Saturday 29 June 2019

Watanzania Watakiwa kuchangamkia fursa ya mifuko mbadala

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala kwa kuwa mahitaji ni makubwa na soko ni kubwa.

Majaliwa amesema hayo jana Ijumaa Juni 28, 2019  wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha mkutano wa 15 wa Bunge la Tanzania.

Amesema uzalishaji wa mifuko hiyo hautoshelezi mahitaji kwa sasa.

Majaliwa amesema utekelezaji wa katazo la Serikali ya Tanzania la mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, wananchi wameonyesha mwitiko wa hali ya juu kutumia mifuko hiyo.

Amesema jumla ya viwanda 11 vimejikita kwenye uzalishaji wa mifuko mbadala 10 vikiwa Dar es Salaam na kimoja Arusha.


Share:

Kauli ya IGP Sirro Baada ya Watanzania 9 Kuuawa Msumbiji

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watanzania wapatao 9 wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa nchini Msumbiji ambako walikwenda kujitafutia riziki.

Akiongea leo mkoani Mtwara eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji amesema mauaji hayo yamefanyika Juni 26, 2019 ambapo pia watu wa Msumbuji kadhaa nao wameuawa.

''Waliofanya haya matukio tutawatafuta na nimeongea na IGP mwenzangu wa Msumbiji nimemuomba tukutane kesho Juni 30, 2019 ili tuongee juu ya tukio hili na mengine'', amesema.

IGP Sirro amesema amesikitishwa sana na vifo vya watanzania hao ambao wamepigwa risasi na watatumia kila njia kuwapa waliofanya mauaji hayo.

Pia ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na majeruhi 6 walionusurika kwenye mauaji hayo. Amewataka wananchi watoe taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wauaji hao.

Imeelezwa kuwa watanzania hao huenda nchini Msumbiji wakati wa msimu wa kilimo kwaajili ya kulima na kujipatia mazao pamoja na kipato.
 


Share:

Wabunge wa Upinzani Wapinga Tundu Lissu Kuvuliwa Ubunge

Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Tanzania wametoa maoni kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii kufuatia Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kutangaza kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kilichokuwa kikikaliwa na Tundu Lisu wa Chadema kiko wazi.

Spika Ndugai alitangaza uamuzi huo jana Ijumaa Juni 28,2019 kabla ya kuahirisha mkutano wa 15 wa Bunge la Bajeti akisema Lissu amepoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na sababu mbili za kutokutoa taarifa kwake (spika) na kutojaza fomu za mali na madeni kwa viongozi wa umma.

Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa Twiter ameandika kuwa “Mh Spika umemvua Mh Tundu Lissu Ubunge? Moyo wangu unavuja damu....Mungu nisaidie,”

Naye Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche ameandika katika ukurasa wake wa Twiter,  “Katika maisha yangu sijawahi kushuhudia unyama wa kiwango hiki,”

“Lissu alipigwa risasi mchana kweupe wakati wa vikao vya bunge,  hakuna mtu amekamatwa mpaka sasa, hakuna mtu alienda kumuona hospital akiwemo spika mwenyewe....Leo wanamvua ubunge?” ameandika Heche.




Share:

Makonda Amuomba Radhi Rais Magufuli

Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars, Paul Makonda amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli kufuatia Stars kupoteza mechi ya pili mfululizo.

Makonda ameomba radhi hiyo jijini Cairo kwamba kila Mtanzania alikuwa na imani ya kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Harambee Stars ambapo Stars ilifungwa bao 3-2.

Makonda amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuiombea timu yao na kuiunga mkono kwani matokeo hayo ni sehemu ya mchezo.

Mkuu huyo alisema licha ya Stars kupoteza ameridhika na jinsi kikosi hicho kilivyocheza kwa nguvu ikiwa ni tofauti na mchezo wa kwanza waliofunga na Senegal bao 2-0.


Share:

India yafanyia majaribio kombora lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia

Serikali ya India imelifanyia majaribio kombora la balestiki linaloitwa Prithvi II lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.

Majaribio ya kombora hilo la kutoka ardhini kuelekea angani la Prithvi II lilibebwa na trela la kubebea mizigo kwa umbali wa kilometa 350 kupitia maeneo ya mji wa Chandrapur wa jimbo la Odisha kusini mwa India.

 Kwa mujibu wa habari hiyo, kombora hilo la balestiki sambamba na kubadili mwelekeo, linaweza pia kuzuia utendajikazi wa mfumo wa makombora. 

Aidha kombora hilo linaweza kubeba vichwa vya mabomu ya kivita na nyuklia kutoka uzito wa kilogramu 500 hadi kilogramu 1000. 

Inafaa kuashiria kuwa, India na Pakistan zimekuwa katika ushindani mkubwa wa kumiliki silaha za nyuklia ambapo kila moja imekuwa ikifanya majaribio ya makombora tofauti yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.

Katika uwanja huo mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu Meja Jenerali Asif Ghafoor, Msemaji wa jeshi la Pakistan alitangaza kuwa, endapo kutatokea vita baina ya India na Pakistan, basi mwanzoni tu mwa vita hivyo, Pakistan itaisambaratisha miji ya Mumbai na New Delhi na kuisawazisha na uso wa ardhi. 

Ghafoor aliyeyasema hayo baada ya kujiri mapigano mafupi kati ya nchi mbili alisisitiza kwamba, jeshi la nchi hiyo likiwa na silaha nzito za aina tofauti limejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuishambulia Kashmir iliyoko katika udhibiti wa India.


Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI


Arsenal wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, lakini si kwa Manchester United ama Liverpool. (90min.com)
Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, ameiomba klabu yake ya Crystal Palace imruhusu ahamie Arsenal. Palace inamthaminisha streka huyo streka huyo kuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Mirror)

Manchester United wanamini kuwa wataweza kukamilisha usajili wa kuwanasa Sean Longstaff, 21, kutoka Newcastle na Bruno Fernandes, 24, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno. (Evening Standard)

Real Madrid watalazimika kulipa kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili kiungo Mfaransa Paul Pogba 26, kutoka Manchester United. (Mirror)
Gareth Bale yawezekana akasilia na Real Madrid baada ya klabu hiyo kushindwa kumpata mnunuzi anayemtaka winga huyo mwenye miaka 29. (Mirror)

Chelsea wanampango wa kumtangaza Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kabla ya wachezaji kurudi mpaumzikoni wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao. plan to announce Derby. (Sun)                Lampard ni moja kati ya wachezaji walioichezea Chelsea                                      kwa mafanikio makaubwa

Liverpool wamefikia makubaliano na Sporting ada ya usajili ipatayo pauni milioni 7 ili kumnunua mshambuliaji kinda Rafael Camacho, 19. (Evening Standard)

Kumefanyika mkutano baina ya viongozi wakuu wa Atletico na Real Madrid juu ya usajili wa usajili wa mshambuliaji Antoine Griezmann, 28, kuelekea dimba la Bernabeu. (L'Equipe - in French)Antoine Griezmann kutimkia Barcelona 

Streka wa Colombia Radamel Falcao, 33, anataka kujiunga na timu inayomilikiwa na David Beckham nchini Marekani Miami pale mkataba wake watakapofiki tamati na klabu ya Monaco. (Sun)

Aston Villa wapo tayari kutuma maombi ya kutaka kumsajili beki wa Southampton Matt Targett. (Express and Star)

Kocha wa West Brom Slaven Bilic anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani klabuni hapo Julian Dicks kujiunga naye kama sehemu ya benchi la ufundi.. (Express and Star)

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

Serikali inawathamini wawekezaji Sekta ya Michezo

Na Shamimu Nyaki -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi pamoja na vituo vya kukuza vipaji katika sekta ya michezo hapa nchini kwakua imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa wachezaji wengi walioliwakilisha Taifa vizuri katika mashindano mbalimbali. 

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jana, Jijini Dodoma alipotembelea kituo cha mafunzo ya Michezo cha Foutain Gate Academy ambapo mbali na kuupongeza uongozi wa kituo hicho na kuahidi kutafuta wafadhili mbalimbali watakaowezesha kituo hicho kufanya vizuri zaidi. 

"Mnafanya kazi kubwa sana ya kuibua na kukuza vipaji, nawaahidi Serikali itaendelea kushirikiana nanyi pale ambapo mtakwama ikiwemo kutuma timu ya Wataalam wa michezo kutoka Wizarani ili waje kutoa ushauri wa kitaalam katika michezo pamoja na kupokea maoni kutoka kwenu ili kwa pamoja tukuze sekta ya michezo"Dkt Mwakyembe. 

Aidha,  Dkt.Mwakyembe ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Michezo kufika katika kituo hicho kuona namna mafunzo yanavyoendeshwa pamoja na kutoa elimu kuhusu taaluma za Michezo zinazotolewa na Chuo cha Michezo cha Malya ili wakufunzi wa kituo hicho waweze kwenda kujifunza zaidi katika chuo hicho. 

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari  hiyo Bw,Dennis Joel amesema kuwa shule hiyo mbali na kutoa elimu,imeweka Michezo kipaumbele ili kupata vijana wengi wasomi lakini pia wanaoweza kucheza michezo mbalimbali ambayo inaweza kuwapatia ajira. 

Kwa upande wake Meneja wa Kituo hicho Bw.Wendo Makau amesema kituo hicho kinalengo la kukuza vipaji na kuwaandaa vijana watakaoshiriki michezo nje ya nchi kwakua vijana wengi wana ndoto ya kufikia hatua ya kucheza nje ya nchi. 

Naye Nahodha wa timu ya mpira wa miguu chini ya umri wa miaka 20 Ramadhan Albert amesema anashukuru nafasi aliyoapata ya kujiunga na kituo hicho kwakua ndoto zake ni kuwa mwanamichezo mkubwa ndani na nje ya nchi.


Share:

Tundu Lissu Kwenda Mahakamani Kupinga Kuvuliwa Ubunge

Baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amepoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge, mwanasiasa huyo ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya risasi ughaibuni amesema atakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.

Lissu alisema hayo jana Ijumaa Juni 28, 2019 wakati akizungumza na gazeti la Mwananchi  kwa njia ya simu akiwa Ubelgiji, ambapo amesisitiza kuwa, tangu aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa Area D jijini Dodoma Septemba 7, 2019 amekuwa akipata matibabu nje ya nchi.

Amesema kwa hatua ya sasa, “Nitawasiliana na wanasheria wangu haraka iwezekanavyo ili kuona cha kufanya lakini Septemba 7 (mwaka huu) ambayo nilikwisha kusema nitarudi sitabadili, nitarudi na alichokifanya Ndugai ni kukoleza mjadala.”

Jana Ijumaa, Spika Ndugai aliliambia Bunge hilo kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kipo wazi.

Amesema hatua hiyo inatokana na Lissu kutojaza taarifa za mali na madeni na sababu ya pili kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.

Mara baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7 mwaka 2017 jijini Dodoma, mwanasiasa huyo  alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo akahamishiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambapo alipatiwa matibabu hadi Januari 6, mwaka jana na kisha kuhamishiwa nchini Ubelgiji hadi leo.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 29 June



















Share:

Friday 28 June 2019

BREAKING: Tundu Lissu Avuliwa Ubunge......Spika Ndugai Ataja Sababu

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameliambia Bunge hilo leo Ijumaa Juni 28, 2019 kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lisu kipo wazi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge ambapo ametaja mambo mawili yaliyomponza Mnadhimu Mkuu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni kutojaza taarifa za mali na madeni na sababu ya pili kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.

Ndugai amesema hajamfukuza Lissu bali Katiba ndiyo imemuondoa mbunge huyo ambaye kikao chake cha mwisho cha Bunge kilikuwa Septemba 7, 2017 ambapo mchana wa siku hiyo alipigwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma.

Mara baada ya kushambuliwa, alipekewa Hospitali ya Rufaa Dodoma kisha usiku huo huo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako alikaa hadi Januari 6 mwaka 2018 alikohamishiwa nchini Ubelgiji aliko mpaka sasa.


Share:

Waziri Mkuu: Mpango Wa Blueprint Kuanza Julai Mosi Mwaka Huu

WAZIRI MKU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint) kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 28) wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma. Amesema wakati kazi hiyo inaendelea Serikali itafanya ufutialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kutathmini kama lengo limefikiwa.

”Utekelezaji wa mpango huo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara nchini, unaojidhihirisha kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imefuta tozo kwamishi 54 zilizobainishwa kwenye mpango huo.”

Waziri Mkuu ametaja tozo zilizoondolewa au kupunguzwa ni pamoja na zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maji

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unaleta tija, ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na Ofisi ya Waziri Mkuu kusambaza blueprint pamoja na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa wizara zote kwa ajili ya kusimamia utekelezaji katika maeneo yao.

Amesema kupitia mpango wa bajeti ya 2019/2020, Serikali itaendelea kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara kwa kutoa unafuu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli nyingine jumuishi.

Wakati huohuo,Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na kilimo tegemezi cha mvua hususani kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuwatoa wananchi katika kilimo hicho.

Amesema hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni pamoja na kuunda upya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inalenga kuiwezesha tume hiyo kusimamia ipasavyo shughuli za umwagiliaji. Pia Serikali imehamishia tume hiyo Wizara ya Kilimo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendeleza kilimo nchini.

”Ili tuweze kufikia lengo la kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 475,056 za sasa hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, tayari nimeielekeza Wizara ya Kilimo isimamia kwa karibu na kutekeleza majukumu yake kwa weledi.”

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa ihakikishe inasimamia vema miradi 22 ya umwagiliaji inayoendelea sasa pamoja na miradi mipya minane itakayojengwa nchini katika pindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Kampuni Ya China Yawekeza $1 Bilioni Sekta Ya Kilimo Tanzania

Kampuni ya Super Agri Technology ya China imesaini makubaliano na kampuni ya Tanzania Agriculture Export Process Zone kuwekeza $1 bilioni katika sekta ya kilimo na usindikaji kwa kipindi cha miaka mitano.

Makubaliano hayo yamesainiwa katika mkutano wa China-Africa Economic& Trade Expo yanayofanyika mji wa Changsha.

Katika hafla hiyo kampuni ya Tanzania Agriculture Export Process Zone iliwakilishwa na Afisa wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Lilian Ndosi.


Share:

TCRA Yaratibu Zoezi La Usajili Walaini Za Simu Kwa Mfumo Wa Alama Za Vidole

Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole ikishirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Jeshi la Polisi Kitengo cha makosa ya mtandaoni,Uhamiaji pamoja na watoa huduma za mawasiliano, stendi kuu ya mabasi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mabel Masasi ni Afisa mwandamizi wa habari na mahusiano kutoka TCRA ambapo amesema kuwa Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu  juu ya matumizisahihi ya vifaa vya mawasiliano,ambapo NIDA wanawasaidia wananchi kupata vitambulisho vya Taifa ambapo mzunguko huo umekuwa ukifanyika nchi nzima ambapo Kilimanjaro ni mkoawa 10.

Amesema kuwa wataendelea kuzunguka mikoa yote lengo kuu likiwa ni kufanya uhamasishaji wa kusajili kwa namba za vitambulisho vya Taifa na kwa alama za vidole na  ili kurahisisha huduma kwa wananchi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo.

Masasi amesema kuwa zipo changamoto malimbali walizokutana nazo na wamejaribu kuyatatua kadiri wanavyozidi kwenda mikoani,amesema kubwa zaidi ni vile amabavyo wananchi wengi wamekuwa wakilalamika hawazijui namba zao za vitambulksho ambapo tumewasihi NIDA waweze kutatua changamoto hiyo kwa wananchi.

Calistus Mhode ni Mkaguzi maidizi kutoka Jeshi la Polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni amesema amesema zoezi hilo linaendelea nchi nzima la mnada kwa mnada ambapo wanashirikiana na Taasisi nyingine za serikali katika kuielimisha jamii na kuwafikia wananchi juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,na matumizi ya teknolojia kwa ujumla .

"Tunawataka wananchi wote wanaokuwa na changamoto zakipolisi sisi tupo  tayari kuwaelimisha na kutafuta suluhu za changamoto mbalimbali amabazo zimewakumba "alisema Calistus.

Abubakari Kakinga Afisa wa NIDA mkoa wa kilimanjaro amesema kuwa wataendelea kutoa hudumakwa wananchi na kama vitambulisho vitakuwa vimechelewa wananchi wanawezakutumia namba za vitambulisho vyao kupata huduma malimbali kama usaajili wa simu zao.

Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kujisajili ya kupata kitambulisho cha Taifa wasisubirie hadi pale zoezi litakapofungwa.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili au tatizo  sugu la Vidonda ya Tumbo, Busha .


 Simu: 0714006521


Share:

Jaguar Anyimwa Tena Dhamama

Mbunge wa Jimbo la Starehe Kenya Jaguar ataendelea kusalia rumande kwa siku 5 zaidi baada ya Mahakama kuagiza Mbunge huyo aendelee kushikiliwa katika kituo cha Polisi mpaka Jumatano ya wiki ijayo kuruhusu uchunguzi zaidi juu ya kesi yake.

Jaguar aliyekuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,  Sinkyani Tobiko, anakabiliwa na  mashtaka ya kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni nchini humo jijini Nairobi katika Barabara ya Kirinyaga alipowataka wafanyabiashara hao kuondoka nchini humo la sivyo watashambuliwa.


Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kutapeli Milioni 2 kwa kutumia sare za JWTZ

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watuhumiwa 6 kwa makosa tofauti ikiwemo kupatikana kwa sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ) na kutumia sare hizo kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu pamoja na unyang’anyi kwa kutumia silaha aina ya Shotgun Magnum Eagle 1 yenye namba 12/76 TS 870.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo SACP Wilbroard Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa matukio hayo ambayo yametokea siku na maeneo tofauti.

==>>Tazama hapo chini


Share:

Kisukari (Diabetes Mellitus) : Chanzo, Dalili na Matibabu Yake

Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania ni ugonjwa wa kisukari. 


Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.
 
Aina za Kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo
 
Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana

Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili wa mtu mwenyewe au autoimmune diseases; au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana yaani idiopathic causes.

Kwa vile, uharibifu katika tezi kongosho hupelekea ukosefu wa insulin au hufanya insulin kuzalishwa kwa kiwango kidogo sana, wagonjwa wa aina hii ya kisukari uhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano kila siku za maisha yao ili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia Kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)
 
Aina ya pili ya Kisukari au type 2 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.

Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).

Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake, wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)
 
Kisukari cha Ujauzito (Gestational DM)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito.

 Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua. 

Hata hivyo karibu asilimia 20 mpaka 50 ya mama wajawazito wanaopata aina hii ya kisukari huweza kuendelea nacho hatimaye kuwa aina ya pili ya kisukari au type 2 DM maishani.
 
Kisukari husababishwa na nini?
Visababishi vya kisukari hutofautiana kulingana na aina husika ya kisukari.
  1. Visababishi vya aina ya kwanza ya kisukari: Aina ya kwanza ya kisukari ina uhusiano mkubwa sana na kurithi. Aidha aina hii pia husababishwa na maambukizi ya Coxsackie virus type B4. Visababishi vingine ni pamoja na sumu inayotokana na kemikali za baadhi ya vyakula (food borne chemical toxins), na kwa baadhi ya watoto wachanga maziwa ya ng’ombe yanaweza kuchochea kinga ya mwili wa mtoto kuushambulia mwili wenyewe (autoimmune reaction) na hivyo kupelekea uharibifu katika tezi kongosho.
  2. Visababishi vya aina ya pili ya kisukari: Kwa ujumla aina hii ya kisukari husababishwa zaidi na mfumo wa maisha na matatizo ya kijeneteki. Aidha vitu kama kuongezeka uzito na unene kupita kiasi (obesity) nayo pia huchangia kutokea kwa aina hii ya kisukari. Sababu nyingine ni pamoja na Kuongezeka umri, maisha ya kivivu na kutofanya mazoezi (physical inactivity) na pia ugonjwa wa tezi kongosho (pancreatitis) ambao hufanya insulin inayozalishwa kuwa na ufanisi mbovu au ya kiwango cha chini.
Dalili za Kisukari
  1. Kukojoa mara kwa mara (polyuria)
  2. Mgonjwa kujihisi kiu kikali na kunywa maji kupitiliza (polydipsia)
  3. Mgonjwa kujihisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia)
  4. Kuchoka haraka (easy fatiguability)
  5. Kupungua uzito
  6. Vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes
  7. Wagonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri.
Aidha kuna dalili maalum ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huu.  Madhara (complications) haya hujulikana kama Diabetic Ketoacidosis na Hyperosmolar non-ketotic coma. Diabetic Ketoacidosis au kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya kwanza ya kisukari (type 1 DM), nayo huwa na dalili zifuatazo
  1. Mgonjwa hutoa harufu ya acetone (inafanana kiasi na harufu ya pombe)
  2. Mgonjwa hupumua kwa haraka na kwa nguvu, hali hii huitwa Kussmaul's breathing
  3. Kujihisi kichefuchefu
  4.  Kutapika
  5.  Kujihisi maumivu ya tumbo na
  6.  Kupoteza fahamu.
Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili (type 2 DM). Hali hii mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwili (dehydration) na mgonjwa huweza kupoteza fahamu.
 
Vipimo na Uchunguzi

Baada ya vipimo, tunaweza kusema kuwa mtu fulani ana kisukari iwapo
  1. Kiwango cha sukari kwenye damu kipo ≥7mmol/L (sawa na 126mg/L) iwapo kipimo kitafanyika kwa mtu ambaye hajala chakula chochote. Kwa jina jingine kipimo hiki huitwa Fasting Blood Glucose (FBG)
  2.  Kiwango cha sukari kwenye damu kipo ≥ 11.1mmol/L (sawa na 200mg/L) kwa mtu ambaye amelishwa gram 75 za glucose ndani ya masaa mawili. Kipimo hiki pia huitwa Oral Glucose Tolerance Test (OGTT).
  3. Au, iwapo mgonjwa atafanyiwa kipimo kinachoitwa glycoslytated hemoglobin (Hb A1C).
Madhara ya Kisukari
Kisukari huweza kusababisha madhara yafuatayo kwa muhusika iwapo hakitatibiwa inavyopaswa.
  1.  Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu kutokana na kuzungukwa na mafuta (Atherosclerosis)
  2.  Mgonjwa kushindwa kuona vizuri au kushindwa kuona kabisa na kuwa kipofu (diabetic retinopathy)
  3.  Kushindwa kufanya kazi vizuri kwa figo
  4.  Mgonjwa kuhisi ganzi na kupoteza kuhisi mikononi na miguu kwa sababu ya kuharibika kwa neva (diabetic neuropathy)
  5.   Kupungua kwa nguvu za kiume.
  6.  Vidonda (diabetic ulcers) hususani vidoleni. Hali hii wakati mwingine hupelekea mgonjwa kukatwa viungo vyake.
  7.  Mgonjwa kuwa hatarini kupata maambukizi ya vimelea mbalimbali hasa bakteria kutokana na kuharibiwa na kushindwa kufanyakazi vizuri kwa chembe nyeupe za damu (White Blood Cells)
Matibabu
Matibabu ya kisukari hutegemea na aina ya kisukari ingawa kwa ujumla kuna hujumuisha matumizi ya dawa na njia ya kubadilisha mfumo (staili) wa maisha.

Kwa aina ya pili ya kisukari (type 2 DM au NIDDM): Aina hii ya kisukari huweza kutibiwa kwa ama dawa au kubadili mfumo wa maisha au vyote viwili kwa pamoja. Katika kubadili mfumo wa maisha, ni muhimu mgonjwa kutilia maanani na kuwa makini na vitu kama aina ya vyakula anavyokula, na kujitahidi na kuongeza kufanya mazoezi ya mwili ili kuepuka kuongezeka uzito kupita kiasi. Kuhusu aina ya vyakula inashauriwa sana
  1. kupunguza kula vyakula vyenye lijamu (cholesterol) ambayo ni mafuta mabaya yaani kula walau chini ya miligramu 300 za lijamu kwa siku.
  2.  kujitahidi sana kula vyakula vya kujenga mwili (protein) angalau kwa asilimia 10-15. Vyakula hivi ni pamoja na nyama na mboga za majani.
  3. kuwa makini na ulaji wa vyakula vya wanga (carbohydrate). Hakikisha visizidi asilimia 50-60 ya chakula unachokula kwa siku. Yaani visiwe ndiyo chakula kikuu kwa siku.
  4.  kupunguza utumiaji wa chumvi katika chakula.
  5.  Kuacha na kuwa muangalifu kutumia pombe.
Suala la ufanyaji mazoezi ni jambo la muhimu kwa vile mazoezi husaidia sana kupunguza uzito, kuondoa mafuta mwilini yanayopunguza utendaji kazi wa insulin na hivyo kuongeza ufanisi na utendaji wa insulin mwilini.

Hali kadhalika, mgonjwa mwenye aina hii ya kisukari anaweza pia kupewa dawa ambazo atatakiwa kunywa kila siku huku akiendelea kufuata ushauri mwingine kama ilivyoelezwa hapo juu.

Dawa hizo ambazo huitwa pia dawa za kushusha kiwango cha sukari mwilini (Oral Hypoglycemic drugs) ni pamoja na zile za kundi la Biguanides kama vile Metformin, za kundi la Sulphonylureas kwa mfano Glipizide, za kundi la Meglitinides, za kundi la Alpha glucosidase inhibitor, zinazojulikana kama Thiazolidinediones, Incretin-mimetic au za kundi la Dipeptidyl peptidase IV inhibitors kwa mfano sitagliptin

Ifahamike pia kuwa wapo baadhi ya wagonjwa wa aina hii ya pili ya kisukari (Type 2 DM) ambao pamoja na kutumia dawa za kunywa za kushusha sukari na kufuata ushauri wa daktari kuhusu mfumo wao wa maisha bado njia hizo zinaweza zisishushe sukari inavyotakiwa. Katika hali kama hiyo, wagonjwa hawa huweza kudungwa pia sindano za insulin kwa muda ili kushusha kiwango cha sukari.
 
Kwa Aina ya Kwanza ya kisukari (Type 1 DM au IDDM)
Pamoja na kurekebisha aina ya vyakula na mazoezi, wagonjwa hawa huitaji kichocheo cha Insulin ili kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.

Dawa za Insulin zimegawanyika katika makundi makuu matatu. Kuna zile zinazofanya kazi kwa muda mfupi (short acting), za muda wa kati (intermediate acting) na zinazofanya kazi kwa muda mrefu (long acting).Kulingana na utendaji wa dawa hizo, mgonjwa anaweza kuelekezwa jinsi ya kujidunga mwenye sindano za insulin nyumbani kwa kufuata maelekezo yafuatayo
  1.  Asubuhi: Mgonjwa hujidunga 2/3 ya insulin nusu saa kabla ya kunywa chai.
  2. Usiku: Mgonjwa hujidunga 1/3 ya insulin nusu saa kabla ya chakula cha usiku.
  3.   Aidha katika hii 2/3 inayotolewa asubuhi, 2/3 yake huwa insulin inayofanya kazi kwa muda wa kati (intermediate acting) na 1/3 ni ile inayofanya kazi haraka (short acting).
  4. Inasisitizwa sana kutojidunga sindano hii bila kupata maelekezo sahihi kwa daktari. Kwa maelekezo zaidi na sahihi ya matibabu kwa kutumia Insulin ni vizuri kuhudhuria kliniki za kisukari, ambazo hupatikana karibu hospitali nyingi hapa nchini.
Matibabu maalum
Matibabu ya hyperosmolar non-ketotic coma (HONKC): Matibabu haya hutolewa hospitali. Mkazo huwekwa katika kusahihisha upungufu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa kati ya lita 8 hadi 10 za maji aina ya Normal saline. Aidha, lita kati ya 1 hadi 2 hutolewa katika masaa ya mwanzo tangu mgonjwa kufkia hospitali. Iwapo kuna ugumu katika kusahihisha kiwango cha kisukari mwilini kwa kutumia dawa za kunywa, Insulin inaweza kutolewa.
 
Matibabu ya Diabetic ketoacidosis (DKA): Kama ilivyo kwa hyperosmolar non-ketotic coma, matibabu ya DKA nayo hutolewa hospitali chini ya uangalizi maalum wa madaktari. Hii ni hali ya hatari, ambapo kama isipotibiwa kwa umakini, inaweza kupelkea kifo cha mgonjwa. Jambo la muhimu katika matibau ni kusahihisha upungufu wa maji mwilini kwa kutumia Normal saline, ambapo lita 1-3 hutolewa ndani ya masaa mawili ya mwanzo, kusahihisha kiwango cha potassium kilichopo katika damu na kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu kwa kutumia Insulin.

Credit: Dr Mayala, TanzMed



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger