Saturday, 30 July 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.
"Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa.
"Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa" Amesema Rais Magufuli.
Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.
Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.
Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Singida
29 Julai, 2016
Audio: Msikilize Rais Magufuli Akizungumzia Jinsi Atakavyoyapiga Mnada Majengo ya Serikali Dar na Atakachofanya Kwa Watumishi Watakaokataa Kuhama
Rais John Magufuli amesema azma ya Serikali yake kuhamia Dodoma haraka iwezekanavyo ipo pale pale huku akiwaonya wale wataong'ang'ania kubaki Dar es Salaaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.
Alitoa msimamo huo mjini Singida jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.
Alisema kuwa licha ya kuhamia Dodoma atahakikisha anauza majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam kwa mnada ili wale wasiotaka kuhama,wahame kwa lazima.
DOWNLOAD HAPA>>>>>http://music.audiomack.com/tracks/mpekuzi-blog/kauli-ya-rais-magufuli-kuhusu-watumishi-watakaokataa-kuhamia-dodoma.mp3?Expires=1469860388&Signature=Tkt1fHvqeGAnYia4-kHzhc1T-R8eNf0nlhlMBBcBJi1Ggz87PO18Q7gLHu5ceVeTdixLL67tIxDVhe1Mo9gTweZkfczrehg~VHg9zkterVlLJU0fwv7ODqwpx1dO~~EjgaoPNi9S7JHKDZQk9S0EYS97TueHMQV3TqLKhl4FXE4_&Key-Pair-Id=APKAIKAIRXBA2H7FXITA
DOWNLOAD HAPA>>>>>>http://music.audiomack.com/tracks/mpekuzi-blog/kauli-ya-rais-magufuli-kuhusu-watumishi-watakaokataa-kuhamia-dodoma-1.mp3?Expires=1469860577&Signature=elpI6pFvDo~PaFI-Bsi4neQOUsQkqJmL4nIPRbUc-ROSODHG1gcPNsQFF-GZGEDEp5K8se5BgfXuw4w87-TKm4ZPBDF8JffkXswzOo9otcmqG-xC-t6ftiVKEuqwgHyimSN35bQlAuvefxQtjIVSlomaSHXpgdnSTvWgULhNlhM_&Key-Pair-Id=APKAIKAIRXBA2H7FXITA
Friday, 29 July 2016
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SABABU ZA KUTOKUCHAGULIWA KWA BAADHI YA WALIOOMBA KUDAHILIWA KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SABABU ZA KUTOKUCHAGULIWA KWA BAADHI YA WALIOOMBA KUDAHILIWA
KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017Baraza linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa kuna baadhi ya waombaji ambao hawakuchaguliwa kwenye uteuzi wa kwanza ambao ulitolewa tarehe 22 Julai 2016.
Mwombaji ambae hakuchaguliwa hupaswa kuangalia kwenye kurasa yake binafsi (profile) ili kupata sababu za kutokuchaguliwa. Sababu za kutokuchaguliwa zinaweza zikawa kama ifuatavyo:
1. Sifa za muombaji kuwa pungufu kulinganisha na sifa za chini za kozi;
2. Nafasi za mafunzo katika chuo na kozi husika kujaa kutokana na ushindani wa waombaji wenye sifa za juu zaidi.
3. Kutokamilisha ujazaji wa maombi kwenye mfumo;
4. Kutoambatanisha vyeti vya masomo kwa baadhi ya waombaji; na
Waombaji wanashauriwa kusoma kwa
makini sababu hizo na kufuata ushauri unaotolewa ili kuweza kuchaguliwa
katika uteuzi unaofuata.Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu. Orodha ya kozi zilizojaa zimeainishwa hapa
.
Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 28 Julai, 2016
Taarifa kwa Wanafunzi Wote Kuhusu tarehe ya Kufungua Chuo sekta ya uvuvi Tanzania bara 2016/2017
Taarifa kwa Wanafunzi Wote Kuhusu Kufungua Chuo
Kurugenzi ya Mafunzo na
Utafiti Inapenda Kuwatangazia Wanafunzi Wote wa Wakala Wa Elimu na
Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwamba, Tarehe ya Kufungua Chuo Imebadilishwa
tena na Hivyo kwa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza (New Comers) Pamoja na
Wale Wanaotarajia Kufanya Mitihani ya Supplementary na Mitihani Maalum
(Special Exams) Wataripoti Kuanzia Siku ya Jumatatu ya Tarehe 29 Mwezi
Agosti. Aidha Wanafunzi Wanaoendelea Wao wataripoti chuo Kuanzia
Jumatatu ya Tarehe 5 Mwezi wa Septemba. Tunaomba Radhi sana Kwa Usumbufu
Wote Ambao utajitokeza.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mafunzo na Utafiti
28/07/2016
MPYA:NAFASI ZA KAZI SUA-FRESH GRADUATE FROM SUA WANAHITAJIKA HARAKA SANA
Fresh graduates required
The School of Agricultural Economics and Business Studies (SAEBS) at the Sokoine University of Agriculture
(SUA) is looking for fresh graduates in BSc Agricultural Economics,
Agri-business Management or any other Agriculture-related disciplines
with some experience in rural households’ data collection to be engaged
for a short-term data collection assignment.
Qualified candidates should send in their application to the email address saebs@suanet.ac.tz copied to amakyoo@yahoo.co.uk ; zekenya@yahoo.com and indicate “ENUMERATOR” in the subject line. Applications can also be dropped at the School’s offices at the New Agribusiness Incubator building off Morogoro – Iringa Highway Road in the main campus, Morogoro Municipality. Applicants must include a cover letter, CV and academic and professional certificates. Application must be received by Friday, 5th
Bingwa wa kubikiri Wasichana Nchini Malawi abainika ana UKIMWI........Rais Aamuru Akamatwe Haraka
Rais wa Malawi, Peter Mutharika juzi alitoa amri ya kukamatwa kwa Eric Aniva ambaye hivi karibuni alibainika kufanya kibarua cha kuwabikiri mabinti wa chini ya umri wa miaka 13 zaidi ya 100.
Amri hiyo ya Rais imekuja baada ya kubainika kuwa mwanamume huyo maarufu kwa jina la ‘Fisi’ anaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Mutharika alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.
Mutharika alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.
Aniva
aliingia matatani baada ya kukiri katika mahojiano akijinasibu kuwa
anaendesha maisha kwa kuwabikiri mabinti na kwamba hulipwa kuanzia dola
nne za Marekani mpaka saba ambayo ni wastani wa Sh10,000 kwa kila mtu.
Mwanamume huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na tambiko.
Mwanamume huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na tambiko.
Waombaji wa Mikopo Elimu ya juu Wafikia 69,820 Mpaka Sasa
JUMLA ya wanafunzi 69,820 wameomba mikopo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) hadi sasa ikiwa zimebaki siku tatu kufikia mwisho wa kupokea maombi hayo.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa
bodi hiyo, Cosmas Mwaisoga, alisema mwaka jana walioomba kupewa mikopo
walikuwa 65,000, hivyo waombaji wa mwaka huu wameongezeka.
Mwaisoga
alisema tofauti na awali, mchakato wa sasa wa kuomba unafanyika kwa
njia ya mtandao na baada ya kutumwa kwao, watayapitia na kwa yale yenye
kasoro, wahusika wataitwa ili wayarekebishe.
Alisema dirisha la uombaji wa mikopo linatarajia kufungwa Jumapili hii.
Katika hatua nyingine, alisema idadi ya wanaorejesha mikopo imeongezeka maradufu baada ya kutakiwa kufanya hivyo.
“Kwa
sasa ni vigumu kutaja idadi yao kwa sababu huwa tunaitoa mwishoni mwa
mwezi kwa hiyo kesho tutakuwa na idadi kamili ya waliorejesha, lakini
ikilinganishwa na huko nyuma, sasa hivi mwitiko wa wanaorejesha
umeongezeka,” alisema.
Mwaisoga
alisema sheria inamtaka aliyekopa aanze kurejesha baada ya mwaka mmoja
wa kuhitimu masomo yake, lakini anapochelewesha, kila mwaka kunakuwa na
penati ya ongezeko la asilimia sita.