Monday 2 December 2019

Papa Msofe afikishwa Mahakamani kwa utakatishaji Fedha, Uhujumu Uchumi

Mfanyabiashara maarufu Marijan Msofe maarufu ‘Papaa Msofe’ na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha wa zaidi ya TSh.Mil 900.

Mbali na Msofe, washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili mwandamizi wa Serikali Ladslaus Komanya amedai washtakiwa wanadaiwa kufanya makosa hayo kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019 ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambapo walijipatia zaidi ya Shilingi Milioni 900.
 

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi, hivyo haina dhamana ambapo shauri hilo limehairishwa hadi December 16, 2019.


Share:

Picha : RC TELACK AZINDUA RASMI USAJILI WA LAINI ZA SIMU SHINYANGA... ''HAACHWI MTU NYUMA,KAMILISHA USAJILI"

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amezindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji kwa wananchi wasajili laini zao za simu.


Uzinduzi huo ukiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Haachwi mtu nyuma,kamilisha usajili’ umefanyika leo Jumatatu Desemba 2,2019 wakati wa Mkutano wa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole uliofanyika katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga 

Akizungumza mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack amewataka wananchi kujitokeza kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole/kibaiometria ambao ni utaratibu wa kusajili laini za simu wa uhakika zaidi.

“Kitambulisho kinachoruhusiwa kutumika katika usajili wa laini za simu ni kitambulisho cha taifa kwani njia ya kibaiometria inafanyika kwa kutumia vifaa vya kielektroniki ambavyo vimeunganishwa kwenye mfumo wa vitambulisho vya taifa unaoratibiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)”,amesema Telack.

Amesema kutokana na changamoto ya wananchi kushindwa kusajili laini zao za simu kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha taifa,Telack amewaagiza maafisa wa NIDA mkoa wa Shinyanga kuweka kambi katika Uwanja wa Zimamoto kusaidia wananchi kupata namba za kitambulisho cha NIDA ili waweze kusajili laini za simu.

“Usajili wa laini unaendelea kufanyika kwenye maduka ya watoa huduma za mawasiliano na wakala wao na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 31,2019 ambapo laini ambazo hazijasajiliwa hazitaweza kutumika kwenye mawasiliano,NIDA ongezeni muda wa kuwa hapa ili muwasaidie wananchi wengi zaidi kupata namba za vitambulisho”,ameongeza Telack.

Mkuu huyo wa mkoa amewatahadhalisha wananchi kuachana na tabia ya kuazimana simu,kununua na kuuziana simu mtaani ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo pindi laini na simu kuonekana zimetumika kutekeleza vitendo vya uhalifu.

“Kila mtu anatakiwa asajili laini yake yeye mwenyewe,usithubutu kumsajilia mtu mwingine kwani endapo akifanya uhalifu vidole vilivyotumika kusajili vitaonekana ni vya kwako hivyo utajiingiza kwenye matatizo”,amesisitiza Telack.

Kwa upande wake, Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau amesema kati ya wananchi 619,915 waliojisajili NIDA,518,327 wameshapata namba za vitambulisho kwa ajili ya kutumia kusajili laini za simu.

Njau ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika kwenye ofisi za serikali za mitaa,vijiji na kata kwenda kuchukua namba za vitambulisho vya NIDA ili wasajili laini zao.

Akizungumza kwa niaba ya Makampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania, Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla amesema,makampuni ya simu yanaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuendesha zoezi la kuhamasisha wananchi wakamilishe usajili za laini zao za simu.

Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki amesema Usajili wa Laini za simu ni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (The Electronic and Postal Commucations Act) ya mwaka 2010 hivyo ni vyema kila mwananchi akasajili laini yake ya simu.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  akizungumza wakati wa kuzindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
kuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akionya wananchi kuacha tabia ya kuazimana simu,kununua na kuuziana simu mtaani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza akati wa kuzindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla
akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipiga picha na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipiga picha na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL namna wanavyoendesha zoezi la usajili wa laini za simu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL namna wanavyoendesha zoezi la usajili wa laini za simu.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisajili laini kwa kutumia kidole kwenye banda la Kampuni ya Simu ya TTCL.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akipokea laini ya TTCL baada ya kusajili kwa kutumia kidole kwenye banda la Kampuni ya Simu ya TTCL.
Wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiondoka katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Kundi la sanaa ' Shinyanga Art Group' linaloongozwa na Msanii Chapchap likitoa burudani.
Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau akitoa maelekezo kwa wananchi namna ya kupata namba za kitambulisho cha NIDA kwa kutumia simu ya mkononi kwa kutuma ujumbe kwenda namba 15096 bure.
Afisa Msajili NIDA wilaya ya Shinyanga, Haruna Mushi akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliojitokeza kuchukua namba za vitambulisho vya NIDA kwenye Banda la NIDA.
Afisa Msajili NIDA wilaya ya Shinyanga, Haruna Mushi akiwasaidia wananchi kuchukua namba za vitambulisho vya taifa kwenye Banda la NIDA.
Wananchi wakiwa kwenye foleni kuchukua namba za vitambulisho vya taifa kwenye banda la NIDA.
Zoezi la Usajili likiendelea katika Banda la NIDA ambapo wananchi wengi wamejitokeza kujiandikisha/kujisajili ili wapate vitambulisho vya taifa.
Wafanyakazi wa Vodacom wakiuza simu za mkononi.
Zoezi la usajili wa laini likiendelea katika banda la Halotel.
Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ukiendelea katika banda la Vodacom.
Burudani kutoka kundi la Shinyanga Art Group ikiendelea.
Ma DJ na ma MC mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye eneo la tukio.
Msanii Chapchap akitoa burudani ya wimbo.
Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla akiagana na Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki baada ya kuzindua zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Picha : SHIRIKA LA PACESHI LAENDESHA MAFUNZO KWA WASAIDIZI WA KISHERIA MKOA WA SHINYANGA




Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESHI), limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kisheria wasaidizi wa kisheria 64, kutoka kwenye halmashauri sita za mkoani Shinyanga, ili wakafanye kazi ya kuwahudumia wananchi wa hali ya chini kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.


Mafunzo hayo ambayo yatachukua muda wa siku 15, yamefunguliwa leo Desemba 2, 2019 na  Msajili Msaidizi wa watoa huduma za kisheria kutoka mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, kwenye ukumbi wa mikutano Kahama Super Lodge Mjini Kahama.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Ngwale, amewataka wasaidizi hao wa kisheria wakaitumie vyema elimu watakayopewa kusaidia wananchi wa hali ya chini kupata haki zao, ambao wamekuwa wakidhulumiwa mali kutokana na kutozijua sheria au kukosa fedha za kuweka mawakili kusimamia kesi zao.

Amesema wasaidizi hao wa kisheria wana msaada mkubwa ndani ya jamii hasa wale wa hali ya chini, ambapo wengi wao wamekuwa wakipoteza haki zao kwa sababu ya kutozijua sheria au ukosefu wa fedha za kulipa mawakili, lakini wasaidizi wa kisheria wataweza kuwasaidia kutafuta haki zao mahakamani bila ya kutoa pesa yoyote.

“Naombeni sana wasaidizi wa kisheria mafunzo haya mkayatumie vyema kusaidia wananchi kupata haki zao hasa wa hali ya chini, na msiende kuendekeza masuala ya rushwa, bali wahudumieni vizuri sababu nyie ndiyo msaada wao mkubwa,”amesema Ngwale.

“Pia mzipitie sheria vizuri zikiwamo zile zinazohusu masuala ya ukatili wa kijinsia hasa Sheria ya mtoto ya mwaka (2009), ili mkatokomeze vitendo vya mimba na ndoa za utotoni, kwa kuwasaidia wahanga wa matukio hayo, kuwashitaki wanaowatendea vitendo hivyo na kuwafunga jela,”ameongeza.

Naye Meneja Mradi wa huduma wa msaada wa kisheria John Shija kutoka Shirika la PACESH Shinyanga mjini, ambao ndiyo wawezeshaji wa mafunzo hayo, amesema wametumia kiasi cha Shilingi Milioni 100.8 kutoa mafunzo kwa wasaidizi hao wa kisheria, ili wakatumikie wananchi wa hali ya chini.

Amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kisheria namna ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hususani kwenye masuala ya ardhi, jinai, mikataba, ajira, mahusiano kazini, Sheria ya ndoa, mtoto, mirathi, migogoro ya ardhi,pamoja na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Aidha amesema mafunzo hayo yameshirikisha wasaidizi wa kisheria 64 kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga, ambazo ni Kahama Mji, Msalala, Ushetu, Kishapu, manispaa ya Shinyanga pamoja na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, chini ya ufadhili wa mfuko wa huduma za Sheria Legal Service Falility (LSF).

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Msajili Msaidizi wa Watoa Huduma za Kisheria  mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya  kuwajengea uwezo wa kisheria wasaidizi wa kisheria 64, kutoka kwenye halmashauri sita za mkoani Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Meneja mradi wa huduma wa msaada wa kisheria John Shija kutoka Shirika la PACESH Shinyanga mjini, akielezea madhumuni ya mafunzo hayo ya Sheria kwa wasaidizi wa kisheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.



Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa sheria.

Msaidizi wa kisheria Twaha Kiliza kutoka manispaa ya Shinyanga , akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo ya sheria.

Msaidizi wa kisheria Yasinta John, kutoka manispaa ya Shinyanga, akielezea namna watakavyo nufaika na mafunzo kupata uelewa mpana wa kisheria kwenda kuhudumia wananchi wa hali ya chini ambao hawazijui sheria ili kupata haki zao za msingi.

Wasaidizi wa kisheria kutoka halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Msajili msaidizi wa watoa huduma za kisheria mkoa wa  Shinyanga Tedson Ngwale.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Share:

Papa Francis amteua Ludovick kuwa Askofu mpya Jimbo la Moshi

Baba Mt. Francis amemteua Askofu Ludovick Joe Minde, kuwa Askofu mpya Jimbo la Moshi. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Askofu wa Kahama. 

Jimbo Moshi limekuwa wazi tangu Desemba 27, 2017 wakati aliyekuwa Askofu wake, Isaac Amani Massawe alipoteuliwa kuwa Askofu Mkuu, Jimbo la Arusha 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger