MTOTO Nasra
Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro,
sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Nasra,
alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26
mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa
wa Morogoro...
Akizungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa
Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema Nasra, aliwekewa
mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni baada ya kuanza
kupumua kwa shida.
Alibainisha
kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini juzi usiku
ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.
VIDEO HAPA
Dk. Kombo
alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi waliamua kumfanyia
vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.
Dk. Kombo,
alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia, ataendelea na
vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.
Alisema licha
ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia chakula na dawa
baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.
Ofisa Muuguzi
wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia mashine hali ya
mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia vipimo kujua
maendeleo yake.
Naye mama mlezi
wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto hajawekewa mashine ya
kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na kiunoni
Mtoto Nasra
alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao walimweleza Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa alikuwa amefichwa
katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Said mkazi
wa Kata hiyo mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment