Sunday 25 October 2020

WANAOISHI MLIMA ULUGURU KUFUNDISHWA MBINU ZA KUENDELEA KUISHI HUKO BILA KUSHUSHWA


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manispaa ya Morogoro Bwana fikiri Juma jukwaani ( Wa Kwanza Kulia) akiwa na Mgombea Udiwani bwana Juma Kiduka kwenye mkutano uliofanyika kwenye Mtaa wa Folkland. Wananchi wa Kata ya Magadu wakifuatilia Mkutano huo wa Kampeni wa kumnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo bwana Juma Kiduka. 

**************************************** 

Na: Calvin Gwabara. 

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Bwana Fikiri Juma amewahakikishia wananchi wanaoishi kwenye mlima Uluguru kuwa hawatashushwa bali watafundishwa njia na mbinu bora za kuishi milimani kama wanavyofanya watu wa Lushoto na kwingine duniani. 

Fikiri ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni ya Udiwani kwenye kata ya Magadu ambayo sehemu ya jamii ya watu wa kata hiyo wanaishi kwenye mlima Uluguru na kuendesha shughuli za Kilimo na ufugaji.

 “ Tumezielekeza Taasisi mbalimbali za Misitu kuacha kwenda kupanda miti kwenye mlima huo badala yake miti hiyo ipandwe na wananchi wa maeneo hayo ili waweze kuitunza tofauti na sasa ambapo miti inayopandwa inakauka kwakuwa wananchi hao wanaona sio sehemu yao na hivyo kukauka” Alisema Bwana Fikiri.

 Akimnadi Mgombea Udiwani wa kata hiyo Juma Kiduka Mwenyekiti huyo wa CCM Manispaa ya Morogoro amesema Serikali ya CCM inajenga viwanda nchi nzima sio tu kutoa ajira bali kuwezesha Wakulima wa Morogoro na nchi nzima kupata Soko la uhakika wa mazao yao.

 “ Hapo Mkambarani kwa pembeni kuna kiwanda cha mfano cha Kisindika mazao ya mikunde kwenye Mkoa wetu kitasaidia sana kuinua maisha ya Wakulima wa Mazao hayo ya Mikunde na ajira kwa vijana na Mama zetu” Aliongeza Bwana Fikiri.

 Amesema kitendo cha kwenda kuuza mali ghafi nchi za nje kunapeleka ajira pia kwa watu wa nje lakini viwanda vikiwa hapa nchini vitatoa ajira hizo kwa vijana na watanzania na hivyo kusaidia kuchichea maendeleo ya Taifa hili ambalo asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wale wanategemea Kilimo.

 Amebainisha kuwa ilani ya CCM ya miaka mitano 2015 hadi 2020 imetekelezwa kwa asilimia 100% ndio maana Chaka kinampa nafasi nyingine ya kusimamia ilani ya CCM kwa miaka mingine mitano na hakuna ubishi kuwa atashinda kwa kishindo. 

Bwana Fikiri amesema kazi iliyopo mbele ya Wana Morogoro Mjini kumchagua Azizi Abood kuwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kiduka kuwa Diwani wa kata ya Magadu na Rais John Pombe Magufuli kuwa Rais wa awamu ya sita ili amalizie kazi kubwa aliyoianza ya kuleta maendeleo ya Tanzania.

 Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa kata ya Magadu Juma Kiduka amesema kuna kazi kubwa inafanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kuleta maendeleo ya kata ya Magadu na Jimbo la Morogoro Mjini hivyo kama Mtumishi wao anakwenda kuwa Mtumishi wao atakayesimamia miradi hiyo ili maendeleo yafikiwe.

 Akizungumzia changamoto ya maji amesema tayari kuna Mradi Mkubwa wa maji unaendelea kwa sasa na utakapokamilika utatatua changamoto zote za maji kwenye kata na Jimbo la Morogoro mjini hivyo waendelee kuiamini CCM maana sera zake zinatekelezeka.

 Awali akizungumza kwenye Mkutano huo Aliyekuwa Meya wa Zamani wa Manispaa ya Morogoro Prof. Romanus Ishengoma amewataka wakazi wa kata hiyo kumuamini Rais John Pombe Magufuli na wagombea wa CCM Kwani amefanya kazi kubwa katika Historia ya Tanzania.

 “Mimi mnadhani Nipo CCM kwa bahati mbaya? Simnajua nina akili kubwa sio? Nipo CCM kwakuwa nina uhakika na kazi za CCM, Sera zake na Wagombea wake” Alisisitiza Prof. Ishengoma. 

Kampeni zinaendelea kupambana Moto katika dakika za lala salama zikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Wananchi wa Tanzania kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Share:

ASKOFU SANGU : JITOKEZE KAPIGE KURA KISHA RUDI NYUMBANI..USIWE CHIMBUKO LA MACHAFUKO WAKATI WA UCHAGUZI


Askofu Liberatus Sangu

Na Simeo Makoba - Simiyu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amewataka Wakatoliki na Watanzania wote kuepuka kuwa chimbuko la machafuko katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

Askofu Sangu ametoa rai hiyo leo Jumapili Oktoba 25,2020 katika misa ya Kipaimara iliyofanyika katika Parokia ya Mwanhuzi wilayani Meatu moani Simiyu zikiwa zimebaiki siku mbili tu za kufanyika kwa zoezi la upigaji wa kura kumchagua Rais,Wabunge na Madiwani.

Askofu Sangu amewataka Watanzania kujitokeza kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka huku wakizingatia maelekezo yanayotolewa na Mamlaka zilizowekwa pamoja na kuhakikisha hawashiriki matukio ya aina yoyote ambayo yanahatarisha amani ya nchi.

“Mkatoliki yeyote mahali popote ulipo usiwe chimbuko la machafuko, timiza wajibu wako wa kupiga kura na kurudi nyumbani, mengine yote ya kuleta vurugu yanatoka kwa muovu na mwenye pepo , tujitayarishe sote kupiga kura kwa amani tukiongozwa na Mungu roho mtakatifu”, amesema Askofu Sangu.

Askofu Sangu amebainisha kuwa amani iliyopo nchini ni tunu pekee ambayo Tanzania imetunukiwa na kwamba kila mmoja anapaswa kuhakikisha anailinda ili iendelee kuwepo.

Katika hatua nyingine Askofu Sangu amewataka watu wote kuwa wajumbe wa amani na ametoa maelekezo kwa waamini wa jimbo lake kusali sala maalum ili kuombea amani ya nchi katika kipindi hiki taifa linapoelekea katika kipindi maalum cha uchaguzi.



Share:

DK. HUSSEIN MWINYI AHITIMISHA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UCHAGUZI ZANZIBAR....KIKWETE ATIA NENO


MWINYI DAY 28: Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi zimefungwa rasmi Leo Jumapili Oktoba 25, 2020 kwenye Viwanja Vya Kibanda Maiti na Mgombea huyo makini na mzoefu mkubwa kabisa amepata nafasi ya kuhutubia Kwenye Mkutano wake huo wa Mwisho wa Kampeni. na haya ndiyo aliyoyaongea Kwenye Kufunga Kampeni hizo ambazo zimehudhuriwa pia na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Mgombea Mwenza Urais Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan. Zanzibar iko tayari na Dkt Mwinyi na mitambo imeshatiki inasubiri tu Oktoba 28.

#YajayoniNeematupu
#Mwinyi2020
Share:

MAGUFULI KUHITIMISHA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI KESHO DODOMA

 

Baada ya siku 60 za kuzunguka nchi nzima kukutana na Watanzania na Kunadi Sera na Ilani bora ya CCM, hatimaye Mgombea Urais wa CCM anahitimisha Kampeni zake Dodoma na kurudi Makao Makuu.

Ni Kesho Jumatatu Oktoba 26, Dkt John Pombe Magufuli atahitimisha Kampeni zake Mkoani Dodoma. Watanzania wamesikia na wamejionea Sera nzuri zilizohubiriwa na CCM kote nchini na Sasa wako tayari kutoa kura Zote kwa CCM.

#KuraKwaMagufuli2020

#T2020JPM

Share:

NKULILA AUNGURUMA NDEMBEZI, AAHIDI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

 Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi sera za CCM na kuomba kura kwa wananchi

Na Marco Maduhu  Shinyanga. 

Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amewaomba wananchi wa Kata hiyo wamchague kwa awamu nyingine tena kuwa diwani wao, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, ili akamilishe miradi ya maendeleo ambayo aliianzisha kwenye kipindi kilichopita. 

Nkulila ametoa ahadi hizo leo kwenye mkutano wake wa kampeni katika mtaa wa Tambukareli, wakati akinadi sera zake kwa wananchi wa Kata ya Ndembezi, kuwa wamchague tena ili aendelee kuwa letea maendeleo ikiwamo kupigania haki za wanyonge. 

Alisema wananchi wa kata hiyo wasije wakafanya makosa siku ya uchaguzi, na kumpigia kura mgombea mwingine wa upinzani, bali wakampigie kura nyingi za ushindi ili aendelee kuwaletea maendeleo, pamoja na kukamilisha miradi mikubwa ambayo aliianzisha ukiwemo wa machinjio ya kisasa na kituo cha afya. 

“Mimi ni diwani mpenda maendeleo na ni mtetezi wa haki za wanyonge, hivyo nipigieni kura nyingi za ushindi siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, pamoja na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi, na mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli ili kwa pamoja tuwaletee maendeleo,”alisema Nkulila. 

“Katika kipindi kilichopita cha uongozi wangu kama diwani wa Kata hii, nadhani mmeshuhudia kazi ambazo nilizifanya, ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, na upimwaji wa viwanja, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kalogo hadi Bugoyi, ujenzi wa machinjio ya kisasa, kituo cha afya, na awamu ijayo tutajenga kituo cha Polisi,”aliongeza. 

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, aliwataka wananchi hao wa Ndembezi siku hiyo ya uchaguzi, wakimaliza kumpigia kura mgombea Urais John Magufuli, Mgombea ubunge Patrobas Katambi, na madiwani wote wa CCM, waondoke kwenye vituo vya kupigia kura na kusubiri matokeo wakiwa nyumbani. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgombea udiwani CCM Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi Sera kwa wananchi ili wamchague Oktoba 28 kuwa diwani wao. Picha zote na Marco Maduhu
Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi (CCM) Manispaa ya Shinyanga David Nkulila akinadi sera za CCM na kuomba kura kwa wananchi
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mwenyekiti wa (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (kushoto), akimnadi Mgombea udiwani Kata ya Ndembezi David Nkulila kwa wananchi wa Kata hiyo, kuwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, wampigie kura za ushindi.
Baadhi ya wenyeviti wa mtaa kutoka Kata ya Ndembezi, wakiwa kwenye mkutano huo wa Kampeni.
Mkutano wa kampeni ukiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger