Monday 1 April 2019

DKT ANNA MGHWIRA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA UPEPO KILIMANJARO

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea maeneo yaliyoathirika na mvua iliyonyesha juzi ikiambatana na upepo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akizungumza na mmoja wa maafisa wa Magereza waliokuwa katika uismamizi wa wafungwa wakati wa kukata miti mikubwa iliyofunga barabara baada ya kuanguka.
Moja ya miti mikubwa iliyoanguka katika ya barabara ukiwa umekatwa.
Kukatika kwa miti hiyo kulikuwa ni fursa kwa watu wengine waliojitokeza kuokota kuni.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama mafundi wa shirika la umeme Tanesco wakati wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua iliyoambatana na upepo.
Mafundi wa TANESCO wakijaribu kurejesha nyaya zilizokatika .
Sehemu ya nyaya zilizokatika kufuatia mvua hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakitembelea Kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya kuku ambacho kuta zake zilianguka pamoja na mti mkubwa kukatika.
Mti ulikuwa jirani kabisa na jengo lililokuwa na mashine za kuangulia vifaranga na kuharibu mashine mbili pamoja na kuahribu mayai zaidi ya 15,000.
Mafundi wakijaribu kuondoa sehemu ya mti ulioangukia jengo hilo.
Sehemu ya mashine hizo.
Mayai yakiwa kwenye mashine tayari kwa ajili ya kuanguliwa.
Vifaranga vya kuku vikiwa katika mashine baada ya kuanguliwa.
Kuku wakubwa wakiwa katika kiwanda hicho kwa ajili ya mayai.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akitizama moja ya nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Old Moshi ambaye paa la nyumba hiyo liliezuliwa kutokana na upepo.
Nyumba nyingine katika shule ya sekondari ya Old Moshi ikiwa imeezuliwa na upepo.
Moja ya miti iliyoanguka katika shule ya sekondari ya Old Moshi ,mti huu uliangukia bweni la wananfunzi bahati nzuri haukuweza kusababisha madhara. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Annag Mghwira akitoa pole kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Old Moshi alipowatembelea kuwajulia hali baada ya mvua iliyoaambatana na upepo kuharibu baadhi ya miundo mbinu zikwemo nyumba za walimu.
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Old Moshi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira (hayupo pichani).

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
Share:

WADAU WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO KWENYE TASNIA YA HABARI TANZANIA


Picha ya pamoja ya washiriki wa semina hiyo

MISA Tanzania na shirika linalojikita katika kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari ili kupunguza migogoro, kuimarisha demokrasia na kuwezesha uhuru wa kupata taarifa la IMS zimewakutanisha wadau mbali mbali katika semina ya kujadili mazingira yaliyopo na kupendekeza namna ya kuzikabili changamoto zinazodumaza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza nchini.

Semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro iliwakutanisha wawakilishi wa wadau mbalimbali wa tasnia ya habari ikiwemo waandishi wa habari,asasi za kiraia,wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu.

Wakijadili,walitaja baadhi ya changamoto zikiwemo za kiuchumi miongoni mwa wanahabari,sheria zisizo rafiki,wadau kutokuwa na uelewa mzuri wa sheria na kanuni washiriki hao wamesema kuwa kutokuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja ndio imekuwa chanzo kikuu cha matatizo mengine kunawiri na kupendekeza kuwa kabla ya kutafuta suluhu nyingine,mkazo uwekwe katika kuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja miongoni mwa wadau wote wa tasnia ya habari.
Bw.Rashweat kutoka International Media Support (IMS) akielezea umuhimu wa ushirikishwaji kwa kila mdau katika mchakato wa kukuza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bw.Alex Benson (wa kwanza kushoto aliyeketi) akielezea umuhimu wa wanahabari kuwa na uelewa wa kanuni zinazowasimamia ili kuepuka kuzikiuka mara kwa mara.
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kwa niaba ya kundi la majadiliano katika semina hiyo
Dr.Geofrey Chambua mshauri wa maendeleo na sheria akielezea uzoefu wake katika kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kutatua changamoto za kimaendeleo.
Mwandishi wa habari wa kujitegemea kutoka Zanzibar Bw.Ali Othman akichangia mawazo katika semina hiyo
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St.John (SMC) Bw.Michael Gwimile akichangia mada katika semina hiyo
Bi.Joyce Shebe mhariri Clouds Media akiwasilisha mada kwa niaba ya kundi la majadiliano katika semina hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akitoa neno la shukrani na kuhitimisha semina hiyo.
Share:

MSANII NIPSEY HUSSLE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Rapper Nipsey Hussle wa nchini Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi alfajiri ya leo, baada ya kuvamiwa na watu ambao mpaka sasa bado hawajajulikana.

Taarifa kutoka Los Angeles nchini Marekani zinasema kwamba tukio hilo limetokea nje ya duka lake la nguo, ambapo walikuja watu wakiwa kwenye gari na kuanza kummiminia risasi kadhaa zilizochukua uhai wake wakati akikimbizwa hospitali.

Kwenye tukio hilo watu wengine wawili wamejeruhiwa, kutokana na risasi zilizokuwa zikipigwa bila mpangilio.

Nipsey Hussle ambaye jina lake halisi ni Ermias Davidson Asghedom alikuwa na miaka 33, na alikulia Kusini mwa Los Angeles akiwa ni mwanachama wa kundi la vijana wa mtaani (Street gang) la Rollin 60s.

Muda mfupi uliopita rapper huyo aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twiiter uliosema kwamba “kuwa na maadui wenye nguvu ni baraka”, jambo ambalo limehusishwa kuwa huenda alijua nini kinakuja kutokea kwake.

Nipsey ameacha mke na watoto wawili wa kike, huku akiwa na album moja iliyokuwa imetajwa kwenye tuzo za Grammy mwaka huu, kama album bora ya rap.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Keo Jumatatu ya April 1




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger