Mume wa umri wa miaka 53 aliyapandwa na mori amemuua jamaa mwenye umri wa miaka 35 baada ya kumpata akirarua tunda lake.
Ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ilifichua Edwin Komen aliuawa kwa kukatwakatwa Alhamisi, Machi 31, usiku huko Ukwala, Keringet, kaunti ndogo ya Kuresoi Kusini.
Kisa hicho kilitokea baada ya jamaa ambaye jina lake halikutajwa kumpiga mwanaume huyo akijivinjari na mkewe nyumbani kwake.
“Akiwa na hasira, mzee huyo mwenye umri wa miaka 53 alinyoosha mkono kuchukua panga na kumshukia jamaa huyo bila huruma akamkata kichwa mara tatu na kumuua papo hapo.
"Katika harakati hiyo mwanamke huyo alikimbia eneo la tukio hadi kwenye mashamba ya karibu na hajaonekana tena," sehemu ya taarifa ya DCI ilisema.
Wanakijiji waliofurika eneo la tukio baada ya kusikia zogo walibaki vinywa wazi kutokana na tukio hilo la kutisha lililotokea katika kijiji chao tulivu.
Chifu wa eneo hilo Peter Lang'at alisema kifo cha Komen kilikuwa cha kusikitisha.
Aliwatahadharisha wakazi kutojichukulia sheria mkononi bali wahakikishe wanazingatia sheria. Mshukiwa alikamatwa na polisi na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Kwingineko, mwanamke mmoja wa Mombasa alipatikana amefariki dunia katika nyumba yake huko Bamburi baada ya kile kinachoaminika kuwa usiku wa kimahaba na jamaa.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Alice Wasike inadaiwa aliaga dunia usiku akilishana uroda na mwanaume ambaye alitoroka baadaye.
Baadaye mtu huyo alitiwa nguvuni.
0 comments:
Post a Comment