Wednesday 1 May 2019

Picha : DIWANI ZUHURA WAZIRI AENDESHA BONANZA LA MICHEZO IBADAKULI



Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri anayetoka tarafa ya Ibadakuli ameendesha Bonanza la michezo kwenye Kata ya Ibadakuli mjini Shinyanga ili kuibua vipaji vya vijana kimchezo, pamoja kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Mei Mosi 2019 kwenye viwanja vya michezo vya Bugweto, kwa kucheza mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti pamoja na mbio za baiskeli, ambapo washindi walipewa zawadi zao.

Akizungumza kwenye Bonanza hilo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri, amesema lengo na madhumuni ni kuinua vipaji vya vijana, kuimarisha umoja, kudumisha amani, pamoja kumuunga mkono Rais John Magufuli ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kusaidia kuinua michezo hapa nchini.

“Bonanza hili limeshirikisha timu nne za mpira wa miguu kutoka Uzogole, Mwagala, Ibadakuli, pamoja na Bugweto , wananchi wameshiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwamo kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti na mbio za baiskeli, ili kuwauganisha kuwa kitu kimoja na kuinua vipaji vya vijana,”amesema Waziri.

“Mbali na bonanza hili pia natarajia kuunda timu ya kata ya Ibadakuli ambayo itakuwa ikishiriki kucheza ngazi ya wilaya, ili kuendelea kuinua vipaji vya vijana kwenye kata hii, ambapo watakuja kuchezea kwenye Timu kubwa na hatimaye kupunguza tatizo la ajira, ikiwamo timu ya hapa nyumbani Stand United,” ameongeza.

Naye Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, amempongeza diwani huyo wa viti maalumu kwa kuanzisha bonanza hilo, ikiwa michezo kwa sasa inatoa ajira nyingi kwa vijana na kutoa wito kwa wanamichezo hao wajitume kwenye michezo hiyo, ili baadae wakacheze kwenye timu kubwa.

Pia amewatahadharisha vijana kuwa makini kuelekea  kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, wasikubali kurubuniwa na baadhi ya vyama na kuvuruga amani ya nchi, bali wawe makini pamoja na kuchagua viongozi ambao watawaongoza vyema na kuwaletea maendeleo kama inavyofanya Serikali ya CCM Chini ya Rais John Magufuli.

Kwa upande wao vijana walioshiriki michezo hiyo akiwamo Makoja Seni , wamemshukuru diwani huyo kwa kufanya Bonanza hilo la michezo ambalo limewapa moyo wa kufanya mazoezi ili kuendeleza vipaji vyao, ambavyo hapo  baadae vitakuja kuwapatia ajira na kuinuka kiuchumi.

Aidha katika Bonanza hilo,Makoja Seni aliibuka mshindi wa mbio za baiskeli, kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake Halima Husein, huku wazee akiibuka Loyce Jiledya, Draft Samweli Kashinje, kuvuta kamba ukipata ushindi mtaa wa Mwagala kwa wanaume, wanawake mtaa wa Bugweto “A”.

Upande wa mpira wa miguu timu ya Bugweto ndiyo wameibuka washindi ambapo wamepewa seti moja ya jezi pamoja na Mpira, wakifautiwa na Timu ya pili ambayo ni Ibadakuli ambao walipata seti moja ya jezi, huku mshindi watatu akiwa ni Mwagala akifuatiwa na Uzogole ambapo wote walipewa mpira mmoja mmoja.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akizungumza kwenye Bonanza la Michezo Kata ya Ibadakuli lililofanyika kwenye eneo la Bugweto na kuelezea madhumuni kuwa ni kuinua vipaji wa vijana pamoja na kutekelezea ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abuu Hafeez Mukadamu akiwaasa vijana kujituma kwenye michezo yao ili ipate kuwasaidia kupata ajira na kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM) Dotto Joshua, akiwataka vijana kupenda michezo ambayo pia itawasaidia kupata afya njema, kupendana pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Diwani wa Kata ya Ibadakuli Msabila Malale akizungumza kwenye Bonanza hilo na kuwataka vijana kudumisha nidhamu kwenye michezo yao na kumpongeza diwani huyo wa viti maalumu Zuhura Waziri kwa kufanya Bonanza hilo ambalo ni muhimu kwa vijana.

Vijana wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali kwenye Bonanza hilo la Michezo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, akifungua Bonanza hilo la Michezo kwenye viwanja vya michezo Bugweto.

Bonanza likianza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.

Mbio za Baiskeli zikiendelea.

Wananchi wakishuhudia mashindano ya mbio za Baiskeli.

Mshindi wa mbio za Baiskeli Makoja Seni akiibuka na ushindi mara baada ya kuwashinda wenzake kwa kuzunguka  Round 60.

Mashindano ya kufukuza kuku yakiendelea.

Halima Husein akiibuka mshindi wa kufukuza Kuku na kisha kuondoka na kitoweo hicho.

Mzee Loyce Jiledya akiibuka mshindi wa kufukuza kuku mara baada ya kuwazidi wazee wenzake na kisha kuondoka na kuku huyo.

Mashindano ya uvutaji wa kamba ukiendelea ambapo washindi waliibuka vijana kutoka Mtaa wa Mwagala.

Mashindano ya kucheza Draft yakiendelea ambapo mshidi aliibuka Samweli Kashinje.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu.

Penat zikipigwa mara baada ya Timu ya vijana ya ufunguzi wa Bonanza hilo, kutoka Bugweto A na B kumaliza dakika 90 bila ya kufungana, ambapo mwenye Jezi ya Njano ni mchezaji kutoka Bugweto B, akipiga Penati na kupata Goli na hatimaye kupata ushindi.

Mchezo kati ya Bugweto FC wenye Jezi Nyekundu ambao ndiyo mabigwa wa Bonanza hilo , wakicheza mchezo wa kirafiki na Bugweto Veterani wenye Jezi ya Njano, ambapo Bugweto FC waliibuka na ushindi wa Goli Moja.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Aboo Hafez Mukadamu, katikati, akiwa na Diwani wa Kata ya Ibadakuli mkono wa kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua, wakiangalia mashindano mbalimbali kwenye Bonanza hilo.

Kabumbu likiendelea kusakatwa kwenye Bonanza hilo.

Mmoja wa wananchi akiwa amepanda juu ya mti kushuhudia michezo mbalimbali kwenye Bonanza hilo la michezo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa mbio za Baiskeli kwa mwenyekiti wao Kande Maganga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa mshindi wa Draft Samweli Kashinje.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Tatu na Wanne wa mpira wa miguu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Pili wa mpira wa miguu Timu ya Ibadakuli kwa kupewa Seti moja ya Jezi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka Timu ya Bugweto ambapo walipewa Seti moja ya jezi pamoja na Mpira.

Mfugaji Bora kwenye michezo ya mpira wa miguu kwenye Bonanza hilo Raymond Peter akipewa zawadi.

Washindi kutoka timu ya Bugweto wakipiga picha ya pamoja.
Mara baada ya kumaliza Bonanza hilo la michezo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafez Mukadamu akimkabidhi kadi ya uanachama ya CCM Daudi Msabila ambaye amehamia kwenye chama hicho kutoka upinzani.

Burudani zikiendelea kutawala mara baada ya Bonanza hilo la michezo likimalizika ambapo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri ambaye ndiye muandaaji, akicheza wimbo na wananchi uitwao Iokote wa msanii Maua Sama

Wimbo wa msanii Maua Sama Iokote ukiendelea kutawala kwenye kufunga Bonanza hilo la michezo.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Kesi Ya Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu Yakwama

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake watano jana walishindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza shauri linalowakabili ikielezwa kuwa basi la Magereza limeharibika.
 
Maimu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 100, likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni katika kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2019.

Wakili  kutoka Takukuru, Leonard Swai  jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally alieleza kuwa, wamepewa taarifa na askari magereza kuwa basi linalowabeba washtakiwa hao kutoka gereza la Segerea kuelekea mahakamani hapo ni bovu.

Kutokana na hali hiyo Swai aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

Hakimu Ally baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 14 itakapotajwa tena.

Mbali na Maimu Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni meneja biashara wa Nida, Aveln Momburi, mkurugenzi wa kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, ofisa usafirishaji, George Ntalima, mkurugenzi wa sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Kati ya mashtaka  yanayowakabili, 24 ni ya kutakatisha fedha,  23 ya kughushi,  43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la  kumdanganya mwajiri na matano ya  kuisababishia hasara mamlaka hiyo.

Mengine ni mawili ya kula njama ya kulaghai, mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.


Share:

Rais Magufuli awataka wafanyakazi kuwa wavumilivu kuhusu nyongeza ya mishahara

Rais Magufuli amesema kuwa hatoongeza mshahara mwaka huu, kwani ahadi yake ya kupandisha mishahara katika uongozi wake haijaisha kwa sababu bado hajamaliza muda wake madarakani.
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo May 1, 2019 mara baada ya hapo awali TUCTA kumuomba atimize  ahadi yake ya kuwaongeza wafanyakazi mishahara.

"Niwaambie ndugu zangu, Katibu mkuu TUCTA alinikumbusha kuhusu ahadi yangu, ninaikumbuka na ninasema muda wangu bado nipo madarakani, ninachoomba muwe na subira.

“Ni kweli kwenye sherehe kama hizi mwaka jana niliahidi kuwa nitaongeza mishahara ya wafanyakazi kabla sijaondoka madarakani, ndugu zangu tuvumilie tu sikutaka kuwadanganya hapa kuwa nimewaongezea mishahara halafu fedha mtakazozipata hazipo, nyinyi endeleeni kuvumilia tupo katika muelekeo mzuri wa suala hili”, Amesema Rais Magufuli na kuongeza;


“Ningeweza kuwaongezea elfu 5 au 10, kesho tu bidhaa zingeanza kupanda hivyo lazima kwanza tujenge uchumi imara. Mimi mwenyewe nilikuwa mwalimu na nikaenda kuoa mwalimu anayejua shida zetu Serikali inawapenda wafanyakazi.




Share:

Kujichua Kwa Muda Mrefu Husababisha Maumbile ya Kiume Kusinyaa na Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Wanaume  wengi  waliofanya  mchezo wa  kujichua  kwa  muda  mrefu hupatwa  na  madhara  ya kuwa  na  kusinyaa  na  kudumaa  kwa  maumbile  yao  ya  kiume  ambayo  huenda  pamoja  na  tatizo  a  Ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Tendo  la  kujichua  kwa  mwanaume  linapofanyika  kwa  kipindi  kirefu huathiri na  kuharibu mishipa  na  misuli  ya uume  na  hivyo  kusababisha  kujengeka  kwa mafuta na tishu zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri.  Jambo  hili  husababisha  makuu mawili; 1. Huzuia  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  kuongezeka jambo  linalotajwa  na  wanasayansi  kama jambo  muhimu  sana  katika  kukua  kwa  uume. 2. Huzuika  kutirika  kwa  damu  kuingia  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili  huathiri  sana  ukuaji  wa  maumbile ya kiume  kwa  sababu  yanapo tokea huathiri uzalishaji  wa  homoni  muhimu  zinazo  husika  na  ukuaji  wa  misuli  ya  uume na matokeo  yake husababisha  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa,kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama uume  wa  mtoto.
 
Hii ndio  sababu  kwanini watu  wengi  walio athirika  na  punyeto  hulalamika  kwamba  maumbile  yao  ya  kiume  hayajaongezeka  tangu  walipo anza  kujihusisha  na  punyeto  wakiwa  na  umri mdogo. 

Maumbile  yao  huonekana  kama  ya  watoto  kwa  sababu hayakupata  nafasi  ya  kupokea  vichochea  vya  kuyafanya  yakue  na  kuongezeka  tangu  walipo  anza  kujihusisha  na  punyeto.

Suluhisho  La  Tatizo La Maumbile  Ya  Kiume  Yaliyo  Sinyaa  Kwa  Sababu  Ya  Punyeto.
Kama  bado  unaendelea  kujihusisha  na punyeto  basi  jitahidi  uache  tabia  hiyo  mara  moja  kwani  inakuharibu. Inaweza  isiwe  rahisi  sana  kuacha  mara  moja  lakini  ukiweka  nia  thabiti  basi  unaweza  kuacha  kabisa  kama  walivyofanikiwa  kuacha  wengine  ambao  walikuwa  wametopea  kwenye  tabia  hiyo  lakini  wakajitahidi  kujilazimisha  na  hatimaye  wakafanikiwa  kuachana  kabisa  na  tabia  hiyo.

==>> Acha kuangalia video chafu za ngono.
Video hizi ndio chanzo kikuu cha punyeto kwa watu wengi hua zinajenga picha nyingi kwenye ubongo na kila picha unayoiona utataka ukaipigie  punyeto hivyo kuacha kuziangalia tu ndio nafuu yako.. 


Weka mipango ya kuzuia kupiga punyeto wakati wa kuoga: bafuni ndio sehemu ambayo inatumika sana na watu wengi kupiga punyeto hivyo ni vizuri kua na mikakati ya kujizuia ukiwa huko kwa kuoga haraka na kuondoka, kuoga maji ya baridi ambayo mara nyingi hayatoi muhemko wa kupiga punyeto.

==>>Epuka kukaa nyumbani peke yako;
Mara nyingi kukaa peke yako kunakufanya ushawishike kufanya tendo hilo, hebu ondoka na ujichanganye na watu wengine au tafuta majirani wa kukaa na kuongelea mambo mengine. 


Fikiria kuhusu madhara yake: kila aliyewahi kupiga punyeto kuna madhara mabayo ameshayapata kama vile misuli ya uume kulegea, kushindwa kurudia tendo uwapo na mwenzi wako, kuishiwa nguvu za kiume, maumbile kusinyaa, kurudi ndani na kuwa kama ya mtoto mdogo.

Acha kusema eti hii punyeto ni ya mwisho: siku zote wapiga punyeto wana akili moja ya kufikiria eti sasa leo napiga afu sirudii tena. Hicho kitu hakipo, kwani kesho yake utasema hivyohivo, kama unaacha acha mara moja ili utunze heshima yako mbele ya mwenzi au mke wako.

Kama utaona  kuna  ugumu  wa  kuacha  tabia  hiyo  na tayari ushaapata madhara ya maumbile kusinyaa na kupungiwa nguvu za kiume, basi  wasiliana nasi kwa ushauri zaidi; Simu  0716-263605


Share:

Video Mpya: Gumbo ft Baba Diamond – Charanga

Wimbo mwingine ambao Baba Diamond Platnumz amesikika nao kwenye Bongo Fleva. Itazame hapa video yake.


Share:

Kikosi cha Taifa Stars cha AFCON chatajwa

Hiki ndicho kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoitwa kwaajili ya mashindano ya AFCON na CHAN.


Share:

Maduro alipongeza jeshi la Venezuela kwa kuzima jaribio la mapinduzi

Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake, harakati ambazo anasema zinaungwa mkono na Marekani.

Maduro amesema Marekani ndiyo iliyochochea na kufadhili kwa hali na mali ghasia zilizoshuhudiwa jana katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini, lakini amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vilifanikiwa kuzima ghasia hizo.

Amesema asilimia 80 ya askari waliotangaza jana kuliasi jeshi na kuyauga mkono maandamano ya wananchi walirubuniwa kufanya hivyo, lakini walipogundua kuwa hizo zilikuwa njama za vinara wa upinzani nchini humo Juan Guaidó na Leopoldo Lopez waliachana na njama hizo.

Vladimir Padrino López, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo sambamba na kupongeza juhudi za Rais Maduro kwa ajili ya kuimarisha usalama na demokrasia, amesema kuwa jeshi lingali linamuunga mkono kikamilifu rais wa nchi hiyo aliyeingia madarakani kwa kura za wananchi.
 
Hii leo waungaji mkono wa serikali ya mrengo wa kushoto ya Caracas wanatazamiwa kufanya maandamano makubwa na kuonyesha uungaji mkono wao kwa serikali ya Maduro, mkabala wa ubeberu na njama za Washington.

Mgogoro unaoshuhudiwa hivi sasa nchini Venezuela ulishtadi mwezi Januari mwaka huu baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani ambaye ni kibaraka wa Marekani na madola ya Magharibi, kujitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela, suala ambalo linakiuka katiba ya nchi hiyo.

Jana Jumanne, Guaido alitangaza kuwa ni siku ya kwanza ya duru ya mwisho ya 'harakati za ukombozi' za kumng'oa madarakani Rais Maduro.


Share:

DRC yafuta uchunguzi dhidi ya Moise Katumbi, huenda akarudi nyumbani

Waendesha Mashitaka wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefuta uchunguzi wa shitaka la jinai dhidi ya Moise Katumbi, mwanasiasa wa upinzani ambaye kwa sasa yuko uhamishoni.

Moise Katumbi alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuajiri askari mamluki wa kigeni wakiwemo askari kadhaa wa Kimarekani waliostaafu kwa lengo la kuangusha utawala uliopita wa Joseph Kabila.

Timothee Mukuntu, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Kijeshi wa DRC alitoa rasmi tangazo hilo jana Jumanne na kufafanua kuwa, "Kwa kuzingatia kuwa rais wa Jamhuri ametoa kipaumbele kwa suala la kupunguza taharuki za kisiasa, tumeona kuwa ni vyema tufutilie mbali uchunguzi huo."

Ingawaje waraka kuhusu tangazo hilo ulitiwa saini tarehe Mosi mwezi Machi, lakini uliwekwa hadharani kwa umma jana Jumanne. Wakili wa Katumbi amesema huu ni wakati mwafaka kwa mteja wake kurejea nyumbani. Hata hivyo Katumbi mwenyewe hajazungumza chochote kuhusu uamuzi huo. 
 
Septemba mwaka jana, Ofisi ya Mashtaka ya Umma nchini humo ilimzuia Moise Katumbi kuwania urais na kutishia kuwa angelikamatwa iwapo angelitia mguu wake nchini DRC, akikabiliwa na tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa. Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo wa urais wa Disemba mwaka jana 2018.

Meya huyo wa zamani wa Katanga mwenye umri wa miaka 54, alikimbilia uhamishoni mwezi Mei mwaka 2016 baada ya kuhitilafiana kisiasa na rais mstaafu Joseph Kabila.


Share:

Biteko akutana na viongozi waandamizi wa wizara na Tume ya madini

Na Issa Mtuwa. Dodoma
Waziri wa madini Doto Biteko amewataka wafanyakazi wa wizara ya madini pamoja na taasisi zake kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kufikia malengo ya wizara hiyo.
 
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na viongozi waandamizi wa wizara ya madini na tume ya madini. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine amezungumzia juu utekelezaji wa maagizo anayoyatoa na usimamizi wa utekeleza wa maagizo yake. Ameongeza kuwa anawategemea sana viongozi hao na wafanyakazi wote katika kufanikisha kazi na malengo ya wizara hiyo.
 
Ametolea mfano wa maagizo aliyowahi kuyatoa ni pamoja na ufutwaji wa leseni zisizo hai ndani ya siku 7 na zingine siku 30 na lile linalo husu mgodi wa North Mara kuhusu utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi ambapo alitoa pia siku 30 kuhakikisha maji hayo yanadhibitiwa. 
 
 Amewaambia viongozi hao kuwa akishatoa maagizo, kazi ya kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo ni kazi yao. Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa Tume Prof. Idris Kikula na tume yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na ziara zake mikoani zimekuwa na tija.
 
Biteko amesisitiza kuwa anatambua mchango wa watumishi wote wa wizara yake hivyo amewaomba kuongeza bidii  na kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakizingatia weledi na uadilifu.
 
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Makamishna. Kwa upande wa tume ya madini waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume Prof. Kikula, Mtendaji mkuu wa tume ya madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Leseni Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Biashara Dkt. Venance Bahati.


Share:

Rais Magufuli Awaonya Wakurugenzi Awanaowatoza Ushuru Wakulima

Rais John Magufuli amesema ni marufuku kwa wakurugenzi na watendaji wa halmashauri kuwatoza ushuru wasafirishaji wa mazao chini ya tani moja na wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya wajasiriamali.

Ametoa onyo hilo  jana Jumanne Aprili 30 katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela katika ziara yake ya siku nane mkoani Mbeya.

Alisema wapo watendaji wa halmashauri wanaoendelea kutoza ushuru kwa wafanyabiashara hao kwa kudhani kuwa wanapoacha wanapunguza mapato.

“Narudia kwa wakurugenzi na watendaji wote wa halmashauri msiwatoze wananchi ushuru wa mzigo wowote usiozidi tani moja. Mkulima wewe safirisha kutoka hapa peleka mahala popote hakuna wa kukutoza ushuru, na hii sheria imepitishwa na Bunge hayupo yeyote wa kuitengua kwa hivyo mkurugenzi ukitengua umevunja sheria una wajibu wa kufukuzwa kazi.”

“Tuzingatie sheria ya kuwalinda wakulima, pakia viazi, maharage, njugu, chochote ilimradi kisizidi tani moja hakuna kulipia, ukizidisha mie simo,” alisema Rais  Magufuli.


Share:

LIVE | JPM kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi kitaifa mkoani Mbeya

LIVE | Rais Magufuli kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi kitaifa mkoani Mbeya


Share:

Waziri Lugola afanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi Stakishari Dar

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi Stakishari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa Kituo hicho.

Waziri Lugola aliwasili kituoni hapo Saa 6:16 mchana ambapo alikutana na wananchi mapokezi ya kituo hicho ambao walifika kwa ajili ya kuwachukulia dhamana ndugu zao walipo katika mahabusu ya kituo hicho, aliwahoji kama wanapata huduma nzuri kutoka kwa askari wa kituo hicho.

Pia Waziri Lugola akiwa katika mapokezi ya kituo hicho, alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa wote waliopo mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji watuhumiwa wote kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya wawepo kituoni hapo.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kuiwahoji mahabusu hao, alisema ziara yake ni ya kawaida ya kufuatilia utendaji kazi wa vituo vya polisi, pia kufuatilia ahadi zake ambazo alizitoa Bungeni kufuatilia vituo mbalimbali vinavyolalamikiwa, na pia yeye Waziri ni wajibu wake kufuatilia utendaji kazi pamoja na maagizo anayoyatoa mara kwa mara ya dhamana zitolewe saa 24 ikiwemo Jumamosi na Jumapili na pamoja na polisi kutowabambikizia kesi wananchi.

“Lengo la hii ziara yangu ni kuboresha utendaji kazi wa vituo vya polisi nchini, sijaja kumuadhibu mtu mimi, hivyo msiwe na wasiwasi, bali kilichonifanya hapa nije nikufuatilia maagizo mbalimbali ambayo niliyatoa kama kweli mnayafanyia kazi,” alisema Lugola.

Lugola aliwataka Makamanda wa polisi mikoa mbalimbali nchini, kusimamia utendaji kazi bora na kuakikisha maagizo yake anayoyatoa yanafanyiwa kazi ipasavyo, na ataendelea kuyafuatilia maagizo yote anayoyatoa na endapo yakipuuzwa hatamvumilia mtu.


Share:

Waziri Mhagama Awaonya Waajiri Wote Kutonyanyasa Wanawake

NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka waajiri wote nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na usawa maeneo ya kazi.

Ameitoa kauli hiyo hii jana tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini ikiwemo; haki na wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.

Waziri alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi yanayoweza kukwamishi jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni viungo muhimu katika kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.

“Mchango wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika nyanja zote za ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize wajibu wao kwa kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na waendelee kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi wengine.”alisisitiza Waziri Mhagama.

Waziri alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema sheria na taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na waajiriwa wenye kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Ninakemea vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo kukoseshwa haki zao na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika kukemea matendo hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.

Aidha Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi kama jukwaa maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.

Aliongezea kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana budi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo katika masuala ya kazi.

“Wanawake umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili kuwa na vigezo mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya kazi.”alisisema Waziri Mhagma.

Naye rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki sawa kwa wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili kuwasaidia wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao ya kazi.

“Wanawake wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao wawapo kazini ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza Nyamhokya.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea kuchangamkia fursa za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake vitakavyosaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la uzalishaji nchini.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 1



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger