Tuesday 5 July 2022

KUTANA NA MZEE ANAYE TREND NA MSEMO MAARUFU WA "KATA SIMU TUPO SITE"


Iwapo umedurusu mitandao ya kijamii, huenda umekutana na video ya mzee mmoja kwenye simu yake akimtaka aliyempigia kukata simu kwa kutumia neno "Kata simu kata simu tupo site we don't like disturbance of the head you understand."

Tayari wanamtandao wengi wanatumia msemo huo kama meme, video, na pia katika majukwaa ya kisiasa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa manifesto ya kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoyah. Aliyeanzisha msemo huo ni msanii mcheshi, Umar Iahbedi Issa almaarufu Mzee Mjegeje mwenye kutoka nchini Tanzania.

Akizungumza katika mahojiano ya awali, Mzee Megeje alibainisha kuwa anavutiwa na sanaa na anataka kuunda maudhui ambayo yanawavutia hadhira.

Mjegeje aliyezaliwa na kukulia huko Bagamoyo, Tanzania, alijieleza kuwa ni mfanyabiashara ambaye alitafuta riziki kutokana na ujasiriamali. Kabla ya kujitosa kwenye sanaa, mchekeshaji huyo mwenye utata alikuwa anamiliki hoteli kubwa nchini Tanzania ambayo ni biashara yenye faida ambayo alikuwa ameweka akiba yake ili kuanzisha.

Hoteli hiyo yenye makao yake makuu katikati ya jiji la Tanga, ilionekana kuwa eneo la kimkakati huku wateja mbalimbali wakimiminika kwa ajili ya kupata chakula. Hata hivyo, alidai kuwa wafanyikazi wake walihusudu mafanikio ya biashara yake na walipanga mpango wa kuangusha biashara yake. Wakati huo, alikuwa akijishughulisha na mipango ya harusi na mpenzi wake, na hivyo kuacha biashara chini ya uangalizi wa wafanyikazi. Alidai kuwa wafanyakazi hao waliharibu biashara yake.

“Nilikuwa na mali nyingi lakini kwa kusalitiwa na marafiki na wafanyakazi, waliniacha na madeni makubwa yaliyoniacha katika hali mbaya ya kifedha.” "Kwa muda wa miezi mitatu, sikuondoka nyumbani kutokana na wakusanyaji wa madeni walikuwa wakinitafuta," alisimulia. Akifunga duka, Megeje alibainisha kuwa alijitosa katika muziki na ubunifu wa maudhui kwa kutumia ujuzi wake wa kuchekesha.

Mchekeshaji huyo alifichua kuwa alitengana na mkewe, lakini akabainisha kuwa bado wana uhusiano mzuri na pamoja wamejaliwa mtoto mmoja.

Aliwashauri vijana kufanya kazi kwa bidii na kujipatia kipato kutokana na jasho lao na pia alisisitiza umuhimu wa kitengo cha familia katika jamii.
Share:

BENKI YA CRDB KATIKA MAONESHO YA 46 YA SABASABA


Mgeni Rasmi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wankele Mene (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul, wakati alipotembelea banda hilo, katika ufunguzi rasmi wa maonesho hayo yanayaendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji.
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wankele Mene (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki (kulia), pindi alipotembelea banda hilo, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo yanayaendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayaendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Meneja wa Biashara wa Kanda ya Mashariki, George Yatera (katikati) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (kushoto) akizungumza na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki, wakati wa maandalizi ya kumkaribisha Mgeni Rasmi wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Wankele Mene, katika banda lao.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Bwana akiyetembelea banda la Benki ya CRDB katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la sabasaba, Angelita Msaki.
Share:

BENKI YA CRDB NA WAKALA WA SERIKALI MTANDAO ZANZIBAR WAINGIA MAKUBALIANO


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government ), Said Seif Said muda mfupi baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa Huduma ya Malipo kwa Mtandao baina ya Benki ya CRDB na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government), utakaolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa Wateja na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kurahisisha ukusanyaji mapato, malipo ya Taasisi za Serikali na binafsi ikiwamo ada na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection). Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Hoteli ya Park Hyatt, Unguja, Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government ), Said Seif Said wakitiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa Huduma ya Malipo kwa Mtandao baina ya Benki ya CRDB na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government), utakaolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa Wateja na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kurahisisha ukusanyaji mapato, malipo ya Taasisi za Serikali na binafsi ikiwamo ada na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection). 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akizungumza katika hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa Huduma ya Malipo kwa Mtandao baina ya Benki ya CRDB na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government), utakaolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa Wateja na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kurahisisha ukusanyaji mapato, malipo ya Taasisi za Serikali na binafsi ikiwamo ada na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection), katika hafla iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Park Hyatt, Unguja, Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government ), Said Seif Said (kulia) akizungumza katika hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa Huduma ya Malipo kwa Mtandao baina ya Benki ya CRDB na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government), utakaolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa Wateja na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kurahisisha ukusanyaji mapato, malipo ya Taasisi za Serikali na binafsi ikiwamo ada na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection), katika hafla iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Park Hyatt, Unguja, Zanzibar.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (kushoto) na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa wakifatilia hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa Huduma ya Malipo kwa Mtandao baina ya Benki ya CRDB na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (E-Government), utakaolenga kuboresha huduma zitolewazo kwa Wateja na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kurahisisha ukusanyaji mapato, malipo ya Taasisi za Serikali na binafsi ikiwamo ada na kusaidia ukuaji wa utalii kwa kuwa na kituo kimoja cha makusanyo (one centre collection), katika hafla iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Park Hyatt, Unguja, Zanzibar.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 5,2022

Magazetini leo Jumanne July 5,2022












Share:

Monday 4 July 2022

NBC KUTOA TZS 65M KWA WASHIRIKI NBC DODOMA INTERNATIONAL MARATHON


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu(wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC, David Raymond wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa zawadi watakazokabidhiwa washindi wa mbio za Kimataifa za NBC Dodoma international Marathon 2022.Kulia ni mtangazaji wa kipindi cha Joto la asubuhi, Gerland Hando pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EFM, Denis Busulwa.Benki hiyo imetangaza kutoa jumla ya Sh65 milioni kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyia Julia 31,2020 mkoani Dodoma.
 Haijawahi kutokea! ndivyo unavyoweza kuzielezea zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio za NBC Dodoma International Marathon ambapo jumla ya Sh65 milioni zitagawiwa kwa washindi 15 watakaoibuka kidedea kwenye mbio hizo.

 Mbio hizo za Kimataifa zitakayofanyika siku ya Jumapili, Julai 31,2022 mkoani Dodoma na zitahusisha Kilomita 42, Kilomita 21 na kilomita 10 huku dhumuni likiwa ni kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

 Akitangaza zawadi za washindi, Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond alisema maandalizi yamekamilika na kwamba zawadi zitakazotolewa zimelenga kutoa hamasa kwa wakimbiaji hasa wa ndani.

Mshindi wa kwanza katika mbio za Kilomita 42 kwa upande wa Wanaume na Wanawake ataondoka na kitita cha Sh8, 000,000 kila mmoja huku wa pili akijitwalia Sh4, 000,000 wa tatu Sh2, 000,000 wa nne Sh1,500,000 huku wa tano akijitwalia Sh1,000,000. 

“Kwa kuzingatia kuwa mcheza kwao hutunzwa, kwa mtanzania ambaye atakuwa wa kwanza ‘Overall Winner’ atapata Shilingi milioni nane na ataongezewa Shilingi milioni 2 kwahiyo ataondoka na jumla ya Shilingi milioni 10,” alisema.

 Kwa upande wa Kilomita 21, mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni nne ambapo mtanzania atakayeshika nafasi hiyo kuongezewa Shilingi Milioni moja na kufanya jumla ya Shilingi 5,000,000. 

Mshindi wa pili atapata Sh2, 000,000, wa tatu 1,500,000 wa nne 1,000,000 wakati wa tano atajitwalia Sh. 700,000.

 Mbio za Kilomita 10 mshindi atajipatia Sh. 1,500,000 wa pili Sh. 1,000,000 wa tatu Sh. 700.000 wa nne Sh. 500,000 wakati wa tano atajishindia Sh. 300,000. 

Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu alisema mbio za mwaka huu zimelenga katika kutoa elimu ya saratani ambapo wameshirikiana na taasisi ya Ocean Road ili kufanikisha zoezi hilo. 

“Kikubwa kwenye zoezi hili ni kutengeneza utamaduni wa kupima mara kwa mara na sisi tunaamini kwa kutumia Marathon hii itatupa platform(jukwaa) kubwa zaidi na tunaamini tutawafikia watu wengi zaidi,” alisema. 

Aliongeza kuwa mbio hizo zitasaidia katika kufungua mipaka ya kibiashara katika mambo mbalimbali ikiwamo zao la zabibu ambapo wawekezaji watapata fursa ya kujionea uzalishaji wake na namna gani wanavyoweza kushikrikiana na Serikali kwenye eneo hilo. Ili kujisajili kushiriki kwenye mbio hizi za kimataifa, unaweza kutembelea tovuti ya events.nbc.co.tz na kulipia ada ya Sh30,000 kwa mbio zote ambapo utajipatia vifaa vya kukimbilia ikiwamo jezi. Mwisho//
Share:

WMA YAANZISHA VITUO ZAIDI YA 5000 VYA UKAGUZI NCHI NZIMA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Stella Kahwa (wa tatu kushot) akiwa pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Taasisi hiyo katika picha ya pamoja kwenye banda lao katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud S. Kigahe (kushoto) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa mara baada ya kutembelea banda la WMA katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (TWA) Bi. Stella Kahwa (wa tatu kulia) akizungumza na Moja ya Mtangazaji wa kipindi Maalum cha Sabasaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea JijiniDar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (TWA) Bi. Stella Kahwa (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na baadhi ya watumishi wa Taasisi hiyo.



Na: Mwandishi wetu, DAR
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Stella Kahwa amesema kuwa Taasisi hiyo imeainisha vituo zaidi ya elfu tano nchi nzima kwaajili ya kufanya ukaguzi ili kuendelea kuhakikisha mtanzania anapata Bidhaa iliyo katika ujazo na vipimo vinavyostahili sambamba na kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu.


Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Stella Kahwa katika mahojiano na waandishi wa habari Julai 3,2022 kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


Kahwa amesema kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kumeleta matokeo chanya na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto mbalinbali zilizokuwa zikiwakabili walaji na kwamba kwa sasa wengi wao wanafanya biashara zao kwa kufuata taratibu zilizopo.


"Kwa sasa Changamoto hii imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunapoenda kufanya kaguzi hatukutani na waliokiuka taratibu hata wale wanaopigwa faini wamepungua sana hadi kufikia asilimia 80 na 85" amesema.


Aidha ameendeleakutoa mwito kwa wafanyabiashara na walaji kwa ujumla kuendelea kufuata taratibu zilizopo ili kila mmoja aweze kunufaika.


Pia amewakaribisha wananchi wote hususani wafanya Biashara kufika kwenye Maonesho ya sabasaba na kutembelea Banda lao ili kujifunza na kufahamu namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.


"Nawaambia wafanyabiashira waje hapa sabasaba wajionee namna ambavyo wakala wa vipimo inavyofanyakazi, Wakala wa Vipimo iko Juu hivi sasa" alihitimisha Kahwa.


Kwa upande wake Afisa Vipimo Mkuu WMA, Bw.Gaspar Matiku amesema kuwa kwa sasa WMA imejipanga kuhakiki vipimo kwenye gari ndogo za biashara (tax) kwa kufunga tax meter ambazo zitasaidia kufahamu mteja ametembea kwa umbali fulani na kuweza kulipa fedha halali ambayo inalingana na umbali aliotembea.


Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujua umbali na fedha ambayo inatakiwa kulipwa na mteja kutokana na umbali uliotumika.


“Biashara ya Tax imekuwa kubwa na inatumika, sasa badala ya mtu kutamkiwa kwamba unatoka hapa ninakwenda sehemu fulani, huyu anakumbia utanipa elfu 20 na mwingine anakuambia utanipa elfu 30 kwa hiyo hakuna usawa kwenye hiyo ruti” Amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger