Mvua kubwa ya upepo iliyoambatana na mawe ya barafu iliyonyesha jana jioni katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imesababisha maafa ya kuanguka nyumba 21, vifo vya mifugo na watoto watatu kunusuirka vifo.
Mwandishi wetu ameshuhudia wakazi wa kijiji cha Mtimbwa katika Manispaa ya Sumbawanga wakijaribu kuokoteza mabaki ya bati zilizoezuliwa katika tukio hilo la mvua ya takribani dakika arobaini na tano na kuzungumza na baadhi ya wahanga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtimbwa, Wilbroad andrea Kapufi ameeleza tathmini ya awali imebaini kuathirika kwa nyumba 21 na kaya zaidi ya 50 zikikosa makazi.
chanzo: Channel Ten tz
0 comments:
Post a Comment