Tuesday 22 January 2019

WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU WAIANGUKIA SERIKALI

Na. Danson Kaijage-Dodoma. WATOTO wanaolelewa kwenye vituo jijini Dodoma wameiomba serikali kudhibiti taasisi,mashirika na watu binafsi wanaojihusisha na utapeli wa kivuli cha watoto yatima na kujipatia mamilioni ya fedha na misaada mbalimbali ambayo haiwafikii walengwa. Ombi hilo lilitolewa na watoto wanaolelewa katika kituo cha Shirika la Malezi Endelevu (SHIME) jijini Dodoma Raheli Rafael na Moses Tobias kwa niaba ya wezao wakati walipokuwa wakipokea misaada mbalimbali iliyotolewa na wanavyuo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Wakizungumza baada ya kupatiwa misaada hiyo iliyotolewa na wanavyuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) watoto…

Source

Share:

MAKONDA AMTAKA SPIKA NDUGAI AMPELEKE TUNDU LISSU MILEMBE.

Na,Mwandishi wetu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaomba watanzania kumsamehe Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu kwa kauli anazozitoa huko nje ya nchi. Makonda ametoa kauli hiyo leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, katika Mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini. Makonda amesema kwamba amegundua kwamba kauli za Lissu zinatokana na kwamba bado hajapona vizuri kichwani kutokana na yeye mwenyewe kukiri wakati alipokuwa akimaliza mahojiano katika kipindi cha ‘Hard Talk’ kilichofanyika jana na kituo…

Source

Share:

SIMBA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI KUTOKA MAGHARIBI

Mchezaji Lamine Moro kutoka Ghana.

Taarifa ya klabu hiyo leo imeeleza kuwa wachezaji walioletwa ni wa eneo la ulinzi na ushambuliaji ambao wanatoka mataifa ya Ghana na Togo na watasajiliwa endapo kocha Patrick Aussems ataridhishwa na kiwango chao.

''Wachezaji Lamine Moro kutoka Ghana (beki) na Hunlede Kissimbo Ayi-Abel kutoka Togo (mshambuliaji) wamejiunga na timu yetu kwa majaribio'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa imefafanua kuwa iwapo Kocha Mkuu Patrick Aussems ataona wanafaa kuwatumia katika mashindano yanayoikabili timu hiyo watasajiliwa.

Tetesi zinaeleza kuwa endapo nyota hao watafuzu italazimika wachezaji wawili wa kimataifa wawili waachwe huku Pascal Wawa na Juuko Murushid, tetesi zinaeleza kuwa wanaweza kuachwa katika eneo la ulinzi.

Simba tayari ina wachezaji 10 wa kimataifa ambao ndio wanatambulika kwa mujibu wa kanuni za TFF hivyo hawaruhusiwi kuongeza.

Chanzo:Eatv
Share:

WAUZA MADINI WALIVYOIBA BENKI KUU

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Y. Kibesse.

Dkt. Kibesse ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam, katika Mkutano wa wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

Awali kabla ya kujibu swali la Rais Magufuli ambaye aliuliza BOT imejipangaje licha ya kuwa hapo nyuma ilikuwa ikishirikiana na wauzaji wanaoibia serikali.

Dkt. Kibese amesema kwamba Benki Kuu haina tatizo na kununua dhahabu, hapo awali mpaka mwaka 1994 BoT ilikuwa ikinunua dhahabu, "taifa lenye watu wasio waaminifu, haliwezi kuwa Taifa endelevu, kilichotukuta tuliuziwa dhahabu feki tukaamua kusimamisha ununuzi".

Ameongeza kuwa, "Tunafahamu kuwa 'Reserve' za Benki Kuu nyingi duniani zinakuwa na hazina za dola na dhahabu, nasi tunaweza lakini tupo tayari kuanza kununua tena. Tunaelewa Benki Kuu nyingi zinakuwa na hazina ya dhahabu".

Chanzo:Eatv
Share:

MAGUFULI AMTAKA WAZIRI ALIYEKAIDI AGIZO LAKE AJIANDAE KUACHIA OFISI

Rais John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Biteko ajiandae kuachia ofisi yeye pamoja na Naibu Waziri wake endapo atashindwa kufunga kamera katika ukuta wa madini.

Rais amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na Wadau wa sekta ya madini nchini.

"Niliagiza kufungwe Kamera katika ukuta wa Mererani lakini mpaka sasa hazijafungwa, ndio tatizo la Mawaziri wa Tanzania unatoa maagizo hawasikilizi" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameongeza kwamba, "Nakuagiza tena Waziri Biteko, kafunge kamera ndani ya mwezi huu maana usipofanya hivyo ujiandae kuondoka na Naibu wako na makatibu wako, yaani hadi niondoke na nyie nimewamaliza".

Pamoja na hayo Rais ametaka Waziri Biteko kuwa mkali katika Wizara hiyo, "Nakuagiza uwe mkali, aliyekuwa Waziri mwenzako hakuwa mkali ndiyo maana nikaamua aende akapumzike ofisi ya Waziri Mkuu".
Share:

CHRISS BROWN AKAMATWA NA POLISI KWA UBAKAJI


Msanii wa muziki nchini Marekani, Chriss Brown na wenzake wawili wamekamatwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa ya ubakaji.

Tukio hilo limetokea mchana huu Jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwa kwenye uchunguzi wa tuhuma za kudaiwa kumbaka binti wa miaka 24 ambaye alikutana naye katika maeneo ya starehe ya usiku, Januari 15.

Mwanamke huyo alimfungulia mashtaka Chriss Brown akilalamika kumfanyia kitendo hicho cha kikatili, alipomualika chumbani kwake akiwa na mwanamke mwenzake, lakini alipokuwa akitoa maelezo yake alienda mwenyewe chumbani na kukutwa na tukio hilo.

Pia mwanamke huyo aliieleza polisi ya Ufaransa kuwa hata walinzi wa msanii huyo mwenye kipaji cha aina yake walimnyanyasa, na ndipo polisi ikaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

Mpaka sasa Chriss Brown hajatoa kauli yoyote juu ya tuhuma hizo, na bado yuko nchini Ufaransa ambako alikuwa na ziara.
Share:

GWAJIMA AMPA USHAURI MZITO RAIS MAGUFULI

Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.

Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.

Kwenye ushauri huo Askofu Gwajima ambaye alianza kwa kumsifu Rais Magufuli, amesema kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye 'exposure' kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

“ Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali mbali duniani”, amesema Askofu Gwajima.

Sambamba na hilo Mchungaji Gwajima ameendelea kueleza kwamba madini tuliyonayo ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.

"Nilipita Mwadui nikashangaa, wakaniuliza tukuletee almasi kwa utani, ndani ya saa moja watu walileta almasi imejaa bakuli haina watu wa kununua, wametoka nazo ndani ya nyumba zao, hizo kama zingelipiwa ushuru nchi yetu ingekuwa mahali pazuri sana”, amesema Gwajima

Hii leo Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo nchini.
Share:

TANESCO YAALIKA WAWEKEZAJI ZAIDI KWENYE VIWANDA ARUSHA


Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina(kushoto), akimsikiliza Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani, Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua kuhusu namna TANESCO ilivyoweza kufikisha umeme wa kutosha kwenye eneo la Mirarani Januari 21, 2019. 
***

UWEKEZAJI kwenye miundombinu ya umeme uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO umeanza kuzaa matunda eneo la machimbo ya madini Mirerani mkoani Manyara.

Serikali kupitia TANESCO iliwekeza kwa kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha KIA na hivyo kuwezesha hali ya upatikanaji umeme ulio bora na wa uhakika kwenye eneo la Mirerani kuongezeka.

Kwa sasa matumizi ya umeme kwenye eneo lote la Mirerani ni kiasi cha Megawati 3.5 lakini kubwa zaidi miongoni mwa watumiaji wakubwa walioanza kufaidika na uwekezaji huo ni pamoja na kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite) na kile cha Mirerani Tanzanite vyote viko Mirerani.

Meneja wa Shirika la Umeme wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani Mhandisi Zacharia Masatu amewaambia waandishi wa habari wanaotembelea eneo hilo kuwa kiwanda hicho pekee kinatumia kiasi cha Megawati 1.1 ya umeme.

Aidha Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina amesema jiji lina ziada ya umeme Megawati 50, na hivyo amewahimiza wawekezaji katika sekta ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kuwekeza ili kufaidi uwekezaji wa serikali katika miundombinu ya umeme nchini.

“Wito wetu kwa wafanyabiashara na wawekezaji, waje wawekeze kwenye mkoa wetu wa Arusha sababu kama tulivyoeleza awali tuna umeme wa kutosha, kwa mkoa mahitaji ni Megawati 75 na uwezo wa kituo chetu ni Megawati 120 kwahiyo unaweza kuona tuna ziada inayofikia Megawati 50” ,lisema Mhandisi Mhina.

Mhandisi Mhina alibainisha kuwa, viwanda vinaweza kuleta matokeo makubwa ya uwekezaji katika miundombinu ya umeme uliofanywa na serikali kwani matumizi ya kiwanda kimoja inaweza kuwa ni mahitaji ya wilaya nzima.

“Viwanda ni njia mojawapo inayoweza kutupeleka kwenye uchumi wa kati tunaotaka kwa haraka zaidi”, alisisitiza.

TANESCO ilifunga mitambo ya kuingiza umeme wa kutosha kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited na kwamba kinajitegemea ambapo kuna jumla ya transfoma pozo kubwa tatu na gharama za ufungaji wa mitambo hiyo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 60.

Aidha afisa wa kiwanda hicho cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (graphite), Nai Mainga alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa madini hayo ya graphite (kinywe) Juni 2018 na kwamba tangu uzalishaji uanze hadi hivi sasa, tayari wamezalisha kiasi cha tani 5,600 na wateja wakubwa wa madini hayo ni China.

“Matumizi makubwa ya madini hayo ya kinywe hutumika kutengeneza vitu maka betri na tunapozungumzia betri ni pamoja na betri zile kubwa za magario na mitambo, lakini pia kuna taarifa kuwa madini hayo hutumika kutengeneza bati maalum la kuzuia injini ya ndege ili isipate moto sana kwani madini haya huchomwa sana ili kupata zao la mwisho”, alifafanua.

Alisema kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zimeanza mchakato wa kusitisha matumizi ya petrol kuendeshea magari na hivyo kuna uwezekano wa kutumia madini haya ili kutengeneza betri za kuendesha magari.

Share:

MAGUFULI ABADILI ‘GIA ANGANI’ MKUTANO WA MADINI...AWEKA PEMBENI MAWAZIRI


Rais John Magufuli amebadilisha mfumo wa ratiba katika mkutano wa madini, ambapo badala ya mawaziri kuwahutubia wadau kwenye mkutano huo, amewataka wadau kutoa changamoto wanazokutana nazo ili waweze kupata suluhisho la matatizo yao.


Lengo la kufanya hivyo ni kutaka kujua kwa nini Tanzania haifaidiki kwa kuuza madini na haimo katika Benki ya Dunia (WB) kwa kuongoza katika kuuza madini hata katika nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam unashirikisha wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini nchini.

“Tunataka tujue kwa nini madini yanatoroshwa na wanaosindikiza ni askari, tume ya madini inafanya nini katika kuhakikisha biashara hii inafanya vizuri, kwa nini Tanzanite pamoja na kujenga ukuta bado inatoroshwa, kwa nini hatuna maeneo ya soko ya madini,” amesema Rais Magufuli

“Tunataka leo tujue tunakosea wapi na kama ni mapepo wachungaji wako hapa, hivyo ni lazima makatibu wakuu, watendaji na mawaziri watueleze kwa nini,” ameongeza.

Amesema kwa maoni yake ameona hayo ndiyo ya kujadiliwa na kuangalia nani anayeanza badala ya viongozi kuwaeleza yao bila kujua changamoto za kweli.

“Ili tutoke kwenye dimbwi hili la sekta kuchangia asilimia nne tufike huko kwenye asilimia 10 mnayoitaka basi tuonyeshe uzalendo wa kweli katika sekta hii,” amesema Rais Magufuli.

Na Aurea Simtowe, Mwananchi


Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install


https://bit.ly/2Qb7qyF
Share:

RONALDO AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKWEPA KULIPA KODI

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo amewasili mjini Madrid huku akiandamwa na idadi kuwa ya waandishi habari ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kukwepa kulipa kodi ambayo huenda yakasababisha kupigwa faini ya €18.8m (£16.6m) .

Jaji mmoja alikataa ombi la mchezaji huyo kuhudhuria kesi hiyo kupitia kanda ya video ama hata kuingia katika jumba hilo kwa kutumia gari ili kuzuia kuandamwa na vyombo vya habari.

Anatarajiwa kukiri mashtaka hayo katika makubaliano ambayo yatamlazimisha kuhudumia kifungo cha mezi 23 jela.

Nchini Uhispania, wafungwa huwa hawahudumii kifungo cha chini ya miaka miwili.

Hali ya makosa ya Ronaldo inamaanisha kwamba hatohudumia kifungo jela.

Mchezaji huyo wa Juventus ambaye aliichezea klabu hiyo usiku wa kuamkia mashtaka hayo aliwasili akiwa anatabasamu.

Wakili wake alikuwa amehoji kwamba kutokana na umaarufu wake , alipaswa kutotumia lango kuu la mahakama kutokana na hali ya usalama.

Así ha llegado Cristiano Ronaldo a la Audiencia Provincial. De la mano de Georgina, firmando autógrafos y sonriente: “Estoy perfecto”


Ronaldo ambaye ni bingwa mara tano wa taji la Ballon d'Or na kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani, anatuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania kati ya 2011 na 2014 wakati alipokuwa akiichezea klabu ya Real Madrid wakati huo akiwa na makao yake nchini Uhispania.

Kesi hiyo inaangazia mikataba ya haki za picha zake.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa fedha hizo zilipitishwa kupitia kampuni zinazotozwa kodi ya chini katika mataifa ya kigeni ili kukwepa kulipa kodi iliohitajika.

Kitita hicho kilidaiwa kuwa cha €14.8m.

Mwaka 2017, wakati madai hayo yalipochipuka, viongozi wa mashtaka walisema kuwa ulikuwa ukiukaji wa ahadi yake nchini Uhispania.

Lakini wakili wa Ronaldo alisema kuwa kutoelewana kuhusu kile kilichohitajika na kili ambacho hakikuhitajika chini ya sheria za Uhispania na kuzuia jaribio lolote la kukwepa kulipa kodi.
Makubaliano hayo yaliofanyika mwezi Juni mwaka uliopita yaliafikiwa na mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Yatawasilishwa mbele ya jaji siku ya Jumanne mahakamani.

Jaji huyo atatangaza uamuzi wake katika kipindi cha siku zijazo.

Ronaldo sio mchezaji wa kiwango cha juu wa pekee kukabiliana na mkono wa mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Mchezaji mwezake wa zamani Xabi Alonso pia anatarajiwa kuwasili mahakamani siku hiyohiyo kwa mara ya kwanza akishtakiwa na shataka kama lake la makosa ya haki za picha zake ya takriban €2m.

Ronaldo pia anakabiliwa na shtaka jingine: Mchezaji huyo anatuhumiwa kutekeleza ubakaji mjini Las Vegas 2009, mashtaka ambayo anapinga.
Chanzo : Bbc
Share:

DAWATI LA MALALAMIKO YA RUSHWA YA NGONO RASMI SHINYANGA

Waandishi wa habari  wakitekeleza majukumu yao ofisi ya TAKUKURU (m) Shinyanga,Kaimu mkuu wa takukuru mkoa wa shinyanga Francis Luena(kulia).

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Shinyanga imelianzisha dawati maalumu litakalosikiliza na kushughulikia vitendo vya rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa shule na vyuo ambao wametajwa kukabiliwa na kadhia hiyo kwa muda mrefu. 


Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa shinyanga Francis Luena alibainisha hayo jana Jumatatu 22,2019 wakati akitoa taarifa ya utendajikazi wa taasisi hiyo kuanzia mwezi oktoba hadi desemba 2018,kwa waandishi wa habari na kusema kuanzishwa kwa dawati hilo ni miongoni mwa mikakati itayotoa  fursa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa sehemu sahihi ya kukimbilia kutoa taarifa wakati wanapokutana na mkasa huo. 

“tuliwahi kufanya utafiti wa rushwa ya ngono kwenye shule za msingi,kwa kweli ule utafiti ulisikitisha tulibaini baadhi ya walimu wanatumia mbinu ya kumchapa na kumpatia adhabu kali mwanafunzi kumbe lengo lake ni kumtaka mwanafunzi huyo kingono,kwa hiyo dawati hili litatoa mwanya kwa wanafunzi kuleta taarifa hizo na kuweza kufanyiwa kazi,” alisema Luena. 

Baadhi ya wanachuo wa chuo cha Mtakatifu Joseph mkoani Shinyanga wameiambia www.malunde.com kuwepo kwa vitendo vya manyanyaso ya kingono kutoka kwa wakufunzi katika baadhi ya vyuo na kwamba hatua hiyo itasaidia kupunguza vitendo hivyo vinavyowaathiri wanafunzi kisaikolojia. 


Kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 ya mwaka 2007 imeitaka taasisi hiyo kuchunguza,kuelimisha umma na kufanya utafiti , kwenye miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wanaojihusisha na masuala ya rushwa. 

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Share:

Je Kwanini Baadhi Ya Wanaume Wengi Wana Ukosefu Ama Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

JE KWANINI BAADHI YA WANAUME WENGI WANA UKOSEFU AMA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO ???

Pata sululisho la matatizo haya na  magonjwa mengine utapona kwa mda mfupi sana hatakama ulihangaika mpaka ukakata tamaaa 

GALIMBO 3 MIX  ni dawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa aina mbili ili kukidhi mahitaji ya mtumiaji, imetengenezwa kwa muundo wa vidonge pamoja na unga kwaajili ya kuponesha tatizo moja kwa moja , huimalisha misuli ya uume iliyolegea wakato wa tendo la mdoa ,na kukufanya ucherewe kufika kileleni kwa mda wa dk ( 20 - 45 ) itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu nira hamu kuisha wara kuhisi kuchoka vilivile huzalisha viini vya uzazi ( manii ) 

YOLAN  hurefusha na kunenepesha  maumbile madogo ya uume na kuwa na uume kuanzia nchi (6-8) tiba kwa mda mfupi sana

Zipo sananu nyingi sana zinazosababisha matatizo hayo  km vile -:punyeto, kisukali,ngili,chango,vidonda vya tumbo,  tumbo kuunguluma na kujaa gesi maumivu ya mgongo ama kiume ,kolodani moja kuvimba ama kuingia ndani  presha nk 

Matatizo haya yote sio mageni, kigeni ni tiba sahihi ya kuponesha matatizo hayo

SUPER MBUKE -:  nidawa ya kuponesha tatizo la kisukali kwa mda mfupi sana , usihangaike wara kuteseka tumia dawa ya mitishamba kwaajili ya tatizo hili na upone kabisa

NTINJIWA  nidawa ya mvuto wa biashara,kazi, kupandishwa cheo,kumfanya mfanyakazi apendwe na bos wake

Pia ninadawa za kumvuta mme , mke,mchumba,hawara, au mtu yoyote unaemuhitaji katika maisha yako hata km yupo mbali na atatulia na kukutimizia cjovjote utakacho na kumfunga asiwe na mtu mwingime ,

Pata tiba za magonjwa mbalimbali ikiwemo miguu kuwaka moto, mgongo,bawasili ,kaswende ,gono na mengine mengi

KWAUSHAULI NA TIBA WASILIANA NA DR CHIKAGO    0743543944   0620510598

Km huna nafasi ya kufika ofisini hudumahii utaletewa hapo ulipo , kwa wale wa mikoani natuma kwanjia ya basi


Share:

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa


Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.


Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,


Share:

TAIRI LA GARI ,MATUNDA YATUMIKA KUTOROSHA MADINI

Wadau wa sekta ya madini nchini wameeleza kusikitishwa na namna ambavyo biashara ya madini inavyoendelea kuendeshwa kimagendo huku wakaguzi wa madini na Jeshi la Polisi wakiwa hawazijui njia hizo.

Wadau wameeleza njia hizo wakati wakizungumza mbele ya Rais Magufuli ambaye ni mgeni rasmi katika mkutano wa kisekta wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa mikutano wa JNICC Jijini Dar es salaam.

Mdau wa dhahabu aliyejitambulisha kwa jina la Solomon Mihayo wa mkoani Geita amesema kuwa watu wanasafirisha dhahabu kimagendo mipakani na licha ya ukaguzi unaofanyika lakini hawawezi kujulikana.

"Mhe. Rais kuna watu wanaiibia serikali lakini siwezi kutaja ni watu gani, watu wanachana kabichi na kuweka hadi kilo mbili za dhahabu na wanapita nazo tu mipakani, watu wanatumia tairi za gari wanaweka dhahabu hadi kilo 10 na hawatambuliki, wengine wanapasua matikiti maji haya wanaficha dhahabu na kupita nazo mipakani", amesema Solomon.

"Kuna mazingira mengi ambayo Polisi pekee hawawezi kutambua, tutawalumu bure tuu. Wanafanya kazi kubwa sana polisi lakini hawawezi kupambana nao", ameongeza.

Pia bwana Solomon kwa niaba ya wadau wa dhahabu, ametoa mapendekezo kuwa wajumuishwe katika kamati zinazoundwa na Wizara husika ili waweze kusaidia kuwatambua na kuwakamata wezi hao.
Share:

SULUHISHO LA UVAMIZI WA ARDHI NA HIFADHI ZA WANYAMA PORI NCHINI

Tanzania inapanga kutathmini upya mipaka ya hifadhi na mbuga zake za wanyama pori na misitu katika kukabiliana na ongezeko la matumizi ya radhi.

Rais John Magufuli ameagiza kusitishwa kwa mpango wa kuwatimua wakaazi wa vijiji vilivyopo kwenye hifadhi za wanyama pori na misitu.

Wizara husika zimetakiwa kutambua na kubaini hifadhi zote na misitu ambazo hazina wanyama pori zitakazoweza kugawanya kwa wakulima na wafugaji ambao wameweka makaazi katika baadhi ya hifadhi nchini.

Hatua hiyo imenuiwa kukabiliana na kuongezeka kwa matumizi ya ardhi hususan kwa jamii za wafugaji na wakulima waliojikita katika maeneo hayo ya hifadhi za wanyama pori.

Taarifa zilizopo ni kwamba wizara zote husika zinapaswa kutekeleza agizo hilo pasi kuchelewa.

Jamii tofuati kama ya Wamaasai ambao ni wafugaji, pia ni wanaohama hama katika kutafutia mifugo yao malisho ni sehemu ya watu wanaoishia kuishi katika hifadhi za wanyama pori.

Mwandishi, mkaazi mjini Arusha, Jane Edward alisema   Ngorongoro ni mojawapo ya hifadhi Tanzania ambapo binadamu wanaishi katika makaazi ya wanyama kwa muda mrefu.

Ameeleza kwamba hilo ni mojawapo ya kivutio kikubwa kinachoitambulisha hifadhi hiyo.

Chanzo:Bbc
Share:

MANNY PACQUIAO AVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA LOS ANGELES

Nyumbani kwa Manny Pacquiao Los Angeles mjini Los Angeles.

Nyumba yake ambayo ipo Los Angeles Marekani ilivamiwa muda mchache tu baada yakushinda pambano lake dhidi ya Adrien Broner.

Ripoti iliyotolewa na Polisi wa mjini Los Angeles imeeleza kuwa nyumba hiyo ilivamiwa usiku wa Jumapili na wezi ambao hawakuweza kuiba chochote kutokana na wana usalama hao kuwahi eneo la tukio na kudhibiti hali hiyo.

Polisi wameeleza kuwa walitumiwa ujumbe juu ya kuwepo kwa wezi hao na mtu mmoja katika timu ya Pacquiao hivyo wakawahi kwa polisi.

Pacquiao alishinda pambano hilo dhidi ya Adrien kwa pointi na baada ya pambano hilo la (WBA world welterweight) akaweka wazi kuwa anahitaji kurudiana na bondia Floyd Mayweather ambaye alimpiga mwaka 2015.

Chanzo:Eatv
Share:

WAZIRI LUGOLA ATAJWA KUTETEA WATUHUMIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepongezwa kwa hatua yake ya kuwatetea baadhi ya watuhumiwa ambao wamekuwa hawatendewi haki pindi wanapokuwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Wakitangaza uamuzi Jijinji Dar es salaam Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRDC) pia walitangaza kuanzishwa kwa operesheni maalum iliyopewa jina la Tetea haki za Watuhumiwa lengo ni kuwatetea watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumo amesema, "tunampongeza Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kujitokeza kuwatetea baadhi ya watuhumiwa nchini".

"Kwa mujibu wa sheria jeshi la polisi lina wajibu wa kumpa mtuhumiwa haki yake ya kupata msaada wa kisheria kitu ambacho kwa Loliondo imekuwa shida na hii ni kwa maeneo yote ya vijijini siyo Loliondo pekee", ameongeza Onesmo Olengurumo.

Mara kwa mara Kangi Lugola amekuwa akiwachukulia hatua baadhi ya Makamanda wa Polisi ambao wamekuwa hawatoi haki kwa wartuhumiwa wa matukio mbalimbali ya kiuhalifu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger