Wednesday 7 December 2022

BUNGE LAPITISHA SHERIA HAKUNA KUJAMIIANA KAMA HAMJAFUNGA NDOA


Bunge la nchini Indonesia limepitisha sheria mpya inayokataza watu kujamiana kama hawajafunga ndoa, ikijumuisha mpaka wageni wanaoingia nchini humo.

Kupitia sheria hiyo mpya wapenzi ambao watashiriki tendo la ndoa na hawajafunga ndoa watafungwa jela mwaka mmoja kwa kuvunja sheria.

Pia ni marufuku kwa mwanamke na mwanaume kuishi pamoja bila ndoa, kifungo chake ni miezi 6 ukivunja sheria.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 7,2022



























Share:

Tuesday 6 December 2022

CCM YAPITISHA MAJINA 374 YA WAGOMBEA UJUMBE WA NEC....ORODHA YOTE HII HAPA

 

NA DIRAMAKINI

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)-NEC imepitisha majina ya wagombea 374 kuwania ujumbe wa NEC.

Wagombea hawa watachuana kuwania viti 30 kwa maana ya 15 Tanzania Bara na 15 Zanzibar katika mkutano mkuu wa CCM unaoanza Desemba 7 hadi 8,2022.

Kikao cha kuchuja majina ya wagombea zaidi ya 2,000 kimefanyika leo Desemba 2022 chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tanzania Bara wamepitishwa wagombea 251 watakaowania nafasi 15. Kati ya hao 251, wanawake ni 79 na wanaume 172;










KUTOKA ZANZIBAR, MAJINA YALIYOPITISHWA



Share:

AMUUA KAKAAKE MKUBWA WAKIGOMBANIA PENZI LA DADA YAO



aafisa wa Upelelezi wanamsaka mwanamume wa umri wa miaka 31 ambaye anadaiwa kumuua kakake mkubwa katika kisa cha madai ya ugomvi wa kimapenzi unaohusisha dada yao mdogo katika eneo la Kirinyaga nchini Kenya.

Inasemekana mshukiwa alimpiga kakake mwenye umri wa miaka 37 kwa kutumia kifaa butu kichwani, usoni na mgongoni baada ya kumpata katika mazingira ya kutatanisha na dada yao wa kambo mwenye umri wa miaka 17.



Idara ya DCI ilisema kwamba ndugu hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yao mwenye umri wa miaka 17.

“Marehemu pia alikuwa na mapenzi ya siri na msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 na hakuweza kukubaliana na kile alichokishuhudia,” taarifa hiyo ilisema.

Marehemu aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Karatina.

Maafisa wa Upelelezi waliofika katika eneo la mkasa waligundua kuwa marehemu awali alikuwa amedaiwa kumpa ujauzito dada yao mwaka jana, lakini alipoteza ujauzito huo mwezi Machi mwaka huu
Share:

TANZANIA, ZAMBIA WAKUTANA KUJADILI USALAMA BOMBA LA MAFUTA

Waziri wa Nishati Mh. January Makamba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhe. Peter Chibwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa ulinzi nchini Zambia, Mhe. Ambrose Lufuma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili amna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli. Mkutano ambao umefanyika leo Desemba 6,2022 Jijini Dar es Salaam.

**********

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati imekutana na Serikali ya Zambia kujadili namna ya kuongeza ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline mara baada ya kubadilisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli.

Akizungumza katika leo Desemba 6,2022 katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amesema kwa sasa inahitajika ulinzi zaidi katika bomba hilo ili kulinda usafirishwaji wa mafuta hayo na ndo maana wamekutana viongozi wa pande zote mbili ili kujadili usalama wa Bomba hilo.

"Kama tukisafirisha diseli maana yake usalama wa bomba unakuwa ni jambo kubwa kwa sababu inaweza kutokea kuchepushwa, hivyo sasa tukaamua serikali zetu mbili kufanya uratibu wa usalama wa hili bomba” Amesema Mhe. Makamba

Kwa upande wake Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhe. Peter Chibwe ameeleza kuwa hapo awali ambapo walikuwa wanasafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania kwenda Zambia ambako yanachakatwa gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa na serikali yao ilikuwa ikitumia ruzuku kubwa hivyo ni wakati sasa wamefanya mapinduzi kwa kusafirisha mafuta ambayo tayari yameshachakatwa.

"Ni wakati wa kufikiria ikiwezekana tuweze kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Tanzania kwenda Zambia hali itakayosaidia kupunguza ukataji miti ovyo kwa ajili ya mkaa na kuni na kuwezesha kutunza mazingirakatika nchi hizi mbili". Amesema

Naye Waziri wa ulinzi Zambia, Mhe. Ambrose Lufuma ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa jambo hili pamoja na timu ya ufundi kwa kufanya kazi nzuri ndani ya siku mbili walizokaa ambapo wameweza kuja na mipango mbalimbali itakayotumika kulinda bomba hilo ikiwemo ufungaji wa camera za CCTV, matumizi ya drones na kuweka askari kwa ajili ya ulinzi masaa yote.

Share:

SHIRIKA LA TCRS LAENDESHA MAFUNZO YA STADI ZA MAISHA KWA MABINTI BALEHE, WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KISHAPU


Watetezi wa haki za Binadamu na wadau wa maendeleo ya jamii Mkoani Shinyanga likiwemo shirika lisilo lakiserikali linalojihusisha na utoaji wa misaada ya kibinadamu na utunzaji wa mazingira la TCRS wameunga mkono juhudi za Serikali kupinga ukatili wakijinsia kwa kutoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana balehe,wanawake vijana na watu wenye ulemavu walioathirika na vitendo vya ukatili kupitia mradi ujulikanao kama CHAGUO LANGU - HAKI YANGU unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na UNFPA na kutekelezwa na TCRS na WILDAF.


Mratibu wa miradi ya TCRS Kellen Machibya amesema mradi huo unashirikisha makundi matatu ya wasichana kuanzia umri wa miaka 10 hadi 19 ambayo ni wasichana balehe, wanawake vijana na wasichana wenye ulemavu ambapo ameeleza kuwa malengo makuu ni kuwafundisha stadi za maisha ili waweze kuishi kama watu wengine na kujiepusha na vishawishi vinavyosababisha vitendo vya ukatili.


Baadhi ya walengwa wa mradi huo wamesema awali walikuwa hawavijui vitendo vya ukatili ni nini hali iliyowasababishia kufanyiwa ukatili bila kujua na kupata madhara lakini baada ya kupata elimu ya stadi za maisha itawasaidia kuishi maisha ya kawaida na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kusababisha wafanyiwe ukatili.


Mariam Lyiuba ni mmoja kati ya mabinti walionusurika kuozeshwa akiwa na umri mdogo amesema baada ya kupata elimu hiyo yeye na wenzake wako tayari kueneza elimu hiyo kwa mabinti na wanawake wengine ili jamii iondokane na changamoto ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji wakijinsia.


Mratibu wa mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu Regina Hipolit amesema makundi hayo matatu yaliyotajwa ni waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili lakini elimu hiyo imelenga kuwakomboa kiuchumi kwakuwa wanafundishwa mabo ya lishe, afya ya uzazi pamoja na kujikinga na ukatili wakijinsia ambapo vijana hao walikuwa hawana uelewa juu ya mambo hayo na elimu hiyo itawasaidia kujua haki zao kwenye maisha.


Mwezeshaji wa mafunzo ya stadi za maisha kupitia MRADI WA CHAGUO LANGU HAKI YANGU Bi. Vestina Mtakyawa amesema tatizo kubwa linalowapata babinti wanaopata mimba za utotoni ni kushindwa kuwalea watoto na kusababisha changamoto ya utapiamulo, magonjwa mbalimbali, na ongezeko la watoto wa mitaani lakini kwa kupata elimu hiyo mimba za utotoni zitapungua lakini pia vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga vitapungua.


Afisa maendeleo ya jamii kata ya Maganzo Neema Gweso amesema mabinti balehe na wanawake vijana ni kundi linaloathirika zaidi na vitendio vya ukatili wakijinsia katika jamii na ukatili ulioshamiri zaidi ni mabinti kuozeshwa wakiwa na umri mdogo, kuwaogesha dawa ya mvuto wa mapenzi ijulikanayo kama samba sababu kuu ni wazazi kutafuta utajiri wa haraka.


Fatuma Katabaro ni msaidizi wa kisheria kutoka kishapu para-legal organization amesema kupitia mradi huo wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU kesi nyingi za ukatili zinazofikishwa kwao zitapungua kwakuwa hali ya ukatili wakijinsia kabla ya hapo ilikuwa ni kubwa changamoto mtambuka ikiwa ni jamii kutotambua kuwa mtoto ni nani.

Afisa ustawi wa jamii mkoa wa shinyanga Lydia Lwesigabo amesema vitendo vya ukatili na unyanyasaji wakijinsia bado vinaendelea kushamiri mkoani humo huku akivitaja kuwa ni akitaja ukatili wakingini,ulawiti,ubakaji na utelekezaji wa watoto na vipigo mila na kutaja mila na desturi potovu kuwa chanzo mtambuka kwa ukatili.


Aidha amesema serikali inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo tcrs na vyombo vya habari kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu wa TCRS wakiongozwa na mpango mkakati wa kutokomeza ukatili wakijinsia kwa wanawake na watiotoi (MTAKUWWA).
Mratibu wa Miradi TCRS, Kellen Machibya akizungumza

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Mratibu wa Mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu Maganzo wilayani Kishapu, Regina Hipolit akizungumza

Mwezeshaji wa mafunzo Vestina Mtakyawa akizungumza
Mwezeshaji wa mafunzo Vestina Mtakyawa akizungumza


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger