Saturday, 9 July 2022

WANAJESHI WAWILI WAFARIKI AJALI YA GARI KUPINDUKA KIGOMA

...


Mabaki ya gari ya jeshi iliyosababisha vifo vya wanajeshi wawili na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kupinduka katika eneo la Kidahwe halmashauri ya wilaya Kigoma.
(Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Askari wawili wa jeshi la wananchi wa Tanzania wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa vibaya kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kuachia njia na kupinduka.


Kaimu Kamanda wa polisi mkoawa Kigoma,Menrad Sindani akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mapema leo  amesema kuwa ajali hiyo imetokea eneo la kijiji cha Kidahwe wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma jana mchana.


Ameitaja gari  iliyopata ajali kuwa ni aina ya Toyota Land Cruiser Hard top lenye namba za usajili 3186 JW 9768 la kikosi cha 825 JKT Mtabila wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.


Kamanda Sindani amewataja waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Havent Michael (31) na Nicholaus Mbinda (31) ambao walifariki wakikimbizwa hospitali ya wilaya mkoa Kigoma Maweni.


Aidha Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma amewataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa Andrea Mathayo (32), Manyama Karilo (32), Ngongolina Julius (19) na Ramadhani Kapile  Dereva wa gari lililopata ajali.


"Kwa sasa miili ya marehemu ipo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa Kigoma Maweni na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo huku taratibu zikifanywa kuwapeleka majeruhi hospitali ya jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam,"Alisema Kamanda Sindani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger