Wednesday 24 May 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 24 2017

Share:

Tuesday 16 May 2017

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA KIDATO CHA TANO-ZANZIBAR PEMBA

Share:

WANAFUNZI WALIOTEULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017-ZANZIBAR UNGUJA

Share:

BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU ZANZIBAR: ANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO MWAKA WA MASOMO 2017/18

Image result for BODI YA MIKOPO ZANZIBAR

TANGAZO

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inawatangazia wanafunzi wote wanaohitaji kujiendeleza katika fani mbalimbali za Elimu ya Juu kuwa fomu za maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18 zitaanza kutolewa kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 02/05/2017 hadi tarehe 31/07/2017.

Mikopo itatolewa kwa waombaji waliotimiza sifa za kujiunga na masomo ya juu katika ngazi za:
  • Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree),
  • Shahada ya Pili (Master Degree)
  • Shahada ya Tatu (PhD).
Walengwa wa maombi ya mikopo ni:
  • Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
  • Wahitimu wa Diploma wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza.
  • Wahitimu wa Shahada ya Kwanza wenye sifa za kujiunga na masomo ya Shahada ya Pili.
  • Wahitimu wa Shahada ya Pili wenye sifa za kujiunga na Shahada ya Tatu.
Kuanzia mwaka wa masomo 2017/18 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar haitatoa mikopo kwa waombaji ambao ni watumishi wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT). Mkazo umewekwa kwa vijana wapya waliomaliza masomo na ambao hawajapata ajira.

Waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia Fani za Vipaumbele vya Serikali ambazo zinapatikana katika tovuti za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz).

Fomu za maombi zitalipiwa shilingi 10,000 ambazo zitalipwa moja kwa moja na muombaji kwenye akaunti namba 021108001357 ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyopo katika Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Wanaohitaji fomu za maombi wanaombwa kufika katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Chakechake Pemba na wanatakiwa kuchukua:
  • Kitambulisho cha Mzanzibari
  • Fomu ya malipo (Pay Slip) kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
  • Vivuli vya vyeti na matokeo ya masomo kwa ngazi aliyohitimu.

SIFA ZA KUPATA MKOPO

Sifa za waombaji wa mikopo ambao maombi yao yanaweza kuzingatiwa wakati wa uteuzi zimetajwa kwenye kifungu cha 20 zikiwemo:
  • Mwombaji awe Mzanzibari
  • Awe ameomba mkopo kwa kujaza Fomu Namba 1 au kupitia njia nyengine yoyote ile ambayo BMEJZ itaona inafaa. Maombi yawe yamewasilishwa ndani ya muda maalum uliowekwa na BMEJZ unaoanzia Mei 2 hadi Julai 31 ya kila mwaka.
  • Awe amepata udahili kwenye chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka husika nchini.
  • Awe amepata alama nzuri za ufaulu.
  • Mwombaji wa shahada ya kwanza (Bachelor/First Degree) aliyehitimu kidato cha sita anapaswa awe amefaulu angalau masomo mawili (Principal subjects) kwa alama za ufaulu zinazoanzia:
  • alama 4.0 kwa wahitimu wa masomo ya sayansi au ufundi;
  • alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya biashara;
  • alama 5.0 kwa wahitimu wa masomo ya sanaa au sayansi jamii.
  • Mwombaji wa shahada ya kwanza aliyehitimu stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) katika masomo ya sayansi au ufundi anatakiwa awe na ufaulu wa alama (GPA) 3.0 au B; wahitimu wa stashahada za masomo ya biashara, sayansi jamii au Sanaa wapate alama kuanzia 3.5 au B+.
  • Mwombaji wa shahada ya uzamili (Master/Second Degree) katika masomo ya sanaa au sayansi jamii awe amehitimu shahada ya kwanza na kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la juu (upper second class). Waombaji wa shahada ya uzamili katika nasomo ya sayansi, ufundi, tiba, uchumi, mipango na biashara wawe na alama za ufaulu za kuanzia daraja la pili la chini (lower second class). Wahitimu wa stashahada ya uzamili wanapaswa kupata alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la chini (lower second class)
  • Mwombaji wa shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy - PhD) awe amehitimu shahada ya uzamili na kupata alama za kuanzia daraja la pili la juu kwa waombaji wa masomo ya sanaa na sayansi jamii. Waombaji wa shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi, ufundi, udaktari na uchumi, mipango na takwimu wapate alama za ufaulu kuanzia daraja la pili la chini.
  • Waombaji wanaoendelea na masomo vyuoni pia wanaweza kuomba kwa kuzingatia sifa za kitaaluma zilizotajwa hapo juu [d(i) –(iv)]. Aidha mwombaji awe amefaulu mitihani yake ya chuo kwa kiwango kitakachomwezesha kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuatia katika ngazi ya masomo anayoombea mkopo.
  • Awe ameomba fani inayolingana na vipaumbele vya SMZ katika mwaka husika.
  • Asiwe na mkopo au udhamini wa masomo kutoka taasisi nyengine.
  • Mwombaji wa shahada ya kwanza asizidi umri wa miaka 40 kuanzia tarehe ya kutuma maombi na mwombaji wa shahada ya uzamili asizidi miaka 45 kuanzia tarehe ya kutuma maombi. Ukomo wa umri wa mwombaji wa shahada ya uzamivu ni miaka 47 kuanzia tarehe ya kutuma maombi.
  • Mwombaji aliyeajiriwa kwenye utumishi wa umma awasilishe barua ya ruhusa kutoka kwa mwajiri wake.
  • Mwombaji anayedaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar awe ameshaanza kulipa deni lake kwa angalau asilimia 25 ya deni lote bila ya kusita kwa malipo ya deni ya kila mwezi.
  • Mwombaji aliyesoma kwa mkopo kutoka BMEJZ awe ameshafanya kazi kwa angalau miaka miwili baada ya kuhitimu masomo yake ya awali kabla ya kuomba mkopo mwengine kutoka BMEJZ.

Angalizo:

  • Waombaji wanaotumia sifa za masomo ya kidato cha nne kuomba udahili katika vyuo vikuu vya nje ya nchi ili kujiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza, maombi yao ya mkopo hayatozingatiwa.
  • Waombaji wa mikopo waliohitimu masomo ya Diploma pasi na kuwa na elimu ya kidato cha sita au sifa za kujiunga na kidato cha sita, wanatakiwa wawe wamefaulu angalau masomo matano ya Kidato cha Nne kwa kiwango cha alama D na kuhitimu ngazi ya cheti (Certificate) kabla ya kujiunga na masomo ya Diploma.
  • Waajiriwa hawahusiki na utaratibu wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka huu wa masomo

FANI ZA VIPAUMBELE WA KIPINDI CHA 2016 - 2020

Tume ya Mipango ya SMZ imetoa taarifa kuhusu utafiti uliofanywa juu ya hali ya utumishi nchini ambayo imeonesha uwepo wa mahitaji makubwa ya wataalamu. Taarifa hiyo imeibua maeneo ya Vipaumbele vya SMZ juu ya mahitaji ya wataalamu na imeagizwa kuwa taarifa hiyo itumike kama kigezo muhimu kwa utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu nchini ili kufikia utekelezaji wa mipango na maendeleo ya rasilimali watu iliyo bora na itakayowaandaa watu wenye ujuzi sahihi, taaluma, tabia na silka zenye tija zinazoendana na mabadiliko ya mfumo wa ushindani wa soko la ajira na kufikia viwango vya juu vya uzalishaji na utoaji huduma.

Ili kurahisisha utekelezaji wa Vipaumbele vya SMZ katika utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu kuanzia mwaka wa masomo 2016/17 hadi 2019/20, Tume ya Mipango imevigawa vipaumbele hivyo katika madaraja matatu tofauti kulingana na umuhimu wa kila kada kama inavyoonekana katika jedwali la hapo chini.

Hivyo, kwa mwaka huu wa masomo, BMEJZ itazingatia kikamilifu taarifa ya Tume ya Mipango wakati wa upokeaji wa maombi ya mikopo na uteuzi wa waombaji katika mwaka wa masomo 2017/18. 

TAARIFA ZAIDI <<BOFYA HAPA>>
Share:

NACTE:GUIDE BOOK AFYA-CHETI NA DIPLOMA 2017/2018

  • THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION
  • ADMISSION REQUIREMENTS - 2017/2018
Guidebook
ADMISSION REQUIREMENTS
Share:

Sunday 14 May 2017

Treni ya Abiria Yapata Ajali Morogoro

Treni ya abiria imepata ajali usiku saa 5 eneo la Stesheni ya Mazimbu Morogoro ambapo mabehewa manne yameegama na matatu yameacha reli.

Ashura Mrisho aliyekuwa anakwenda Tabora amejeruhiwa kwa kuangukiwa na mizigo. Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala 
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 14 2017

Share:

TCRA yawatahadharisha watumiaji wa kompyuta juu ya shambulio la Kirusi Kiitwacho WANNACRY kwenye kompyuta

Shambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.

Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.

Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
==> Hii ni Tahadhari Iliyotolewa  na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA  kuhusu Kirusi hicho

Advertisement
==
Share:

Wednesday 10 May 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 10/05/2017
Share:

ADMISSION OF STUDENTS FOR VARIOUS CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2017/2018

THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION

(NACTE)
PUBLIC NOTICE

ADMISSION OF STUDENTS FOR VARIOUS CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2017/2018

The National Council for Technical Education (NACTE) is a statutory body established under the National Council for Technical Education Act, Cap. 129, to oversee and coordinate the provision of technical education and training in Tanzania.  Under the establishing Act, in order to attain and maintain the status of a training provider, all institutions are required to be registered, accredited and have their curricula approved by the Council. Institutions are not allowed to admit students and start offering any programme without the approval of the Council.

The Council wishes to inform all technical education stakeholders and the general public that, admission and selection of students for various Certificate and Diploma Programmes offered by Technical Institutions, Universities and their constituent Colleges shall be conducted by Technical Institutions and Universities themselves.

Kindly be informed that, all applications for admissions should be submitted to respective technical Institutions or Universities except for public institutions offering health & allied sciences; and teacher education courses.

Admission into public institutions offering health & allied sciences, and teacher education courses shall be coordinated by the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly & Children; and Ministry of Education, Science & Technology respectively in collaboration with NACTE. In that respect, all applications for admission into Certificate and Diploma programmes for health & allied sciences; and teacher education programmes delivered by public health & allied sciences schools, and public Teacher Training Colleges should be made online via NACTE website (www.nacte.go.tz) or through the respective schools and colleges that will submit received applications for admission through their respective Institutional Panel.

The Council wishes also to inform that, publication of selected students will be made by the respective Technical Institutions or Universities and selected students for health & allied sciences and teacher education programmes will be made public through NACTE website and respective Ministry’s websites.

The Council further wishes to inform that, applications for admission will be received as described above from 15th May, 2017 to 20th August, 2017. Publication of selected students for various Certificate and Diploma programmes will be made on 14th September, 2017. Studies for academic year 2017/2018 will commence from 25th September, 2017.

Issued by:
OFFICE OF THE EXECUTIVE SECRETARY
NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION (NACTE)
DATED: 10TH MAY, 2017
Share:

NACTE : Udahili na uchaguzi 2017/18 wa Astashahada na Stashahada kutafanyika moja kwa moja vyuoni

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

==========

upload_2017-5-10_20-35-15.png
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 10/05/2017
Share:

Sunday 7 May 2017

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY TAREHE 7.5.2017

Share:

Barua ya Bodi ya Ligi kuhusu sakata la alama tatu kati ya Kagera Sugar na Simba SC.

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC juu ya sakata lao la kupokwa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar wakidai kumcheza mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
 
Kwa mujibu wa barua kutoka katika Bodi ya Ligi zimesema kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano wakati akicheza mchezo dhidi ya Simba uliofanyikia uwanja wa Kaitaba, Bukoba Aprili 2 mwaka huu.

"TFF ambayo ndiyo yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndiyo iliyokaimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu iliitisha kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilichunguza kwa undani sakata hili na baada ya uchunguzi wao ambao walihoji watu mbalimbali, walituandikia kutujulisha kuwa wamebaini mchezaji Mohamed Fakhi anayelalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 siku ya mchezo wa Kagera Sugara dhidi ya Simba hivyo alikuwa halali kucheza mchezo huo". Ilisema barua hiyo
Share:

Saturday 6 May 2017

Habari Mbaya: Wanafunzi 20 wahofiwa kufa katika ajali ya basi Karatu

Wanafunzi zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea wilayani Karatu leo asubuhi.
Habari zinaarifu kuwa , basi hilo limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi .
Inaarifiwa kuwa Wanafunzi hao  ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu.
Share:

Update: Wanafunzi Waliofariki Katika Ajali Leo Wafika 32

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera.

Mkumbo amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo Luck Vicent ya mjini Arusha.

Kati ya wale waliofariki 28 walikuwa wanafunzi huku watatu wakiwa ni dereva na walimu wao

Ripoti zinasema kuwa basi hilo liliteleza na kukosa mwelekeo ,likatoka katika barabara na kuanguka katika mto katika eneo la Marera eneo la Rhotia, kilomita chache kabla ya karatu katika barabara ya Arusha
Share:

Lowassa awalilia wanafunzi Waliofariki katika Ajali........Maiti 32 zapelekwa mochwari katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema

Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Share:

Friday 5 May 2017

TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI

 Displaying MOJA.JPG
TANZANIA YAPOKEA TUZO UMEME VIJIJINI
Jitihada za Wizara ya Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.

Serikali imetunukiwa Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno. Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger