Thursday 26 November 2020
TPB BENKI YATOA MSAADA VITENDEA KAZI OFISI YA ARDHI MKOA WA TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa mbili na printa moja zilizotolewa na Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya milioni 3.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu kwa ajili ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Tanga Mkuu WA Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa mbili na printa moja zilizotolewa na Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya milioni 3.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu kwa ajili ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Tanga Mkuu WA Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa mbili na printa moja zilizotolewa na Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya milioni 3.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu kwa ajili ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Tanga
BENKI ya Posta imetoa msaada wa vitendea kazi kompyuta mbili na printa moja zenye thamani ya milioni 3.5 kwa ajili ya ofisi ya Ardhi mpya Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu yao ya kuisaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu alisema msaada huo ni wajibu wao kama benki wakiwa wanaihudumia jamii hivyo wakaona umuhimu wa kuisaidia jamii katika kukutana na changamoto mbalimbali.
Alisema kwamba wanaamini hivyo vifaa ambavyo wamevitoa vitasaidia kuwahudumia wananchi na kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga .
“Hivyo tunaamini vifaa tulivyovitoa leo vitasaidia kuwahudumia wananchi na kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga “Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha.
Awali akizungumza mara baada ya kupokea hivyo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliishuku Benki hiyo kwa msaada huo ambao wameutoa kwa ajili ya ofisi ya ardhi mkoa huo.
Alisema kwamba kama wanavyofahamu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Magufuli imejipambanua kwenye kufanya maboresho na kutatua changamoto za ardhi katika Taifa letu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema ardhi inachangamoto nyingi sana na kwa mkoa huo hivyo anafarijika kuona kwamba ofisi imefunguliwa ikiwa inahitaji mahitaji mengi ikiwemo upatikanaji wa thamani na vifaa kama ambavyo vimekabidhiwa.
“Hivyo niwaambie kwamba mmekuja wakati muafaka kusawaidia na kuwapatia huduma watumishi wetu wa ofisi ya ardhina vifaa hii sio kwamba watavitumia kwa maslahi yao bali ni kwa maslahi ya wananchi wa mkoa wa Tanga “Alisema RC Shigella.
Hata hivyo aliwaishukuru benki hiyo kwa msaada huo huku akieleza kwamba ni matumaini yake kuona vifaa hivyo vinatunza na ili viweze kudumu na kupata thamani.
“Lakini niwaambie wananchi wa mkoa watembelea ofisi ya ardhi wapate hati na waweze kuzitumia kwa ajili ya kukopa na eneo pekee ni benki ya posta lakini wafungue akanti zao kwenye benki hiyo”Alisema RC Shigella.
Wednesday 25 November 2020
BABA ASAKWA KWA KUMUUA MTOTO WAKE
TAREHE 22.11.2020 MAJIRA YA 11:30HRS HUKO KATA YA BUSWELU, WILAYA YA ILEMELA, ATHUMAN ADAM, MIAKA 10, MKEREWE, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU, SHULE YA MSINGI NYAMADOKE, BUSWELU, ALIUAWA KWA KILE KICHODAIWA KUSHAMBULIWA NA FIMBO SEHEMU ZA MWILI WAKE NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADAM ATHUMAN, MIAKA KATI YA 30-40, MKEREWE, FUNDI UJENZI, NYAMADOKE, MTUHUMIWA HUYO BAADA YA KUTEKELEZA UKATILI HUO ALITOROKA, NA JESHI LA POLISI LINAFANYA KILA JITIHADA KUHAKIKISHA ANATIWA NGUVUNI ILI AFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI HOSPITALI YA BUGANDO NA KUKABIDIWA NDUGU KWA MAZISHI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWAONYA NA KUTOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI WOTE KUWA MAKINI NA AINA YA ADHABU WANAZOTOA KWA WATOTO, KWANI WANAWEZA KUJIKUTA WAKITENDA MAKOSA YA KIJINAI NA HATIMAYE KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
25, NOVEMBA 2020
SAVE THE CHILDREN YATOA MAFUNZO JUU YA BAJETI INAYOMHUSU MTOTO
MNYIKA : MDEE NA WENZAKE WALIOAPISHWA WAMEJITEUA ...TUMEWAITA KWENYE KIKAO CHA KAMATI KUU
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa siku mbili kwa wanachama wake 19, ambao jana walikula viapo Bungeni vya kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachofanyika Novemba 27, 2020.
"Kwa kuwa jambo hili ni la dharura natangaza wito (Public notice), kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana, kufika makao makuu ya chama bila kukosa siku ya Ijumaaa ya Novemba 27, 2020, saa 2:00 asubuhi, kutoka popote pale walipo kamati kuu inaweza kuchukua hatua za dharura kama itaona maslahi ya jumla ya chama yanaweza kuathiriwa", amesema John Mnyika.
Aidha Mnyika akizungumzia suala la wabunge hao kula kiapo hicho amesema kuwa, "Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote ya mtu yeyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kujazwa na kiapo cha hakimu kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi ni kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi, wameenda kuapishwa bila baraka ya chama".
Wabunge 19 wanaotakiwa kuwasili siku ya ijumaa ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko na wengine walioapishwa kwa siku ya jana katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.