Thursday, 14 November 2024

BENKI KUU YA TANZANIA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA

...

 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog                                         

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeendesha semina kwa waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha umma kuhusu majukumu ya benki hiyo na masuala ya kifedha muhimu kwa taifa.

Semina hiyo ya siku mbili inafanyika katika Ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza, na inahusisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mara na Geita.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo,ameeleza kuwa, mafunzo hayo yatagusia masuala muhimu kama vile muundo na majukumu ya Benki Kuu, maana ya sera ya fedha inayotumia riba ya Benki Kuu, umuhimu wa dhahabu kama sehemu ya akiba ya fedha za kigeni, na utekelezaji wa sheria na kanuni zinazohusu huduma ndogo za fedha.

Aidha, Mwaikambo amesema mada nyingine itahusu ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kuondoa noti za zamani kutoka mzunguko, alama za usalama wa fedha na utunzaji wake, pamoja na mtazamo wa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania.

Semina hii inatoa fursa kwa waandishi wa habari kuwa na uelewa wa kina kuhusu masuala ya kifedha na sera za Benki Kuu, ili waweze kutoa taarifa sahihi na za kitaalamu kwa umma, hivyo kusaidia kuongeza ufanisi katika ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi za kifedha.

Mkurugenzi wa BOT Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa leo Jumatano Novemba 14,2024 katika ukumbi wa BOT Tawi la Mwanza - Picha na Kadama Malunde

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger