Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani |
MSTAHIKI meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani leo kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaj Mustapha Selebosi |
Madiwani kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia kikao hicho |
MSTAHIKI meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi amepongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuthamini imani za watu ambapo kwa waislamu wanaendelea kufanya ibada zao misikitini na wakristo wanaendelea kufanya ibada zao kanisani.
Meya Sellebosi aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani ambapo alisema kwamba Rais Magufuli amekuwa ni kielelezo tosha kwamba ni kiongozi ambaye anathamini imani za wananchi wake na ndio maana ibada zinaendelea kwenye maeneo mbalimbali.
Alisema kwamba lazima wawe makini na ugonjwa huo wa Corona huku akieleza kwamba kwa wale wenye mitandao wanaosoma kila siku wanatambua adhari ambazo zimetokana na ugonjwa huo duniani
Mstahiki Meya huyo alisema wakati wanawasiliana na jamaa zake wanaokaa Italia wanasema hakuna shughuli hata moja inayofanyika nchini humo hakuna kutembea wala kukutana kutokana na kila mtu kulazimika kukaa nyumbani kwake.
Aidha alisema hata Mombasa nchini Kenya kuna muingiliono wa familia hata ibada watu bada watu wanafanya majumbani mwao hivyo hatuna budi kumshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kuthamini imani za watanzania.
“Leo nichukue nafasi hii kumpoingeza Rais Dkt Magufuli kwa kuthamini imani za watu waislamu tunaendelea kufanya ibada zetu misikitini wakristo tunaendelea kufanya ibada wetu kanisani “Alisema
Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba Jiji hilo limejipanga kuhakikisha linakabiliana na ugonjwa wa Corona kwa kuchukua hatua ya kuweka vifaa maalumu vya kunawia mikono kabla ya kuingia kupata huduma kwenye taasisiza umma.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwaagiza maafisa tarafa wilayani humo kuhakikisha wanasimamia maeneo yote ya kutolea huduma wahakikisha wanakuwa na eneo la kunawia mikono na dawa kabla ya kupata huduma.
“Nataka kupata taarifa ni wapi ambapo hawajatekeleza jambo ..tunatamani tuone taasisi zote na maeneo ya kutolea huduma yaweze kuwa kichocheo kikubwa kutoa elimu kwa kupambana na ugonjwa wa Corona”Alisema
0 comments:
Post a Comment