Thursday 29 July 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 29,2021









Share:

CHANJO YA CORONA YAMUIBUA MGEJA..AMPONGEZA RAIS SAMIA KURUHUSU WATANZANIA KUCHANJWA,WANAOPOTOSHA WAKAE KIMYA



Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation ya Mjini Kahama mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana ofisini kwake muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua chanjo ya kinga ya ugonjwa wa Covid 19 (Picha na Suleiman Abeid)

**
Na Suleiman Abeid,TimesMajira Online,Shinyanga

TAASISI ya Tanzania Mzalendo Foundation yenye Makao Makuu yake wilayani Kahama mkoani Shinyanga imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara wa kuruhusu watanzania kupatiwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo, Khamis Mgeja katika maongezi yake na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kahama muda mfupi baada ya Rais Samia kuzindua rasmi chanjo Covid 19.

Mgeja amesema kitendo cha Rais Samia kinastahili kupongezwa na kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake na kwamba hatua hiyo itanusuru maisha ya watanzania wengi watakaokubali kuchanjwa chanjo hiyo japokuwa wapo wachache wanaopingana na msimamo huo wa Serikali.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Rais Samia kwa uamuzi wa kuruhusu chanjo ya kinga ya Corona kuingizwa hapa nchini, na ameonesha njia kwa yeye mwenyewe kuanza kuchanjwa chanjo hiyo na ameifanya nchi yetu iwe miongoni mwa mataifa mengine duniani yanayowajari wananchi wake,”

“Pia nawapongeza wadau wengine wote walioungana na Rais wetu ikiwemo viongozi wa madhehebu ya kidini katika kujitokeza kuchanja chanjo hii, hili suala linagusa hatima ya maisha yetu, kila anayejisikia ni muhimu akachanjwa maana Rais kaisha onesha njia,” ameeleza Mgeja.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga ametoa wito kwa watanzania ambao bado wanatoa maneno ya upotoshaji kuhusiana na chanjo hiyo ya kinga ya Covid 19 wakidai haifai na ina madhara.

Amefafanua kuwa ni vyema watu wanaotaka kupotosha ukweli wakakaa kimya badala ya kuendelea kuwapotosha watu kwa maneno yasiyokuwa ya kitaalamu ambapo ameiomba Serikali iharakishe kusambaza chanjo hiyo katika mikoa yote nchini ili watu waweze kuchanjwa.

“Jambo hili ni la hiari basi, hawa wanaotaka kupotosha tunawaomba wakae kimya, suala hili ni la kihiari, ni muhimu watu waendelee kushauriwa wajitokeze kuchanjwa, na sisi huku mikoani tunasubiri chanjo hii ifike haraka mikoani na mawilayani ili watu waweze kuchanjwa,”

“Hawa wanaopinga ni vyema sasa wakatupa mbadala wa kitaalamu tutumie njia gani katika kujikinga na ugonjwa huu, na jambo hili ni la hatari kuona watu wasiokuwa na utaalamu wa kidaktari ndiyo wanaosimama kidete kupinga, na watuoneshe kwa vigezo kwa nini chanjo hii haifai,” ameeleza.

Vilevile amewataka watu hao wanaoupinga msimamo wa Serikali wakaacha mambo ya kitaalamu yasemewe na watu wenye utaalamu wa masuala ya kiafya, suala la kitaalamu lisiingizwe kwenye siasa na wanasiasa waachiwe wafanye kazi zao za kisiasa.

Mgeja ameonesha kushangazwa na kitendo cha wanasiasa kuingilia masuala ya kitaalamu kwa kuukataa ukweli na kuupinga ambapo amehoji ni vipi upande wa wataalamu hawaingilii masuala ya kisiasa ambapo alisema upotoshaji wao unaweza kuliingiza Taifa la Tanzania katika matatizo makubwa.

“Vilevile nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini na viongozi wote wa kidini na wale wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa jinsi walivyoonesha msimamo mzuri katika kuunga mkono maamuzi ya Serikali kuhusiana na janga la ugonjwa wa Covid 19,”

“Niwaombe tu watanzania hivi sasa tupo kwenye janga zito na tukifanya mizaha tunaweza kuteketeza maelfu ya watanzania kwa jambo ambalo linaweza kuzuilika mapema kabla halijatuletea madhara makubwa, wakumbuke ule usemi wa “….Akili za kuambiwa changanya na za kwako, watauona ukweli na msimamo wa Rais Samia,” ameeleza Mgeja.

Rais Samia Suluhu Hassan jana amezindua rasmi chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 ambapo alisema japokuwa wapo baadhi ya watanzania wanaopinga chanjo hiyo lakini wengi wao wanaunga mkono na kwamba Serikali itahakikisha wale wote wanaotaka kuchanjwa wanachanjwa.
Share:

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATETA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA MJINI LONDON UINGEREZA

Mhe. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe Patricia Scotland mjini London, Uingereza. Rais Mstaafu kama Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) yupo huko kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi kwa ajili ya kuchangia Elimu utakaofanyika tarehe 28-29 Julai,2021.

Share:

ZU YAENDELEA KUNG'ARA MAONYESHO YA (TCU)



Chuo kikuu Cha Zanzibar, ZANZIBAR UNIVERISTY (ZU) Cha Tanzania visiwani kimeendelea kung'ara kwenye maonyesho ya kumi na sita (16) yanayoandaliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania.

Dr .Salama Yusuf ambaye ni muadhili Mkuu wa chuo hicho wakati wa mazungumzo yake  leo Julai 28,2021  amesema wanawakaribisha wanafunzi mbalimbali na wa jinsia zote kufika chuoni kwao.

Amesema kwenye maonyesho hayo wanafanya udahili na inakuwa rahisi kwa mzazi au mwanafunzi kufanyiwa udahili kwenye banda lao..

Aidha Dr. Salama aliwashauri waandaaji wa Maonyesho hayo kuyaboresha zaidi kwa sababu ni msaada mkubwa kwa wazazi ama wanafunzi,

Alisema pia (ZU)ni chuo kizuri chenye walimu wazuri na mwanafunzi akimaliza chuoni hapo anakuwa mbobezi wa suala ambalo alilisomea.

Aidha Alisema kutokana na wimbi la tatu (3)la Uviko-19 Zanzibar University inakabiliana sana kwani kuna sehemu maalumu yenye maji tiririka na sabuni

Alisema wanapokuwa sarasani wanawaweka anafunzi kwa umbali kidogo na hata mwalimu anahakikisha wanafunzi wote wamevaa barakoa
Share:

NABII JOSHUA: ACHENI KUPINGA CHANJO, RAIS SAMIA SONGA MBELE



Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala


Na Mwandishi Wetu, Kihonda

KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala amewataka viongozi wa kisiasa na kidini kuacha kutumia ushawishi walio nao katika jamii kuipinga chanjo ya virusi vya corona.

"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hekima yake ya kuruhusu chanjo ije nchini kwa ajili ya ustawi wa afya za wananchi wetu wa Tanzania;

Wito huo ameutoa muda mfupi baada ya maombi ya kuliombea Taifa ambayo alikuwa anayafanya maalum Yespa, Kihond mjini Morogoro ili Mungu aweze kuiponya Tanzania na watu wake huku akisisitiza kuwa, licha ya maombi pia ni jukumu la kila mmoja kuzingatia miongozo na kanuni zinazotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya ili kukabiliana na Corona.

"Ushauri wangu kwa viongozi wa kijamii hasa viongozi wa dini tusitumie ushawishi tulio nao miongoni mwa jamii yetu kupinga suala la chanjo, hilo ni jambo ambalo linaweza kuligawa Taifa na kulifanya lisitawalike na jambo ambalo si nzuri kwa kuwa linawazoeza watu kupingana na maamuzi ya mamlaka za nchi.

"Tabia hii ya viongozi wa dini kuipinga Serikali hadharani wakati tunayo fursa ya kuishauri Serikali bila vipaza sauti kwa hakika inatengeneza watu wenye kiburi wasiotii viongozi wa nchi na kutokutii mamlaka maandiko yanasema ni uasi na huko ni kugombana na Mungu,"alifafanua Nabii Dkt.Joshua.

Pia aliwaomba wananchi wasiogope juu ya chanjo, "Serikali yetu ipo makini sana na inaongozwa na Mungu, kamwe haiwezi kuwaangamiza watu wake. Mwisho namuomba Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aendelee kuwaa hodari na moyo wa ushujaa, asiyumbe anapoyumbishwa sisi wananchi na kanisa tunamuombea sana na tupo pamoja na serikali yake.

"Mimi binafsi ninamwahidi kuwa nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kuisaidia Serikali kutoa elimu kwa wananchi ili waokoe afya zao dhidi ya Corona kwa njia ya chanjo,"alisema Nabii Dkt.Joshua.

Wito huo ameutoa ikiwa leo Julai 28, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongozana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali wamezindua rasmi chanjo ya corona nchini.

Uzinduzi huo umefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amesema chanjo hiyo ni salama na asingekuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kuchanjwa chanjo ya Corona kama ingekuwa si salama.

Hatua hiyo inakuja baada ya wiki iliyopita Tanzania kupokea zaidi ya dozi milioni 1.05 za chanjo aina ya Johnson & Johnson zilizotolewa na Marekani kupitia mpango wa upatikanaji wa chanjo wa Covax.

Katika mpango huo, wapo baadhi ya watu wanaopingana na harakati hizo wakieleza chanjo hizo sio salama na wapo wanaounga mkono, lakini kiongozi huyo mkuu wa nchi amewaondoa hofu wananchi kuhusiana na hilo.

Rais Samia alisema yeye ni mama wa watoto wanne, ni bibi wa wajukuu kadhaa wanaompenda sana na yeye kuwapenda, ni mke pia lakini mbali ya yote ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi wa nchi hii.

“Nategemewa kama mama, kama bibi, kama Rais, kama Amiri Jeshi Mkuu, nisingejitoa mwenyewe nikajipeleka kwenye kifo, nikajipeleka kwenye hatari nikijua kwamba nina majukumu yote haya yananitegemea .

“Lakini nimetoka kuonyesha umma wanaonifuata nyuma nikijua kama Rais ni mchungaji na nina watu wengi nyuma nawachunga na wananitazama mimi hivyo nisingetoka kujihatarisha,”amesema Rais Samia.

Rais amebainisha kuwa amekubali kwa hiari yake kuchanja akijua kwamba ndani ya mwili wake ana chanjo kadhaa ambazo ameishi nazo kwa miaka 61 sasa kwani tangu amezaliwa kuna chanjo mbalimbali wamekuwa wakichanjwa, mbali na zingine wanazochanjwa njiani wakiwa wanasafiri ikiwemo ya homa ya manjano.

Hivyo kwake haoni hatari iliyoko na baada ya wanasayansi kujirishisha hivyo yupo tayari kuchanja na kuwa kuwaomba Watanzania wapuuze yote wanayoyasikia kuhusiana na chanjo hiyo.

“Kwa wale ambao koo zao hazijaguswa, hawajapata madhara ya maradhi haya wanaweza kusema wanavyotaka. Lakini nenda leo Moshi, nenda Arusha ,nenda Kagera, hata Dar es Salaam uonane na zile koo ambazo zimeshaguswa na haya maradhi wana maneno ya kukuambia na kama wangeweza leo wote wangekuwa hapa kutaka kuchanja kuepukana na ile hasara walioipata,"alisema.
Share:

Wednesday 28 July 2021

Tanzia : MKURUGENZI WA KAMPUNI YA FRESHO INVESTMENT, FREDY SHOO 'Fresho' AFARIKI DUNIA


Fredy Shoo maarufu Fresho enzi za uhai wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd ya Mjini Shinyanga Fredy Shoo maarufu Fresho amefariki dunia leo jioni Jumatano Julai 28,2021 wakati akiendelea kupata matibabu jijini Dar es salaam.

Mwekezaji Mzawa Fredy Shoo ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambulia pamba , kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba pamoja na uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ uliopo katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Fresho. Amina
Share:

NAMNA NILIVYOWEZA SAIDIA MME WANGU KUACHA KUTUMIAJI WA POMBE


Wanasemaga pombe sio kitu kibaya lakini inategemea na mnywaji wa hiyo pombe yupo katika hali gani au kichwa chake kinaweza kuhimili pombe kiasi gani, ukilitambua hilo basi pombe haitokusumbua kwani hata watengenezaji wa bidhaa hizo wanashauri tunywe kistaarabu.

Lakini pia matatizo yanaweza kutokea endapo mnywaji wa pombe hiyo amekunywa kiasi gani, katika hali ya kawaida unywaji wa pombe unaweza kupelekea kutoelewana katika familia, kutoisaidia familia yako na kujikita kwenye pombe na hata kutokufanya mambo ya maendeleo ya mtu binafsi.

Kwa majina naitwa Wini Kweka nafanya kazi katika kampuni moja ya usafirishaji jijini Mwanza nimeolewa na bwana yangu ameajiriwa katika Benki moja hapa jijini Dar es salaam, na tuna watoto wawili mmoja yuko kidato cha pili mwingine darasa la nne.

Mme wangu yeye ni mtumiaji wa pombe lakini naweza sema yeye ni mmoja kati ya watu wanaoitumia pombe vibaya kwa sababu maana anakunywa pombe nyingi kiasi kwamba anavua nguo na kulala baa kabisa mara nyingine.

Matumizi yake ya pombe yamepelekea tukose maendeleo kwa muda mrefu sana ukizingatia mshahara wake karibia wote alikua akiumalizia huko anaponywea pombe, ilikuwa anapokea mshahara halafu anasema bado hajapokea kisha wote anaumalizia kwenye pombe na kabla mwezi haujaisha pesa yake inakuwa ishakata.

Na hio inapelekea kwamba anakuwa na marafiki wenzake akiwa baa hivyo huwanunulia watu wengi katika meza yake na kupelekea kiasi kingi cha pesa kutumika kwa mara moja hasa hasa katika suala la kijinga la unywaji wa pombe.

Mimi nikiwa kama mke wangu nilikuwa namshauri kila mara nikimwambia kwanini asiache pombe na tufanye mambo ya maana akawa ananijibu kazi zake ndo zinamfanya awe mlevi, kwa hiyo mzigo wote ukawa umenielemea mimi kuanzia watoto, chakula na kila kitu.

Maisha yetu yalikuwa hivyo hivyo tu, maana mme wangu kabla hajapokea mshahara wake tunapanga vitu muhimu vya kufanya ila akishapokea anakuwa tofauti hadi nikimkumbusha naambulia kipigo.

Niliweza washirikisha marafiki zangu ili kupata ushauri kutoka kwao ila majibu niliyopata ni kuwa wanasema kampani yake ya marafiki ndo tatizo kwani wamekuwa na utaratibu wa kunywa pombe kila wakitoka kufanya kazi zao za siku hiyo.

Mimi sikukata tamaa juu ya mme wangu kwa sababu nilitazama upande wa pili wa watoto wetu nikikata tamaa juu ya Baba yao maisha gani wataishi. Siku moja nikiwa nilimtembelea shangazi yangu na katika maongezi nikamshirikisha na tatizo langu akaniambia hata yeye mme wake alikuwa na tatizo hilo zamani na kunipatia namba ya mtu aliyemsaidia mme wake kuacha pombe.

Niliwasiliana na Kiwangadoctors kisha nikawatembelea ofisini kwao. Nilipata huduma kutoka kwa Dr. Kiwanga kisha nikarejea nyumbani kwa ajiri ya kutumia ile dawa ambayo nilipewa na Dr. Kiwanga.

Nikiwa natumia ile dawa mme wangu alianza kutapika kila akinywa pombe au akihisi harufu ya pombe, na mwisho wake aliacha mwenyewe na hivi sasa mme wangu hatumii pombe kabisa au kinywaji chochote cha kulewesha.

Nikiwa ofisini kwa Dr. Kiwanga niliambiwa kuwa wana dawa ya Nguvu za kiume, dawa ya kufanya nyota yako ing’ae, dawa ya mapenzi, dawa ya Sukari pamoja na dawa ya kurejesha mpenzi wako.

Wasiliana na kiwangadoctors kwa namba ya simu +254 769404965 au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com kupata taarifa zaidi kuhusu kiwanga doctors.
Share:

MME WANGU KANIFUKUZA KWA NYUMBA YETU BAADA KUGUNDUA KUWA ANATEMBEA NA MDADA WA KAZI

Share:

Institute of Rural Development Planning IRDP Prospectus 2021/2022

Institute of Rural Development Planning IRDP Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Institute of Rural Development Planning – IRDP have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details […]

This post Institute of Rural Development Planning IRDP Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

DC MKINGA KANALI SURUMBU AWATAKA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) ILIYOBORESHWA

 

MKUU wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati akizindua mpango wa bima ya Afya iliyoboreshwa wilayani Mkinga (CHF) iliyofanyika kwenye eneo la Maramba wilayani humo kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Amani Kasinya na kushoto ni Mratibu wa CHF mkoa wa Tanga Imani Rwatamabanga

 

Mratibu wa CHF mkoa wa Tanga Imani Rwatamabanga akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mganga Mkuu wawilaya ya Mkinga (DMO) akizungumza wakati wa uzinduzi
Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson akieleza umuhimu wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) katika uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga,Kanali Maulidi Surumbu katikati aliyevaa tisheti nyeupe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Amani Kasinya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe  na kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkinga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi huo

KATIBU Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kushoto akifuatilia kwa umakini matukio wakati wa uzinduzi huo
Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson kushoto akimsikiliza kwa umakini mkazi wa wilaya hiyo Seif Selemani aliyekwenda kwenye banda lao wakati uzinduzi wa mpango huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo

NA OSCAR ASSENGA, MKINGA

MKUU wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga,Kanali Maulidi Surumbu amewahamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa ili kuweza kupata matibabu wanapougua na hivyo kuwaondolewa changamoto ambazo wanaweza kukutana nazo.

Kanali Surumbu aliyasema hayo wakati akizindua kampeni ya Uhamasishaji wananchi wa Mkinga kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa iliyofanyika kata ya Maramba wilayani Mkinga.

Alisema mpango huo ni mzuri kwa sababu una wahakikishia huduma ya matibabu pindi wanapougua na hivyo kupunguza kiasi kikubwa cha changamoto za kupata huduma za matibabu na kusaidia kuboresha huduma za afya kwenye vituo husika.

“Mwanachama anapojiunga na CHF kuna asilimia 10 ambazo hurudishwa kwenye vituo vya afya hivyo nitumie nafasi hii kuwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mkinga kuhakikisha mnachangamkia mpango huu “Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema wilaya hiyo ilianza kusajili wanachama kwa kutumia mfumo wa kieletroniki Januari mwaka jana na kaya wanafika watu wasiozidi sita wanapata matibabu kwenye wilaya ya Mkinga na Mkoa wa Tanga kwa miezi 12.

“Mpaka kufikia leo 26,Julai Mkinga imesaijili kaya 661 kati ya kaya 6071 zilizotakiwa kusajili kwa mwaka kati ya hizo kata 661 zilizosajiliwa kaya 506 zimechangiwa na wafadhili,kaya 155 wananchi wa mkinga wamejiunga kwa hiari hivyo ni sawa na asilimia 2.7 ya lengo iliyowekewa wilaya hiyo kwa mwaka”Alisema

Alisema hali hiyo inaonyesha wananchi Mkinga bado hawajahamasika vya kutosha kuhusu umuhiumu wa kujiungaa na mfuko wa afya ya jamii hivyo kupitia kampeni hiyo ambayo inaizindua itakwenda kuwa chachu ya kuhamaksisha kuwa juu ya uhumu wa kujiunga mfuko wa afya ua jamii iliyoboresha.

“Kauli mbiu ya kampeni hii inasema CHF iliyoboreshwa kwa afya ya kila mtanzania jiunge leo hivyo ni matarajio yangu kwamba baada ya uzinduzi huo wananchi wote mtajiunga na kujisajili”Alisema

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii Mkoa wa Tanga Imani Rwatamabanga alisema lengo la kitaifa kwa CHF ni kufikia asilimia 30 ya watanzania wote wanaopaswa kujiunga na CHF ifikapo June 2021 sasa leo ni Julai mwisho ni asilimai 30 kwa Taifa.

Alisema kwa mkoa wa Tanga ili kufikia lengo hilo la asilimia 30 ya wakazi wa mkoa huo walipaswa kufikia kaya zipatazo 146,954 hadi June 2021 katika kufikia lengo hilo mkoa unapaswa kuandikisha kaya 14,695 ambao ni sawa na asilimia 3 kwa kila mwezi,Kaya 48,985 ambayo ni sawa na asilimia kwa robo mwaka na kaya 146,954 ambayo ni asilimia 30 kwa mwaka.

Aidha alisema takwimu za leo kwa wilaya hiyo kwa mujibu wa tamisemi ina watu 137,268 sawa na kaya 27,454 kama walikuwa wanataka kwenda vizuri kila mwezi walipaswa kusajili kaya 824 na robo mwaka wawe wamesajili kaya 2,745 ambapo wangekuwa wamesajili kwa mwaka kaya 8,230 ambayo ingewapa asilimia 30.

Alisema hadi asubuhi kaya ambazo zimesajiliwa ni 155 hivyo kwa pamoja viongozi viongozi ,wananchi washirikiane wameane hamasa ili kuweza kuongeza idadi ya kaya ambazo zitakuwa zimesajiliwa.

Hata hivyo kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson alisema mfuko huo unafaida kubwa sana kwa wananchi hivyo wanapaswa kuchangamkia kujiunga nao ili waweze kunufaika na huduma za matibabu katika vituo vya Afya.

Alisema fursa hiyo ni muhimu na nzuri hivyo wajitokeze kujiunga ili kuweza kunufaika na mfuko huo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkinga Amani Kasinya alisema mpango huo ni mzuri na ni matunda ya serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma za Matibabu.

Kasinya aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanachangamkie mfuko huo ambao unafaida kubwa kwao kutokana na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapokuwa wakiugua.
Share:

Live : RAIS SAMIA ANAZINDUA CHANJO YA CORONA TANZANIA MUDA HUU


Rais wa Jamhuri ya Muungano a Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28,2021 anatarajiwa kuzindua utoaji wa chanjo nchini ambapo pia atachoma chanjo hiyo…
Share:

Tanzania Institute of Accountancy TIA Prospectus 2021/2022

Tanzania Institute of Accountancy TIA Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Tanzania Institute of Accountancy – TIA have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about TIA […]

This post Tanzania Institute of Accountancy TIA Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Institute of Tax Administration ITA Prospectus 2021/2022

Institute of Tax Administration ITA Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Institute of Tax Administration – ITA have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about ITA […]

This post Institute of Tax Administration ITA Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Water Institute WI Prospectus 2021/2022

Water Institute WI Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Water Institute – WI have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about WI Prospectus 2021/2022, how to […]

This post Water Institute WI Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Public Health Specialist – Data Analyst at United States Embassy Tanzania

U.S. MISSION DAR ES SALAAM VACANCY ANNOUNCEMENT The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and qualified applicants for the positions below (Click link below to read full job descriptions and mode of application…): Position Title: Public Health Specialist – Data Analyst (All Interested Candidates) Vacancy Number: DaresSalaam-2021-029 Open to: All Interested Candidates/All Sources Opening […]

This post Public Health Specialist – Data Analyst at United States Embassy Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Kilimanjaro Christian Medical College KCMUCO Prospectus 2021/2022

Kilimanjaro Christian Medical College KCMUCO Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Kilimanjaro Christian Medical College – KCMUCO have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about KCMUCO […]

This post Kilimanjaro Christian Medical College KCMUCO Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Stella Maris Mtwara University College STEMMUCO Prospectus 2021/2022

Stella Maris Mtwara University College STEMMUCO Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Stella Maris Mtwara University College – STEMMUCO have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details […]

This post Stella Maris Mtwara University College STEMMUCO Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger