Visanduku vya mawasiliano ajali ya ndege ya Brazil vyapatikana
Ndege
iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil
ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa
zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia
mawasiliano.
Katika
mnara wa mawasiliano ya ndege , rubani alisikika akirudia mara kadhaa
akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme
iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.
Kabla
hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho ,rubani alisikika
akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia
saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo
katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari
nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda
zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha
ajali ya ndege hiyo.
Wanajeshi
wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na
ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege
hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika
nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.
Wadadisi
wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia
juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya
uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.
Wachezaji
wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian
kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa
miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia
.Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana
kuomboleza vifo vyao.
Kwa
muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la
Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu
kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.
Mmoja wa
manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza
namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya
kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza
kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati
ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.
Visanduku
viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari
vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.
Wachunguzi
wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika
Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa
Uingereza BAE nchini Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo
wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika
mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa
maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao
inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika
uwanja wa Chapeco.
Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.
Timu hiyo
iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi
ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa
wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika
.Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na
waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza
maisha
0 comments:
Post a Comment