Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali
imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi
nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017
Dokta
Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016,
kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa
ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.
Alisema
kuwa fedha hizo zimewekwa kwenye mfuko wa Hazina, ili kuwawezesha wadau
na taasisi zitakazo husika kupanga utaratibu mzuri wa matumizi ya
fedha hizo.
“Fedha hizi zitaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu” aliongeza Waziri Mpango
Akizungumza
kuhusu mikopo ya wanawake na vijana, Dokta Mpango, alisema kuwa
serikali, kupitia Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu, imepanga kutumia shilingi
1bn kuendeleza ujuzi kwa vijana wasio na ajira na shilingi 1.955bn
kuwainua wanawake kiuchumi
Alifafanua
kuwa halmashauri za wilaya, miji na majiji zitaendelea na utaratibu wao
wa kutenga asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kutoa mikopo kwa vijana na
asilimia nyingine 5 kwaajili ya kuwawezesha wanawake katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment