Tuesday 3 August 2021

Monitoring And Evaluation Officer at Aga Khan Health Service

 Monitoring And Evaluation Officer     Aga Khan Health Service, Tanzania (AKHST) – an Agency of the Aga Khan Development Network (AKDN), a Not-for-Profit International Organization that supports social development programs in Tan­zania. AKHST has completed a major expansion to position the institution to become a leading and integrated tertiary and teaching health care system in […]

This post Monitoring And Evaluation Officer at Aga Khan Health Service has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

4 Job Opportunities at TPC Limited – Various Posts

TPC Ltd is one of the fast growing sugar producing companies in Tanzania. The company is situated at the foot of Mount Kilimanjaro, 22kms south of Moshi Municipality. Applications are invited from qualified, energetic, proactive and dynamic Tanzanians to fill job vacancies position below in the Garage and Transport Department……   POST: WELDER (Trailers, Wagons, Tractor Implements) […]

This post 4 Job Opportunities at TPC Limited – Various Posts has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 3, 2021

 

ap
Share:

BILIONI 1.2 KUJENGA SOKA LA KIMATAIFA LA KUUZIA DAGAA KIPUMBWI WILAYANI PANGANI



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zingibar wilayani Mkinga mara baada ya kukagua jengo la BMU lililojengwa kupitia mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH) wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kipumbwi wilayani Pangani mara baada ya kukagua jengo la BMU lililojengwa kupitia mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH) wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo



Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kulia akikagua jengo la BMU Kijiji cha Zingibar wilayani Mkinga wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akiwa na Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah wakikagua jengo la BMU Kijiji cha Zingibar wilayani Mkinga wakati wa ziara hiyo

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiendelea na ukaguzi wa Jengo la BMU Kijiji cha Zingibar
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikagua Jengo la BMU Kijiji cha Zingibar wilayani Mkinga wakati wa ziara yake kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akigawa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Nne kwa ajili ya kilimo cha mwani kwa vikundi vitatu vya wakulima wa zao hilo wilayani Mkinga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Horohoro wilayani humo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya ambapo kunajengwa mnada wa mifugo wakati alipolitembelea eneo hilo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula


NA OSCAR ASSENGA, PANGANI.


SERIKALI inatarajiwa kutumia Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kimataifa la kuuzia dagaa Kata ya Kipumbwi Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambalo litatumika na wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi.


Hayo yalisemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo, iliyoambatana na ukaguzi wa majengo ya Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (BMU) katika Wilaya za Mkinga na Pangani.

Majengo hayo yaliyojengwa kupitia mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH).


Alisema wanunuzi wa dagaa wanaotoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi, Rwanda na Burundi wataenda kununua dagaa kutoka Kipumbwi hivyo wafanyabiashara wa kata hiyo hawatapata shida ya kutafuta soko la dagaa.


“Niwaambie serikali imesikia na inakusudia kujenga kujenga soko la Kimataifa la kuuza dagaa, msipate shida kuuza dagaa wenu.” Alisema
Waziri Ndaki.


Aidha, Waziri Ndaki alitoa onyo kwa viongozi wa BMU maeneo mbalimbali nchini, ambao wamekuwa wakishiriki vitendo vya uvuvi haramu pamoja na baadhi ya wavuvi kuwa vikundi hivyo vitavunjwa na wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.


Alifafanua pia baadhi ya BMU zimekuwa zikishindwa kutekeleza wajibu wake na kujikuta wakishirikiana na wavuvi haramu ambapo aliwataka kuacha vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria.


Akiwa wilayani Mkinga kwenye Kijiji cha Zingibari, Waziri Ndaki alisema serikali itaendelea kuwawezesha wakulima wa mwani kwa vifaa pamoja na utaalamu ili waweze kuzalisha kwa tija zao hilo kwa wingi na ubora
unaohitajika sokoni.


Alitoa kauli hiyo wakati akitoa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Nne kwa ajili ya kilimo cha mwani kwa vikundi vitatu vya wakulima wa zao hilo wilayani Mkinga.


Alisema kuwa kutokana na zao hilo kuwa la kiuchumi kwa wananchi wa mwambao wa pwani ya Bahari ya Hindi, serikali imeanza kuweka mazingira mazuri ya uwezeshaji na kutafuta masoko ya uhakika ili wakulima
waweze kunufaika kiuchumi.


"Huu msaada wa vifaa kwa ajili ya kilimo utafika katika maeneo yote yenye uzalishaji na msisitizo tumeanza kuweka kwenye elimu ya
namna ya kulima zao la mwani kwa ajili ya tija zaidi." alisema Waziri Ndaki


Kuhusu sekta ya mifugo, Waziri Ndaki alieleza sababu za kuanzishwa minada kwenye mipaka mbalimbali hapa nchini ambapo ikiwa na lengo la kuhakikisha wafugaji kutoka Tanzania wanauza mifugo kwenye minada hiyo
na wanunuzi wanatoka nchi nyingine kwenda kununua ili kudhibiti
utoroshaji.


Waziri Ndaki alisema hayo baada ya kufika katika mnada wa mipakani wa Horohoro kujionea miundombinu mbaimbali inayowekwa kabla ya kuanza rasmi kwa mnada huo ambao anasema utakuwa na matokeo chanya pindi utakapokamilika.


“Licha ya kusaidia kupunguza utoroshaji wa mifugo mnada utasaidia kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo kuinua uchumi wao, kwa sababu wakipeleka ng’ombe nje ya nchi wanauza bei ya juu lakini pia tunataka tuwapunguzie wananchi adha ya kuvuka mipaka kwani jambo hili wakati mwingine linasababisha kuuza mifugo yao kwa bei ya
chini” Alisema


Hata hivyo Waziri Ndaki alisema wameamua kuondoa shida hizo kwa kuwa na minada ya mipakani ili wafugaji waweze kuuza mifugo yao maeneo rasmi na serikali iweze kupata mapato yao .

 

Share:

Monday 2 August 2021

Mpyaa : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOGTUWE TUNAKUTUMIA HABARI BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Share:

Tanzania, Rwanda Zakubaliana Kuimarisha na Kukuza Ushirikiano



Share:

Vimba na TECNO Camon 17 na Spark 7 Ujishindie Kitita Cha Shilingi Milioni 100

 ZAWADI ZA THAMANI YA SH.100 MILIONI KUSHINDANIWA KATIKA MSIMU HUU WA PROMOSHENI YA VIMBA.
 
Kampuni ya simu TECNO kupitia ukurasa @tecnomobiletanzania inawakambusha wateja wa simu za TECNO kuhusiana na promosheni ya VIMBA. TECNO inawataka wateja wote wa TECNO kununua TECNO Camon 17 na Spark 7 katika msimu huu wa kampeni ya VIMBA. 

Kampeni hii ya VIMBA itadumu hadi tarehe 13/8/2021 na kwa kipindi hiki chote wateja wa simu za TECNO wataingia katika droo la bahati na sibu na mshindi kuondoka na zawadi ya gari.
 

Baadhi ya zawadi nyengine zimeorodheshwa kuwa ni jokofu na pikipiki lakini pia kuna zawadi za papo hapo kama earbuds, smartwatch na Radio speaker usiache kutembelea maduka ya TECNO katika msimu huu wa promosheni ya Vimba kwani kama ilivyo ada pia utauziwa simu hizo mbili kwa punguzo la bei.
 

TECNO Camon 17 na TECNO Spark 7 ni matoleo mapya kwa mwaka huu wa 2021 kutoka TECNO ambapo TECNO Camon 17 inaendelea kushikilia taji la simu yenye selfie kali duniani ikiwa na MP48 na 4k Video resolution na sifa nyengine ni processor ya Mediatek Helio G95, 5000mAh na MP64 za kamera ya nyuma ikiwa na black and white mode kwajili ya kuchukua filamu katika ubora stahiki. 


TECNO Spark 7 ni moja kati ya simu za TECNO yenye bei rafiki unachokipata kutoka Spark 7 ni zaidi ya unacholipia TECNO Spark 7 ni yenye kuchukua picha simu yenye wigo mpana wa kioo cha inch 6.52HD+ na MP16 za kamera ya nyuma na flash 4 lakini pia simu yenye ujazo mkubwa wa 5000mAh na hii kuifanya TECNO Spark 7 simu sahihi kwa mwanafunzi mwenye kutumia mda mwingi kujisomea mtandaoni.  

 
https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/  



Share:

IGP Sirro Aionya CHADEMA na Wanaokusudia Kufanya Vurugu


Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana kwa namna yoyote.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agost 2,2021 Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema tuhuma dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA  Freeman Mbowe na wenzake ziko chini ya mamlaka ya mahakama.


Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo la kupanga njama za ugaidi na uhujumu uchumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Sirro amewaonya wale wote wanaokusudia kufanya maandamano tarehe 5 Agosti 2021, siku ambayo kesi hiyo itatajwa tena kutokufanya hivyo kwani “kuvamia mahakama ni sawa na kuvamia kambi ya jeshi.”

"Jeshi la polisi halitegemei mtu au kikundi cha watu kwa namna yoyote kutoa shinikizo kwa mamlaka ya mahakama au kwa mtuhumiwa Freeman Mbowe aachiwe "amesema Sirro.

"Jeshi la polisi linatoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kitakachojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au namna yoyote ile kutoa shinikizo lolote,"amesema.

“Chadema wanasema mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa, wanavyoona wao hawezi kufanya hivyo, sasa kama Mbowe ni mkweli na amamuamini Mungu waende wakamuulize jambo hili unasemaje.”

“Lakini kabla ya uchaguzi nilisema kuna watu wamepanga kuhakikisha uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na nilisema wamepanga kuua viongozi na nilisema tutawakamata,” amesema Sirro

“Habari ya yeye wajue ni binadamu, anaweza kufanya makosa, tumempeleka mahakamani tuiache mahakama itimize wajibu wake.” amesema Sirro
 

Sirro amewataka viongozi wa dini na taasisi nyingine ziache kusema Mbowe anaaonewa na badaala yake wasubiri mahakama iamue.



Share:

IGP SIRRO AWATAKA CHADEMA WASUBIRI MAHAKAMA ITAKAVYOAMUA JUU YA MBOWE

 

Na Dickson Billikwija,Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP SIMON SIRRO amekita Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kuacha maneno maneno na kusubiri maamuzi ya Mahakama itakavyootoa maamuzi kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe.

Akiongea leo Agosti 02,2021 jijini Dar es Salaam mbele ya Wanahabari IGP Sirro alisema kufanya maandamano ni sawa na kuvunja sheria na ukivunja sheria ni sawa na kufanya uhairifu,

Alisema wafuasi wa CHADEMA wasimuone Mwenyekiti wao Kama malaika ni mtu ambaye hawezi kukosea,

Kwa msisitizo aliendelea kusema kwamba wao (CHADEMA) wamuulize Mwenyekiti wao Kama ameonewa na ana uhakika kama ana imani na dini yake atasema ukweli.

IGP Sirro aliwataka watanzania kutoshawishika na hao vyama Vya upinzani kwa kuwataka eti wafanye maandamano kuja dar na kwenda mpk Mahakama Kuu.

IGP Sirro alisema yeye kwa kushirikiana na jeshi la polisi hawata waacha waalifu.Alisema mwenye hekma aiachie Mahakama iamue.

Sanjari na hi]nlo IGP Sirro aliziomba halmashauri zote Nchi kutunga sheria ndogondogo zitakazosaidia wananchi kuchangia Ulinzi shirikishi,


Alizipongeza Halmashauri mbili za Temeke na Kinondoni kuwa na sheria ndogondogo ambazo zimekuwa mwongozo kwa jeshi la polisi

Share:

SERIKALI KUPELEKA CHANJO YA CORONA MAKAMBI YA WAKIMBIZI

 Na Abubakari Akida,MOHA
Serikali imesema iko katika mpango wa kupeleka Chanjo ya UVIKO 19 katika Makambi na Makazi ya Wakimbizi katika mikoa ya Kigoma,Tabora na Katavi ikiwa ni mpango mkakati wa kukabiliana na wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Katumba kinachotumiwa na wakimbizi na raia wapya wanaokadiriwa kufikia 86,233  toka nchini Burundi ambao walikimbia mapigano ya kikabila yaliyotokea nchini kwao 1974.

“Katika kukabiliana na janga la UVIKO 19 tayari Wakuu wa Makambi washaanza  kutambua idadi ya watu ambao wanauhitaji wa hiari wa kupata chanjo hiyo ili jamii ya wakimbizi wanaokaa katika makambi yaliyopo nchini ili muda ukifika tuwe na takwimu sahihi za wanaohitaji kuchanjwa na tayari kama mnavyoona tayari zoezi la chanjo lishaanza baada ya siku chache kuzinduliwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu,wito pekee naotoa kwa wakimbizi kufuata ushauri wa wataalamu wa afya katika kujikinga na maradhi hayo ambayo dunia sasa inapitia” amesema Naibu Waziri Chilo

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wa UVIKO 19 katika Kituo cha Afya Katumba, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dkt.Veneranda Msati amesema hawana mgonjwa aliyefika kituoni huku akielezea utolewaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wagonjwa na mama wajawazito wanaofika katika kituo hicho kupata huduma.

“Kwasasa katika kituo chetu hatuna mgonjwa yoyote wa Corona tunachofanya ni kutoa ushauri wa kujikinga na maradhi hayo kwa wagonjwa wanaofika hapa kupata huduma za afya ikiwemo na akina mama wajawazito lakini pia tunatuma wataalamu wetu wa afya kwenda kuwafundisha wananchi katika makazi yao jinsi ya kunawa kwa maji safi tiririka na kukaa umbali unaoshauriwa ili kuepuka maambukizi ya UVIKO”amesema Dkt. Veneranda

Awali akisoma taarifa ya makazi hayo,Mkuu wa Makazi ya Katumba,John Mwita amesema hali ya usalama ni shwari huku wakiendelea kutoa elimu na kufuata sheria za kuishi katika makazi kwa wakimbizi hao.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA



Share:

MREMBO AKAMATWA BAADA YA JAMAA ALIYEKUWA ANACHONYA NAE ASALI HOTELINI KUFARIKI



Polisi katika kaunti ya Kiambu Ndumberi nchini Kenya wamemkamata mwanamke mmoja baada ya jamaa aliyekuwa akipalilia mgomba wakiwa kwenye chumba cha anasa kufariki dunia.

Wawili hao walikuwa katika chumba kwenye hoteli ya Konteina walipokuwa wakionja tunda la penzi. 

Moses Muiruri aliamua kukodi chumba hicho baada ya wawili hao kuonja chupa kadhaa Ijumaa Julai 30,2021.

 Duru kwenye mkahawa huo ziliambia gazeti la Standard kuwa wawili hao waliingia kwenye chumba nambari saba saa 4:30 asubuhi.

 Kufikia Jumamosi Julai 31, kipusa huyo alijaribu kutoroka kutoka hoteli hiyo baada ya mambo kuenda sege mnege.

 Polisi waliitwa baada ya Muiruri kupatikana kwenye chumba hicho akiwa amefariki dunia.


Mkuu wa polisi Ndumberi Badel Mohammed alisema mwendazake alipatwa akivuja damu kutoka mdomoni.

Kisa sawa na hicho kiliripotiwa Murang'a ambapo buda alizimia na kufariki dunia katika chumba alipokuwa na mpenziwe.

 Frederick Opiyo alikuwa kwenye mkahawa wa Rurago saa tatu usiku Julai 27 akiwa na mpenzi wake Mary Mwende Munyalo kabla ya kuzirai na kuzima. 

Mwende alisema alikuwa akuioga wakati ambapo aliskia dume huyo akiunguruma huku akiwa na matatizo ya kupumua.

 Polisi walisema walifika katika eneo la mkasa na kupata vifaa vya kazi vikiwamo mipira ya kondomu na pia dawa za kuongeza nguvu za mapenzi.
Share:

SERIKALI YAAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI KUTOA AJIRA VIJIJINI


Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021 katika Kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akitoa maagizo kwa wakandarasi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa kifaa mbadala cha wiring UMETA kinapatikana ili wananchi wasiomudu gharama za wiring waweze kuvitumia kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge akiongea na umati wa wananchi wa Kijiji cha Nalasi kilichopo Wilaya ya Tunduru ambako uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili uliofanyika tarehe 01/08/2021.
Watoto wakifuatilia matukio ya uzinduzi.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwakabidhi wazee kifaa cha UMETA ambacho ni mbadala wa wiring ili waweze kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akiwa na Mkuu wa Ruvuma Brigedia Jenerali,Balozi Wilbert Ibuge pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga Makofi mara baada ya kuzindua Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru Agosti 1,2021.

........................................

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana waliopo katika vijiji ambapo miradi hiyo inatekelezwa.

Dkt. Kalemani alitoa agizo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili ngazi ya mikoa katika Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Agosti 1,2021 katika kijiji cha Nalasi Wilaya ya Tunduru.

“Wakandarasi chukueni vibarua kutoka katika vijiji ambavyo mnapeleka umeme” alisema na kuongeza kuwa lengo ni kufanya miradi hiyo iwe na tija kwa kuwashirikisha wananchi katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.

Aidha, Mhe. Kalemani amesema Serikali itatumia zaidi ya Shilingi bilioni 71 kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vijiji 265 ambavyo havina huduma ya nishati hiyo katika Mkoa wa Ruvuma.

“Katika Mkoa wa Rvuma, vijiji vyenye umeme ni 289 kati ya 554. Kwa kutambua hilo leo ninawakabidhi wakandarasi waushambulie Mkoa wa Ruuma na kuhakikisha vijiji vyote vilivyosalia 265 vinapatiwa umeme kupitia mradi huu. Nipende kutoa rai kwa Watanzania wote kuwa kila Mtanzania atapata Nishati ya Umeme” alisema Waziri Kalemani.

Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Tunduru ambako Mradi umezinduliwa kuna vijiji 85 ambavyo hadi sasa bado havijafikiwa na huduma ya umeme na kwa kutambua hilo, Serikali imetenga takribani Shilingi bilioni 23.52 kwa ajili ya kuvifikishia umeme vijiji hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge aliwataka wananchi wasihujumu miundombinu ya kusambaza umeme kwa kuiba nyaya na vifaa vingine na wawe walinzi wa miundombinu hiyo.
Share:

Relationship Manager; SME at NMB Bank

Relationship Manager; SME     Job Purpose Responsible for growing both Liabilities (Deposits) and Assets from Small and Medium Enterprises (SMEs) for Business banking; advising Business Banking department on business strategy, assisting SME Business Bankers /Relationship Officers/Branch Managers in recruiting business customers to ensure SME business growth. Main Responsibilities   Actively selling SME deposits, lending and […]

This post Relationship Manager; SME at NMB Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Mhe.Sheha Mpemba Faki ajiuzulu.



Share:

Jengo la kudhibiti mifumo la kituo cha kupokea na kusambaza umeme cha Msamvu - Morogoro Lateketea Kwa Moto

Ofisi za Kituo kikubwa cha kupokea na kusambaza umeme Msamvu - Morogoro limewaka moto na kusababisha Mkoa wa Morogoro kukosa umeme.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, lakini taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa wataalamu  na mafundi wanaendelea na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka. 





Share:

Mbunge wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpemba Faki ajiuzulu


 

Share:

PICHA: Rais Samia Awasili Nchini Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali Nchini Rwanda kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Paul Kagame leo Agosti 02,2021.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger