Monday, 24 April 2023

WAUMINI ZAIDI YA 20 WAJIUA KWA NJAA WAKIFUNGA BILA KULA WALA KUNYWA MFULULIZO...MCHUNGAJI ALIWAHADAA WAKIFA WATAONANA NA YESU

...
Jeshi la Polisi nchini Kenya wamefukua miili ya watu zaidi ya 20 ambao ni waumini wa kanisa la News International Church, ambao inadaiwa wamefariki dunia kwa njaa baada ya kufuata maelekezo ya mchungaji wao ya kufunga mfululizo.


Mchungaji Paul Makenzie Nthenge ndiye anayedaiwa kuwapa maelekezo hayo waumini wake, ikidaiwa kwamba aliwaambia wakifunga mfululizo, wataenda kuonana ana kwa ana na Yesu.

Tayari mchungaji huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo huku taarifa zikieleza kwamba huenda makaburi mengine yakabainika.


Makachero ambao walifika Malindi eneo la Shakahola wamepata makaburi zaidi katika msitu ambao washirika wa kanisa waliambiwa wafunge hadi kufariki dunia.

Makachero walifika eneo hilo kuwaokoa washirika wa kanisa la Good News International chini ya mhubiri Paul Mackenzie na sasa wamepata makaburi zaidi.
Kufikia sasa makachero wanasema watu watatu, akiwamo msichana wa miaka 16, waliokolewa na kufikishwa hospitali kupokea matibabu. Sasa ripoti zinasema kuwa jumla ya makaburi 27 yameweza kutambuliwa na maswali kuzuka kuhusu watu waliofariki dunia kufikia sasa.


Inaarifiwa wanaochunguza kisa hicho wameweza kupata taarifa muhimu kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Mackenzie ambao wameokolewa. 

Kwa mujibu wa afisa wa watoto eneo la Pwani George Migosi, washirika wa kanisa hilo walikuwa wafunge hadi kufariki wakianza na watoto, kisha kina mama na hatimaye wanaume.

 Sasa maswali yameibuka ni vipi mhubiri aliwachukua washirika wake na kuwapumbaza hadi wakapoteza maisha yao.
Maswali yanayoibuka ni kuhusu ilipokuwa serikali wakati huu ambapo washirika walikuwa kwenye msitu. "Chifu na asasi zingine za serikali walikuwa wapi wakati huu wote wa pasta kuwauzia washirika ajenda za kupotosha," mmoja wa wakazi alisema. 

Maombi hayo yalikuwa yakifanywa kwenye msitu mmoja eneo la Kilifi.


Makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamefukua miili mingi katika Msitu wa Shakahola, Kilifi, inayoaminika kuwa ya wafuasi wa mchungaji tata Paul Mackenzie.


Katika zoezi hilo la Jumapili, Aprili 23, miili sita ilipatikana kwa mara ya kwanza kwenye makaburi matatu yenye kina kirefu.

Kaburi moja lilikuwa na miili mitatu, jingine lilikuwa na miwili na la tatu lilikuwa na moja. Saa chache baadaye, miili 12 zaidi ilipatikana katika makaburi saba, na hivyo kuongeza idadi ya mateka wa mchungaji huo kufikia 39.


Polisi sasa wametangaza boma la kiongozi wa ibada Mackenzie kuwa kaburi la pamoja. Wakati wa uchimbaji, mwanamke mmoja aliokolewa katika moja ya maficho na inasemekana alikuwa katika hali mbaya. Licha ya kuchungulia kifo, alidokezea polisi kwamba hataki kuokolewa. 

Kama ilivyoripotiwa awali, Pasta Mackenzie anatuhumiwa kushawishi waumini wake kufunga, bila kula wala kunywa chochote akiwahadaa kwamba wakifa wataonana na Yesu.

Mnamo Ijumaa, Aprili 21, wapelelezi wa DCI walianza kuweka alama kwenye makaburi na kufukua miili ya watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wake wanaoaminika kujiua kwa njaa. Wakati wakiwaokoa wafuasi wa Mackenzie katika msitu wa Shakahola, wapelelezi hao walipatana na makaburi 12 ambayo hayakuwa na alama. Wapelelezi hao pia waliwaokoa watu wengine watatu miongoni mwao, msichana mwenye umri wa miaka 16, ambaye alikimbizwa hospitalini kwa matibabu. Wapelelezi hao pia waliwaokoa watu wengine watatu miongoni mwao, msichana mwenye umri wa miaka 16 ambaye alikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger