Friday, 14 October 2022

Picha : MBIO ZA BAISKELI ZATIKISA SHINYANGA, CRDB YAKUSANYA UNIT 391 ZA DAMU, WASHINDI HAWA HAPA

...

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli Km 150 Shinyanga - Isaka Boniphace Ngwata akiwasili katika eneo la Kambarage baada ya kukimbia kwa muda wa saa 4 na dakika 5.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limefanikisha kupatikana kwa Unit 391 za damu salama huku washindi 40 wakiondoka na zawadi nono ya shilingi 6,450,000/=.

Tamasha hilo limefanyika leo Ijumaa Oktoba 14,2022 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga likiongozwa na Kauli mbiu ‘Shinyanga Yetu, Damu Yetu’ ambapo mgeni rasmi alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Shinyanga, Joel Daudi Mbale Unit 391 za damu salama zimepatikana kupitia Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB ikiwa ni asilimia 78.2% ya malengo ya Benki ya CRDB iliyojiwekea kwani matarajio yalikuwa ni kupata Unit 500.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (katikati), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (kushoto) na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) wakichangia damu salama katika uwanja wa CCM Kambarage.

Tamasha la Mbio za Baiskeli limeshuhudiwa na mamia ya wananchi na wapenzi na mbio za baiskeli mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani ambapo zaidi ya wachezaji wa baiskeli 275 wameshiriki mbio hizo.

Katibu wa Chama cha Waendesha Baiskeli Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ndembi Tuma amesema waendesha baiskeli wabobevu walioshiriki mbio za kilomita 150 kutoka Kambarage Mjini Shinyanga hadi Isaka (Km 75 kwenda, 75 kurudi) wameanza mbio saa 2:43 asubuhi na kumaliza mbio saa 6:48 mchana wakitumia muda wa saa 4 na dakika 5 ikiwa ni kasi kubwa zaidi ukilinganisha na mwaka jana (2021) ambapo walikimbia kilomita 150 kwa muda wa saa 5 na dakika 50.

Akizungumzia kuhusu zawadi na washindi wa mbio za baiskeli, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui amesema katika kundi la Wabobevu wa baiskeli waliokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) kwa muda wa saa 4 na dakika 5 mshindi wa kwanza ni Boniphace Ngwata aliyeondoka na medali ya dhahabu na kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,500,000/= , mshindi wa pili ni Dotto Mahega aliyepata zawadi ya Sh. 1,000,000/= na wa tatu ni Kashinje Kapemba aliyepata sh. 500,000/=.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli Km 150 Shinyanga - Isaka Boniphace Ngwata akiwasili katika eneo la Kambarage baada ya kukimbia kwa muda wa saa 4 na dakika 5.

"Katika kundi hilo, George Zengo ameshika nafasi ya nne na kuondoka na zawadi ya sh. 300,000/=, Kulwa Gelard mshindi wa tano aliyepata sh. 200,000/=, nafasi ya 6 ni Mungu ataleta sh.50,000/=, 7 Makoja Hamis – 50,000/=, 8 Malaika Leonard – 50,000/=, 9 Gelard Konda – 50,000/=, 10 Masunga Duba – 50,000/= na washindi kuanzia nafasi ya 11 hadi 20 wote wameondoka na zawadi ya shilingi 20,000/= kila mmoja ambao ni 11 Amos George, 12 Said Kulwa, 13 Kulwa Mahega,14 Richard Charles, 15 Frank Malki, 16 Peter Ishudu, 17 Mwigulu Mdogo, 18 Jagard Gelard, 19 Kulwa Ntyuki na 20 Paul Mahega",ameeleza Pamui.

Katika kundi la Vijana waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60 mshindi ni Frank Kichuya aliyeondoka na zawadi ya medali ya dhahabu na shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Kadochiza Amos zawadi y ash. 300,000/=,mshindi wa tatu Simon George sh. 200,000/= wa nne Masele Kichuya sh. 100,000/=, wa tano Gidson Mzuzu sh. 50,000/= na washindi wa nafasi ya 6 hadi 10 wakipata zawadi ya sh. 20,000/= kila mmoja ambao ni 6 Mzanzibar Dotto, 7 Moshi Mahega, 8 Joseph Paschal, 9 Askari Mahega na 10 ni Alfunne Kilimanja.

Pamui amesema kwa upande wa kundi la wanawake waendesha baiskeli ambao wamezunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40 mshindi wa kwanza ambaye ni Kipepeo Futimbili amepata zawadi ya shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Makilikili Joseph sh. 300,000/=, wa tatu ni Modesta Kashinje sh ,200,000/=, mshindi wa nne ni Maria Mwigulu sh. 100,000/=, wa tano ni Femineta Charles sh. 50,000/= na washindi wa 6 hadi 10 wameondoka na kifuta jasho cha shilingi 20,000/= kila mmoja ambao ni 6 Pili Hamis, 7 Schola Omary, 8 Kang’wa Joseph, 9 Stela Clement na 10 Maria Robert.
Wanawake waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40.

Tamasha hilo limeenda sanjari na bonanza la mpira wa miguu kati ya CRDB Digital FC na SHUWASA ambapo SHUWASA wameibuka washindi kwa bao 1-0 na kuondoka na zawadi ya sh. 100,000/= na cheti huku SHYCOM wakitoka sare ya magoli 3-3 na JAMBO na kuondoka na zawadi ya shilingi 75,000/= na cheti kila mmoja wakati huo huo CRDB Digital Queens ikiicharaza Shycom magoli 34 kwa 4 na kuondoka na zawadi ya sh. 50,000/= na cheti.

Katika Tamasha hilo wanafunzi wa shule ya Sekondari Uhuru Elizabeth Joshua na Ibrahim Jumanne Kagong’wa wameondoka na kitita cha sh. 100,000/= kila mmoja na kutokana na kuwa mstari wa mbele kuchangia damu mara kwa mara.

Pamui amesema Benki ya CRDB inaendelea kuunga mkono juhudi za Chama Tawala (Chama cha Mapinduzi CCM) na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na michezo akiongeza kuwa huu ni mwaka wa tano imekuwa ikiandaa tamasha la michezo ili kuhamasisha uchangiaji damu salama.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ameishukuru na kuipongeza Benki ya CRDB kuandaa Tamasha la Mbio za Baiskeli ili kuunga mkono maendeleo katika sekta ya afya kwa kuhamasisha uchangiaji damu salama kwa ajili ya wahitaji wa damu wakiwemo akina mama wajawazito na watoto katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga huku akiwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu na kufanya mazoezi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi amepongeza Benki ya CRDB kwa kuwa wazalendo na kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mbio hizo za baiskeli zimetanguliwa na Mazoezi ya kukimbia ‘Jogging’, mazoezi ya viungo ‘Aerobics’ yakiongozwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Mbali na Benki ya CRDB kuandaa Tamasha la Mbio za Baiskeli, wadhamini wenza ni Kampuni ya Jambo Food Products, Gaki Investment Co. Ltd na Fresho Investment Co. ltd.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizindua Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB leo Ijumaa Oktoba 14,2022. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Kaimu RTO Mkoa wa Shinyanga ACP, Dezidery Kaigwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Katibu wa Chama cha Waendesha Baiskeli Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ndembi Tuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Wabobevu wa baiskeli wakiwa katika eneo la Kambarage Mjini Shinyanga wakijiandaa kuanza kukimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) ambapo mshindi wa kwanza ni Boniphace Ngwata aliyeondoka na medali ya dhahabu na kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,500,000/= , mshindi wa pili ni Dotto Mahega aliyepata zawadi ya Sh. 1,000,000/= na wa tatu ni Kashinje Kapemba aliyepata sh. 500,000/=.
Viongozi mbalimbali wakipiga picha ya kumbukumbu na Waendesha baiskeli waliokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka)
Waendesha baiskeli wakianza kukimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka)
Waendesha baiskeli wakianza kukimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka)
Waendesha baiskeli wakianza kukimbia kilomita 150 kutoka Shinyanga hadi Isaka
Mashabiki wa mbio za Baiskeli wakiwa katika eneo la Kambarage Mjini Shinyanga wakisubiri kuona mshindi wa mbio za baiskeli kilomita 150 kutoka Shinyanga hadi Isaka na kurudi tena Shinyanga
Mashabiki wa mbio za Baiskeli wakiwa katika eneo la Kambarage Mjini Shinyanga wakisubiri kuona mshindi wa mbio za baiskeli kilomita 150 kutoka Shinyanga hadi Isaka

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli Shinyanga - Isaka Boniphace Ngwata akiwasili katika eneo la Kambarage baada ya kukimbia kwa muda wa saa 4 na dakika 5 na kuondoka na zawadi nono kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,500,000/= , mshindi wa pili ni Dotto Mahega aliyepata zawadi ya Sh. 1,000,000/= na wa tatu ni Kashinje Kapemba aliyepata sh. 500,000/=.
Wachezaji wa Baiskeli wakiwasili katika eneo la Kambarage baada ya kukimbia kwa muda wa saa 4 na dakika 5 mbio za kilomita 150 Shinyanga- Isaka/Isaka - Shinyanga
Mashabiki wa mbio za Baiskeli wakiwa katika eneo la Kambarage Mjini Shinyanga wakiwa katika eneo la Kambarage Mjini Shinyanga wakiwapokea washindi wa mbio za baiskeli kilomita 150 kutoka Shinyanga hadi Isaka na kurudi tena Shinyanga.

Kundi la Vijana waendesha baiskeli wakijiandaa kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60.
Kundi la Vijana waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60
Kundi la Vijana waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60
Kundi la Vijana waendesha baiskeli wakimaliza kuzunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60 ambapo aliyeibuka mshindi ni Frank Kichuya aliyeondoka na zawadi ya medali ya dhahabu na shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Kadochiza Amos zawadi y ash. 300,000/=,mshindi wa tatu Simon George sh. 200,000/=
Wanawake waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40 ambapo mshindi wa kwanza ambaye ni Kipepeo Futimbili (aliyevaa nguo nyekundu) amepata zawadi ya shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Makilikili Joseph sh. 300,000/=, wa tatu ni Modesta Kashinje sh ,200,000/=
Wanawake waendesha baiskeli wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40.
Mshindi wa kwanza Kipepeo Futimbili kundi la wanawake waendesha baiskeli akimaliza kuzungumka uwanja wa CCM Kambarage mara 40 na kuondoka na zawadi ya shilingi 500,000/=.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (katikati), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (kushoto) na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) wakichangia damu salama katika uwanja wa CCM Kambarage
Wadau wakichangia damu salama katika uwanja wa CCM Kambarage. Kushoto ni Mchoma Chips Maarufu Mjini Shinyanga Juma Chips akifuatiwa na Mhamasishaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo Mjini Shinyanga, maarufu Toffee Up Town
Wadau wakichangia damu salama katika uwanja wa CCM Kambarage
Wadau wakichangia damu salama katika uwanja wa CCM Kambarage
Huduma za Kibenki zikiendelea kutolewa katika uwanja wa CCM Kambarage
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Katibu wa Chama cha Waendesha Baiskeli Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ndembi Tuma akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Shinyanga, Joel Daudi Mbale akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Mtaalamu wa afya, Moris Mwita akitoa elimu kwa wananchi kuhusu Ugonjwa wa Ebola wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza wakati wa Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Boniphace Ngwata kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,500,000/= baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wabobevu wa baiskeli waliokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) kwa muda wa saa 4 na dakika 5.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Dotto Mahega kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/= baada ya kuibuka mshindi wa pili katika kundi la Wabobevu wa baiskeli waliokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) kwa muda wa saa 4 na dakika 5.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Kashinje Kapemba kitita cha pesa taslimu kiasi cha shilingi 500,000/= baada ya kuibuka mshindi wa tatu katika kundi la Wabobevu wa baiskeli waliokimbia kilomita 150 (Shinyanga- Isaka) kwa muda wa saa 4 na dakika 5.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Kipepeo Futimbili zawadi ya shilingi 500,000/= ambaye ni mshindi wa kwanza kundi la Wanawake waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Makilikili Joseph zawadi ya shilingi 300,000/= ambaye ni mshindi wa pili kundi la Wanawake waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Modesta Kashinje zawadi ya shilingi 200,000/= ambaye ni mshindi wa tatu kundi la Wanawake waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 40.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Frank Kichuya zawadi ya shilingi 500,000/= aliyeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Vijana waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Kadochiza Amos zawadi ya shilingi 300,000/= aliyeibuka mshindi wa pili katika kundi la Vijana waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimvalisha medali ya dhahabu na kumkabidhi Simon George zawadi ya shilingi 200,000/= aliyeibuka mshindi wa tatu katika kundi la Vijana waendesha baiskeli waliozunguka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara 60.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimkabidhi cheti na fedha shilingi 100,000/= mwanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru Ibrahim Jumanne Kagong’wa kutokana na kuwa mstari wa mbele kuchangia damu salama mara kwa mara.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akimkabidhi cheti na fedha shilingi 100,000/= mwanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru, Elizabeth Joshua kutokana na kuwa mstari wa mbele kuchangia damu salama mara kwa mara.
Burudani ikiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage
Wadau wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Wadau wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Wadau wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Maafisa kutoka Benki ya CRDB Makao Makuu wakiwa katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Wadau wakifanya Mazoezi ya kukimbia ‘Jogging’ kutoka eneo la Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kuelekea kwenye uwanja wa CCM Kambarage ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Wadau wakifanya Mazoezi ya kukimbia ‘Jogging’ kuelekea kwenye uwanja wa CCM Kambarage ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Wadau wakiwa katika benki ya CRDB Tawi la Shinyanga wakati wakifanya Mazoezi ya kukimbia ‘Jogging’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB

Wadau wakifanya mazoezi ya viungo ‘Aerobics’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui
Wadau wakifanya mazoezi ya viungo ‘Aerobics’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB

Wadau wakifanya mazoezi ya viungo ‘Aerobics’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Wadau wakifanya mazoezi ya viungo ‘Aerobics’ ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Tamasha la Mbio za Baiskeli lililoandaliwa na Benki ya CRDB.
Mtanange ukiendelea kati ya SHYCOM na JAMBO ambapo walitoka sare ya kufungana magoli 3-3
Mchezo ukiendelea kati ya CRDB Digital Queens na Shycom ambapo CRDB Digital Queens iliicharaza Shycom magoli 34 kwa 4
Kikosi cha mpira wa miguu SHUWASA
Kikosi cha mpira wa miguu CRDB Digital
Mchezo wa mpira wa miguu kati ya CRDB Digital FC na SHUWASA ukiendelea ambapo SHUWASA wameibuka washindi kwa bao 1-0
Picha ya kumbukumbu baada ya Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB
Viongozi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja baada ya Tamasha la Mbio za Baiskeli Shinyanga lililoandaliwa na Benki ya CRDB leo Ijumaa Oktoba 14,2022.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger