yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye kiwanja cha shule hiyo.
Share:

Job opportunities at I&M Bank

Information Security Officer l&M Bank (T) Ltd, a subsidiary of l&M Group which has presence in Kenya, Tanzania, Rwanda and Mauritius invites applications from suitably qualified candidates to fill the following available positions. JOB TITLE:  INFORMATION SECURITY OFFICER REPORTS TO:  HEAD OF RISK JOB PURPOSE: Protecting organization’s computers, networks and data against threats, such as security breaches, computer viruses… Read More »

The post Job opportunities at I&M Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi za kazi TADEPA- Jobs at TADEPA August 2019

Information about TADEPA Tanzania Development and AIDS Prevention Association (TADEPA) is a Tanzanian Nongovernmental organization (NGO) currently offices in Kagera, Geita, Shinyanga and Dodoma regions. Was formed and registered in 1997 and acquired mandated to work in all regions of Tanzania mainland. The main purpose of TADEPA is to promote development in totality through and fight against public… Read More »

The post Nafasi za kazi TADEPA- Jobs at TADEPA August 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at Vodacom, Head of Revenue Assurance

Head of Revenue Assurance   Role purpose: The key purpose of the Head of Revenue Assurance is to ensure completeness and accuracy of the company revenue streams across CBU, EBU and M-Pesa Units. In addition to checking on the integrity of systems in place, the position requires an inclination towards continuous improvements in revenue chain, proactive design and implementation… Read More »

The post Job Opportunity at Vodacom, Head of Revenue Assurance appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunity at NETIS Tanzania, Project Sheq officer

JOB TITLE: Project Sheq officer INDUSTRY: Telecommunication LOCATION: Dar es Salaam. ROLE PURPOSE To ensure that NETIS’s Quality, Safety, Health, Social, Security, Cultural, Environmental and Risk Management systems are defined, implemented, maintained and adhered to according to best practice standards at all levels of the organisation within Tanzania. KEY PEFORMANCE AREAS Document and communicate all SHERQ manuals and policies… Read More »

The post Job Opportunity at NETIS Tanzania, Project Sheq officer appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

11 Job Vacancies at BAK-AID Tanzania

EXCITING CAREER OPPORTUNITIES OVERVIEW BAKWATA NATIONAL HIV/AIDS PROGRAM (BAK-AIDS) is a Faith Based Organization (FBO) implementing HIV programs to support Tanzania Government efforts to reduce the rate of HIV pandemic in Tanzania. Since inception, BAK-AIDS has played a big role in supporting Tanzania’s social development initiatives by implementing health programs which include HIV and AIDS education and other… Read More »

The post 11 Job Vacancies at BAK-AID Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wizara ya elimu (MOE): Commonwealth scholarships tenable in the United Kingdom 2020

Wizara ya elimu (MOE): Commonwealth scholarships tenable in the United Kingdom 2020: scholarships for tanzanians to study in tanzania, how to apply for commonwealth scholarship, commonwealth scholarship 2019/2020, tanzania scholarship 2019, how to apply for commonwealth scholarship 2019, what is commonwealth scholarship, commonwealth scholarship 2020, commonwealth scholarship application portal. The Ministry of Education, Science, and Technology as a… Read More »

The post Wizara ya elimu (MOE): Commonwealth scholarships tenable in the United Kingdom 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ardhi University- How to confirm selection 2020- Maelekezo jinsi ya kuthibitisha udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja

Ardhi University- How to confirm selection 2020- Maelekezo jinsi ya kuthibitisha udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja- Ardhi University (ARU) 2019. The Ardhi University (ARU) was established after transforming the former University College of Lands and Architectural Studies (UCLAS) which was then a constituent college of the University of Dar es Salaam from 1st July 1996. The… Read More »

The post Ardhi University- How to confirm selection 2020- Maelekezo jinsi ya kuthibitisha udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ardhi University 2nd Round selection release date

Ardhi University 2nd Round selection release date 2019 The Ardhi University (ARU) was established after transforming the former University College of Lands and Architectural Studies (UCLAS) which was then a constituent college of the University of Dar es Salaam from 1st July 1996. The history of Ardhi University, however, dates back to 1956 when the then Surveying Training… Read More »

The post Ardhi University 2nd Round selection release date appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi 61 za kazi Muhimbili National Hospital

Job opportunities at Muhimbili National Hospita (MNH) VACANCIES ANNOUNCEMENT AT MNH On behalf of the Muhimbili National Hospital (MNH), Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 61 vacant posts as mentioned below. A tertiary specialised and super specialist Hospital in Tanzania organized into nine directorates with bed capacity of 2,178 out of which 1,570 beds are… Read More »

The post Nafasi 61 za kazi Muhimbili National Hospital appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAUMINI WASUSIA IBADA WAKIDAI PASTA MGENI BADO MBICHI HAJAOA 'ATAHARIBU BINTI ZAO'

Kisanga cha aina yake kimezuka katika kanisa moja la Gachororo, kaunti ya Kiambu nchini Kenya baada ya washirika kukosa kuhudhuria ibada wakidai pasta mgeni aliyetumwa kuwahudumia hakuwa na mke. 

Kondoo hao walisema kwamba, mtumishi alikuwa barobaro mwenye umri mdogo na kudai huenda alikuwa na njama fiche kanisani humo. 

Kwa mujibu wa Taifa Leo, washirika hao walianza kuondoka kanisani mmoja baada ya mwingine pindi tu mtumishi huyo aliposimama na kujitambulisha. 

Penyenye zinaarifu kwamba washirika hao walielezea wasiwasi wao kuhusu umri mdogo wa pasta kwani walihofia huenda akawa tishio kwa mabinti zao.

"Hata hajaoa. Mabinti zetu wataponea kweli. Huyu hapana. Huyu ni pasta hatari," washirika walisikika wakiteta.

 Inasemekana, pasta alijaribu kuwatuliza washirika hao na kuwaambia nia yake pale ilikuwa ni kueneza ijili ya Bwana na wala sio mambo mengine.

"Hayo hayawezekani. Nyinyi ni kama mnafanya biashara na kanisa. Rudi kwenu ukomae kwanza," mshirika mmoja alimfokea mchungaji. 

Duru zinaarifu kwamba, mtumishi huyo alikuwa amepewa uhamisho hadi tawi la kanisa hilo na kutoka alikokuwa akihubiri. 

Jaribilo la wazee wa kanisa kutuliza hali lilizua mzozo mkali huku waumini wakiwafokea na kuwataka kumshauri barobaro huyo kutafuta kazi nyingine ya kufanya na wala sio kuchunga kondoo. 

Penyenye zinaarifu kwamba, washiriki hao walimpa pasta muda wa siku mbili kusanya virago na kurejea alikotoka mara moja. 

 "Sisi hapa hatutaki kesi na wewe. Wasichana wetu wangali shuleni. Damu yako jinsi tunavyoiona ingali moto. Jipange uende kuhubiri kanisa lingine," waumini walizidi kumuonya pasta.

 Inadaiwa wazee walinza kuondoka mmoja baada ya mwingine na kumwacha pasta pekee yake baada ya kushindwa kudhibiti hali kanisani.
Share:

WADAU WA NAFAKA WAKUTANA DAR KUJADILI FURSA


 Wadau wa mazao ya nafaka, wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhate Hasunga wakati akihutubia mkutano wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi  kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam 
 Mhe. Waziri Hasunga.
 Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano huo.
 Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
 Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storagefacilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
 Bi. Margareth Nzuki (katikati), akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Dkt. Bunogelo kuhusu utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses)
.

 Mkuurgenzi Mtednaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Japhet Justine akipiga makofi wakati mkutano huo ukiendelea.
 Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
  Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
 Bi.Margareth Nzuki (kushoto), kutoka ESRF akibadilishana mawazo na Bi. Vumilia L. Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo wakati wa mkutano huo.
 Mshiriki akitoa maoni yake.
 Oswald Mashindani (kushoto), kutoka ESRF akizunhumza jambo mbele ya Katibu Mkuu (mstaafu) Wizxara ya Fedha, Bw. Paniel Lyimo (katikati) wakati wa mkutano huo.
 Mhe. Hadsunga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na manaibu waziri makatibu wakuu na Mwenyekiti wa TPSF.
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
***
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MKUTANO wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi umefunguliwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2019.

Mkutano huo ambao umewajumuisha wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa maghala ya nafaka Lengo lake ni kuangalia fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi ya kuzifikia ikiwa ni pamoja na masoko.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo uliowakutanisha wadau kutoka mikoa mbalimbali  nchini, Mhe. Hasunga ambaye alifuatana na Manaibu wake, Mhe. Husein Bashe, na Mhe. Omary Mgumba alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kuelimishwa kuhusu fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika, uwezo wa Tanzania kuzalisha na nafasi ya wafanyabiashara kushiriki kikamilifu lakini pia washiriki watapata fursa ya kujifunza athari za upotevu wa mazao ya nafaka baada yamavuno na mkakati wa serikali kudhibidi hali hiyo.

“Kitaalamu wanasema utafiti uliofanyika Tanzania na  nchi nyingi za Kusini asilimia 40 ya mazao yote yakiwemo ya nafaka yanapotea baada ya mavuno kwa kuharibika na matatizo mengine, hii haikubaliki mkulima amewekeza, amevuna halavu mazao yake yanaharibika, lazima tuwe na mkakati wa kuzuia hali hii.” Alitoa hakikisho Mhe. Waziri Hasunga na kuongeza.

Kulingana na uzalishaji uliopo, nafaka nyingi kama mahindi mtama na nafaka nyingine huhifadhiwa katika kiwango kisichoridhisha hali hii huchangia kupoteza ubora wa nafaka na hatimaye huchangia kuzorota kwa ustawi wa afya zetu, alifafanua zaidi Mheshimiwa Waziri.

Alisema Agosti 1, mwaka huu kwenye sherehe za Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganow a Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati wa namna ya kupambana na kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Katika utafiti wake ilioufanya hivi karibuni Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya Mradi wa Rapid Response Implementation Support to the Ministry of Agriculture and Agriculture Sector Lead Ministry (RARIS) unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation umebaini kuwa hali ya maghala mengi ya watu binafsi hayatoi taarifa serikalini na hii ni kutokana na mfumo wa sasa wa maghala.

Akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses), Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt.Hoseana Lunogelo alisema ESRF ilifanya utafiti wa hali (status) ya maghala nchini na kubaini kuwa maghala ya watu binafsi hayalazimiki kisheria kutoa taarifa serikalini kuhusu nini kimehifadhiwa na kiasi gani cha nafaka kilichohifadhiwa ndani ya maghala hayo na hali hii serikali inategemea tu maghala ya Serikali yaani (Public Storage Facilities ) kupitia Werehouse Reseat Regulatory Board ili kujua takwimu za hali ya chakula nchini.

“Kwa sasa kuna maghala 3,430 yaliyopo kati ya hayo ni 185 tu ndiyo kuna uhakika wa kupata tawimu endapo zitahitajika lakini yaliyosalia huwezi kupata takwimu hizo kwa sababu hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo.” Alifafanua Dkt. Lunogelo.

Alisema hii ni changamoto kubwa, kama serikali inapata taarifa kutoka kwenye maghala machache sana nchini na yale mengi haipati taarifa zake, maana yake Serikali haiwezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na upatikanaji wa chakula nchini na hiyo ina athari mbaya kwenye usalama wa chakula na pia ina athari mbaya pia kwenye biashara.” Alsiema Dkt. Lunogelo.
Share:

AMUOMBA MSAMAHA MAGUFULI BAADA KUUA MKEWE KWA KUMCHOMA VISU KISHA KUJIUA KWA KUJIKATA KOROMEO


Jovither Kaijage, Ukerewe
Mkazi wa Kijiji cha Kagera wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, Celestin Masatu (39) amejichoma kisu tumboni, kujikata kolomeo na kufa baada ya kumfanyia ukatili mkewe Jenifa Julias (30) wa kumchanachana mwilini na kisu, huku akiacha ujumbe akiomba msamaha kwa Rais John Magufuli kwa kitendo alichokifanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 7.15 usiku, katika nyumba ya kulala wageni ya Emma iliyoko eneo la kata ya Nakatungulu mjini Nansio.

Alisema baada ya kumchoma visu mkewe na baadaye kujichoma kisu na kujikata koromeo, majeruhi hao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya mjini Nansio usiku huo huo ili kupatiwa matibabu lakini Masatu alipoteza maisha asubuhi siku iliyofuata wakati mkewe akihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Kamanda huyo alisema kabla ya kujidhuru kwa kujichoma na kisu tumboni, kisha kukatakata utumbo wake na baadaye kolomeo, Masatu alimchoma visu tumboni na shingoni mkewe na kusababisha utumbo na mfuko wa kizazi uliokuwa na mtoto mchanga wa miezi miwili kutoka nje.

Alisema wawili hao, awali waliwahi kuishi pamoja kama mme na mke na walijaliwa kupata watoto wawili kabla ya mwanamke kuamua kuondoka na vifaa vya nyumbani na kwenda kuishi peke yake katika kijiji cha Bukongo.

Alisema hata hivyo katika siku za hivi karibuni walirejesha mahusiano yao ya ndoa na hadi siku hiyo ya tukio walikubaliana wakutane lakini kumbe mwanaume alikuwa na mpango wa kumdhuru mwenzake kwa sababu ya wivu wa mapenzi.

Baada ya Polisi kufanya upekuzi kwenye chumba walichofikia, mbali ya kupata kisu kilichotumika kuwadhuru na vitu vyao vingine kama nguo na viatu, pia lilipatikana daftari lenye maandishi yanayosadikika kuandikwa na Masatu akiomba msahama kwa Rais Magufuli kwa kosa alilolifanya na mgawanyo wa mali zake.

“Sehemu ya barua hiyo imeandikwa hivi, nanuku: ‘Naomba radhi kwa serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kitendo nilitakachofanya kwa hiari yangu.’ Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Emma, Musiba Mayunga alisema alishitushwa na kelele za mwanamke akiomba msaada usiku wa manane na alipowataka wafungue mlango, mwanaume alikataa ndipo aliomba msaada wa uongozi wa kitongoji na Polisi.

Alisema kelele hizo ziliwaamusha wageni wengine waliofikia kwenye nyumba yake na ndio waliofanikiwa kuvunja mlango wa chumba na kuwatoa wanandoa hao wakiwa na majeraha.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Sokoni, Kata ya Nakatungulu, Celestin Mangwesa alisema baada ya kujulishwa na kufika eneo la tukio, alishuhudia mwanamke akitoka nje ya chumba utumbo ukiwa nje. Alisema mwanaume aligoma kutoka hadi Polisi walipowasili na kuamua kuingia ndani ndipo akatolewa akiwa amepoteza fahamu kutokana na majeraha makubwa aliyokuwanayo.
Share:

MAHAKAMA YAELEZWA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA KAPOOZA MGUU,ANA SHIDA YA KUPUMUA

Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulielekeza Jeshi la Magereza mteja wao kwenda kupimwa katika hospitali ya Serikali.

Wakili wa utetezi, Jebra Kambole amedai leo Ijumaa Agosti 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili Kambole amedai usiku wa kuamkia Agosti 2, 2019 mteja wake akiwa gerezani alianza kuumwa na hadi leo ana shida ya kupumua.

"Nilienda kumuona nikakuta amepooza mguu na kushindwa kutembea kwa siku mbili pamoja na kuishiwa nguvu, sisi kama mawakili na ndugu hatujui nini anachoumwa."

"Kwa kuwa mteja wetu hajapata vipimo ambavyo vinastahili tunaomba Mahakama ielekeze Jeshi la Magereza mteja wetu akapimwe katika hospitali yoyote ya serikali ikiwemo Muhimbili penye vipimo vya uhakika," amedai Wakili Kambole

Wakili Wakyo amedai swala la ugonjwa hakuna mtu anayeweza kupingana nalo lakini huwezi kulielekeza Jeshi la Magereza kwenda kumpima katika hospitali fulani.

"Mahakama yako haiwezi kuamuru kupelekwa hospitali fulani kwa kuwa hajawahi kuwasilisha maombi akakataliwa lakini sheria inasema makosa ya uhujumu uchumi yanasikilizwa na Mahakama Kuu hivyo Mahakama hii haina uwezo wa kutoa uamuzi wowote" ameeleza Wakili Wankyo

Via Mwananchi
Share:

Rais Magufuli Atoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni za kuamini kuwa watawala wa zamani wa Mataifa ya Afrika ndio wenye uwezo wa kusaidia kusimamia na kuendeleza rasilimali zilipo katika Bara la Afrika.

Rais Magufuli ametoa wito huo jana Ikulu alipohutubia Mkutano wa 6 wa Jukwaa la Uongozi Afrika unaohudhuriwa na Marais Wastaafu Benjamin William Mkapa (Tanzania), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Hassan Mohamud (Somalia), Hery Rajaonarimampianina (Madagascar), Mabalozi, Wawakilishi wa Kimataifa na washiriki wa Jukwaa la Uongozi Afrika.

“Maana hasa ya kupigania uhuru ilikuwa ni kurejesha rasilimali na hasa maliasili zetu lakini pia kuwa na maamuzi kamili kuhusu namna ya kuzisimamia na kuzitumia kwa manufaa yetu ili kuleta ukombozi wa kiuchumi, na hii ndio maana pekee ya kulinda uhuru wa kisiasa” Rais Magufuli

Tusijidanganye watawala wetu wa zamani hawawezi kugeuka kwa usiku mmoja na kuwa wajomba zetu au wakombozi wetu kiuchumi, utegemezi huu ndio umeimarisha mizizi na misingi ya ukoloni mamboleo, ni lazima tuamke” Rais Magufuli.


Share:

TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA AGOSTI 30,2019

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, hatosaini kuongeza mkataba wake hivi sasa na anataka kujiunga na Real Madrid haraka iwezekanavyo. (Marca)

Paris St-Germain inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27, kama mchezaji atakayeichukua nafasi ya mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, anayekaribia kurudi Barcelona. (Le Parisien)

Bayer Leverkusen inataka kumsaini beki wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Ubelgiji Jan Vertonghen, aliye na miaka 32, kabla ya kuwadia Jumatatu muda wa mwisho wa dirisha la uhamisho Ulaya. (Kicker)

Beki kamili wa Manchester United na timu ya taifa ya Italia Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, yupo katika majadiliano kurudi katika ligi ya Serie A na klabu ya Parma. (La Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na timu ya taifa ya Misri Mohamed Elneny, aliye na miaka 27, yupo katika mazungumzo na timu ya Uturuki Besiktas kuhusu uhamisho wa msimu mzima kwa mkopo (Sky Sports)
Meneja wa Gunners Unai Emery anasema beki kamili mwenye umri wa miaka 33 Nacho Monreal, aliyehusishwa na uhamisho kwenda Real Sociedad, huenda akaondoka katika klabu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Mirror)

Bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasua sua kumuita mlinzi wa timu ya taifa ya Ivory Coast Serge Aurier kwa Derby ya London kaskazini siku ya Jumapili huko Arsenal wakati mchezaji huyo wa miaka 26 akiwa anaweza kuondoka kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu. (Evening Standard)

Manchester United ilijitoa katika mkataba wa msimu wa joto ya mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kutokana na matakwa ya malipo ya mchezaji huyo wa Argentina ya thamani ya £18m kwa mwaka. (Mail)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26, amepunguza uzito wa mwili baada ya kufuata muongozo wa lishe chini ya meneja Antonio Conte tangu raia huyo wa Ubelgiji kujiunga na Inter Milan. (Mail)

Mlinzi wa Barcelona Gerard Pique anatumai kuwa Harry Maguire ataweza kuisaidia klabu yake ya zamani Manchester United kushinda taji la ligi kuu ya England. (Express)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Aaron Tshibola amejiunga na timu ya Ubelgiji Waasland-Beveren kwa mkataba wa miaka mitatu. (Birmingham Mail)

Arsenal dhidi ya Tottenham inajitayarisha kuipiku Liverpool dhidi ya Everton katika mchezo mkali wa Derby katika ligi kuu ya England. (Sun)

Kipa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, mwenye umri wa miaka 26, amekubali kujiunga na Real Madrid. (RMC Sport)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, ametuma ujumbe kwa wachezaji wenzake wa Manchester United katika Instagram kabla ya kujiunga na Inter Milan kwa mkopo. (Manchester Evening News)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)

Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)

Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo - huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)
Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)
Chanzo - BBC
Share:

MAREHEMU ALIYEZIKWA NA TAI,VIATU AZUA BALAA.....'ANATAKA AZIKWE UPYA'

Huenda familia moja kutoka eneo la Ikolomani, kaunti ya Kakamega nchini Kenya ikafukua maiti ya jamaa wao waliyemzika kufuatia ripoti kwamba alikuwa anawahangaisha kwa kutozingatia utaratibu wakati wa mazishi yake.

 Inasemekana marehemu Pius Shipanda Shitsukane, ambaye alihudumu kama naibu wa chifu katika mtaa wa Shiseso na aliyezikwa hizi majuzi, amekuwa akiwahangaisha jamaa zake na kutaka mwili wake ufukuliwe. 

Inaelezwa kuwa Mkewe Shipanda amekuwa akiugua tangu kuzikwa kwa mumewe na wazee wa jamii wamedai maradhi yanayomkumba yamesababishwa na gadhabu ya mumewe.

Pius Shipanda alidaiwa kuzikwa akiwa amevishwa viatu na tai kinyume na mila na desturi za jamii ambapo baadhi ya jamaa wa familia hiyo walidai wamekuwa wakikumbwa na masaibu katika nyumba yao tangu jamaa huyo azikwe.

Duru zinaarifu kwamba, marehemu alivishwa viatu na tai na kisha rungu ambayo alipenda kutembea nayo haswa wakati akihudhuria vikao vya wanaume wa kikatoliki ikatiwa katika sanduku lake kabla ya kuzikwa.

 Pindi tu baada ya mazishi yake katika boma lake kijijini Ikhumbula-Ibukhubi, mkewe alianza kuugua na kulazwa hospitalini.

 Hata hivyo, wakazi wanaamini chifu huyo ndiye chanzo cha mkewe kuugua kwa kuwa alikuwa hajafurahishwa na mazishi yake. 

 "Ni kinyume na mila za jamii ya Luhya kumzika marehemu na bidhaa kama vile tai, saa, pesa, shanga, chupi au soski," Lawrence Alusiola ambaye ni mzee wa jamii alisema.

 Alisema wale wote ambao wamekiuka tamaduni hiyo wamepokea adhabu na kulazimika kuufukua mwili ili kuondoa vifaa alivyozikwa navyo marehemu. 

 "Tumeshuhudia visa kama hivyo kwa miaka ya hapo awali. Unapata familia inakiuka desturi zetu na kusisitiza kuwazika wapendwa wao jinsi wanavyotaka kisha wanajuta baadaye wakati wanapotatizwa na marehemu," Elias Khwani mzee mwingine kutoka jamii hiyo alisema.

 Inadaiwa, marehemu Shipanda amekuwa akiwatatatiza jamaa wa familia yake haswa nyakati za usiku akitaka tai, viatu na rungu aliyozikwa navyo ziondolewe.

"Maradhia ambayo yamemkumba mkewe ghafla yanahusikana na marehemu kwa kuwa baadhi ya wanachama wa kikundi cha wanaume wa kikatoliki walikataa kusikiza ushauri wa wazee na kumzika marehemu na bidhaa zisizostahili. Ni sharti waufukue mwili au familia itazidi kuhangaika," mzee mwingine wa jamii alitoa tahadhari. 
Via Tuko
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger