Tuesday 11 April 2017

MPYA:HII HAPA LIST YA WALIMU WANAOSUBIRIWA KUAJIRIWA MDA WOWOTE KUANZIA SASA

Image result for SERIKALI YA TANZANIA
Share:

JINSI SIMBA ILIVYOPATA USHINDI WA KIHISTORIA DHIDI YA MBAO UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA

Simba wamepata ushindi wa kihistoria dhidi ya Mbao FC mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

Mbao FC walianza kwa kutangulia kupata magoli mawili kipindi cha kwanza na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo. Magoli ya Mbao yamefungwa na Bernard dakika ya 18 na dakika ya 33.
Hadi dakika ya 80 Simba ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 matokeo ambayo kama yangebaki hivyo dakika 90 zinamalizika basi Wekundu wa Msimbazi wangekuwa kwenye nafasi finyu ya kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.
Mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi la Simba kwa kumtoa Pastory Athanas na nafasi yake kuchuliwa na Said Ndemla, Blagnon na Mavugo wakaingia kuchukua nafasi za Liuzio na Hamad ndiyo yaliyo badili mchezo na kuipa Simba ushindi wa kwanza Kanda ya Ziwa msimu huu baada ya kuchapwa 2-1 na Kagera Sugar Jumapili iliyopita.
Magoli ya Simba yamefungwa dakika za lala salama ambapo goli lao la kwanza limefungwa dakika ya 82 na Frederick Blagnon. Uzembe wa golikipa wa Mbao Erick Ngwegwe ambaye aliuacha mpira udunde kisha akashindwa kuudaka kwa usahihi ulitua miguuni mwa Blagnon akafunga goli la pili dakika ya 90+1 na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Wakati kila mmoja akiamini mchezo utamalizika kwa sare ya Mbao 2-2 Simba, Mzamiru Yassin akaifungia Simba goli la tatu dakika ya 90+7 kwa shuti kali baada ya beki wa Mbao kupiga kichwa mpira ambao ulitua kwa Mzamiru kisha kiungo huyo wa Simba kuachia mkwaju uliomshinda mlinda mlango wa Mbao.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 58 ikiwa imecheza mechi 26 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa pointi mbili zaidi ya Yanga wanaoshuka kwenye nafasi ya pili lakini wakiwa na faida ya mechi moja mkononi.
Mbao inaendelea kubaki na pointi zake 27 ikiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, pointi nne zaidi ya Toto Africans ambayo ipo katika timu tatu zitakazoshuka daraja.
Simba wataendelea kubaki jijini Mwanza wakisubiri kucheza dhidi ya Toto Africans timu ambayo imekuwa mwiba kwa ‘mnyama’ hususan mechi inapochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mbao FC wamefungwa mechi zao zote (mbili) walizokutana na Simba msimu huu. Kabla ya kuchapwa 3-2 leo April 10, 2017, walifungwa 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa October 20, 2016 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
Swali ambalo mashabiki wengi wa Simba huenda wakawa hawajalipatia majibu ni kwanini Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo, Said Ndemla na golikipa Daniel Agyei kuanzia nje wakati wanne hao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni?
Kikosi cha Simba kilichoanza kwenye mechi dhidi ya Mbao kiliongozwa na Juuko Murshid (nahodha), Peter Manyika Jr (GK), Hamadi Juma, Mohamed Hussein, Bessala Bokungu, James Kotei, Mzamiru Yassin, Juma Liuzio, Mohamed Ibrahim na Pastory Athanas.
Walionzia benchi ni Daniel Agyei, Mwinyi Kazimoto, Frederick Blagnon, Hija Ugando, Ibrahim Ajib, Said Ndemla na Laudit Mavugo.
Matokeo kutoka uwanja wa Manungu Complex, Turiani, Morogoro
Mtibwa Sugar 0-0 Azam FC
Share:

Nafasi za Kazi National Environment Management Council (NEMC)

DIRECTOR GENERAL OF NATIONAL ENVIRONMENT MANAGEMENT COUNCIL (NEMC) - 1 POST
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL TAREHE 11.4.2017

Share:

Monday 10 April 2017

ROMA MKATOLIKI ASIMULIA JINSI ALIVYOTEKWA NA KUTESWA AKIWA NA WENZAKE WATATU


Mwanamuziki Roma Mkatoliki amezungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu usiku wa Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records Masaki jijini Dar es Salaam.
Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi na kupelekwa eneo ambalo halijulikani. 
Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka hawakujua ni wapi.
Tumekuandikia kile alichosimulia.
Wakati naendelea na shughuli zangu, walifika watu ambao sikuweza kuwafahamu mbaya zaidi walikuwa na silaha za moto na amri yao ya kwanza ilikuwa ni ingia ndani ya gari. 


Baada ya kuingia tu ndani ya gari, nakumbuka wale watu walitufunga usoni na vitambaa na kutuamuru tuiname chini kwa order ya kwamba inama chini na usiinuke na wakiwa wameshika silaha za moto. 

Hofu yetu ikatufanya wote tuiname chini na gari ikaanza kuondoka maeneo ya studio na ikaelekea ambako sisi hatukupajua.
Tulipofika hiyo sehemu ambayo hatuijui tukiwa tumefungwa usoni, na walitufunga na pingu.

 Tukaenda sehemu ambayo hatuijui, kwa kuhisi tu hujui chochote na ndio sehemu ambayo tulikaa kwa siku zote tatu kwasababu ilikuwa ni Jumatano, Alhamis, tunakuja kupata sisi usalama ilikuwa ni Ijumaa usiku kuamkia Jumamosi. 

Kwahiyo siku zote watu kilichokuwa kinaendelea huko ambako tupo na hatupafahamu, kuna mahojiano yalikuwa yanaendelea baina yetu na wale watu, mahojiano yenyewe ndio hizo details ambazo nasema tumesharipoti katika vyombo vya dola wanaendelea na upelelezi, wakimaliza upelelezi, wao wenyewe wataongea watatoa taarifa.
Lakini mahojiano hayo yaliendana na vipigo ambavyo nimeonesha majereha. Kila mtu alipata majereha, kila mtu alipigwa, kwahiyo mahojiano yalikuwa yanaendelea na hizo torture mpaka siku ya Ijumaa usiku sababu hatukuwa tunaweza kugundua ni saa ngapi. 

Tulitolewa hapo tulipokuwepo na kuingizwa ndani ya gari na safari ilipoanza hapo tukiwa tumefungwa vilevile lakini safari hiyo tulifungwa na mdomo, tukafungwa na miguu tukiwa ndani ya gari tukaenda umbali ambao hatukuweza kujua ni wapi mpaka kufika eneo ambalo tukatupwa tukiwa katika hali hiyo wote wanne.
Ilikuwa ni usiku sanam hatukuweza kujua ni wapi lakini tulifikiri ni kwenye dimbwi tu la maji tumetupwa. 

Niliweza kujifungua mimi wa kwanza nikawafungua na wenzangu, hatukujua ni maeneo gani lakini yalikuwa maeneo ya baharini, tulikuwa na maumivu sana. 

Nilivyoweza kuwafungua wenzangu tukajikuta tuko salama, tukaanza kutembea kwa muda kiasi na baada ya muda tukakutana na kibao fulani kimeandikwa mahaba beach tukagundua kuwa pale ni maeneo ya Ununio.

Tulitembea kwa umbali mrefu sana mpaka tulipoweza kupata msaada baada ya hapo tukaenda kuripoti maelezo yote katika kituo cha polisi.
ALIPOFIKA NYUMBANI
Tulipofika Mbezi mimi nagonga mlango, ndani hakuna mtu, nikazunguka mlango wa nyuma nikavunja mlango wa nyumbani kwangu. Kuingia ndani familia hakuna, hilo lilikuwa pigo jingine kwangu sababu sikujua familia yangu nayo imeenda wapi.

Hiyo ikawa hofu nyingine, kwahiyo tulichokifanya nikawaambia tubadilishe nguo nikachukua nguo nikawa wenzangu, tutokea katika zile nguo za matatizo.

Nikawaambia kama familia haipo nadhani hapa si salama, ilikuwa inaelekea alfajiri saa kumi saa kumi na moja ikabidi tutoke tutafute bajaji tukiwa katika mavazi salama ikawa ni nafuu kwetu. 

Tulipotafuta bajaji tukaomba namba ya simu ya bajaji kumpigia mtu. Na mtu wa kwanza kumpigia ni bosi wetu J-Murder, hakutuamini kwamba ni sisi kwasababu ya kile alichokuwa anajua kinaendelea uraiani.

Kwa ufupi Haya ni baadhi ya Maneno ya Roma
1. Kwanza natoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, nimeona mmesimama imara, pia serikali.
2.Kilichotokea ni kama case study maana kimetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana. 
3.Niwaambie ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa. 
4.Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge. 
5.Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa. 
6.Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya. 
7.Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari. 
8.Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana. 
9.Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaazna kutembea bila kujua tuko wapi. 
10.Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika. 
Share:

HISTORIA YA JESHI LA POLISI TANZANIA


Share:

Mbinu Za Kupata Wafadhili Kutoka Nje Ya Nchi, Ili Kuitekeleza Fursa Yako

Wiki moja iliyopita niliacha ahadi yangu ya kuwa makala ijayo nitakueleza namna ya kupata wafadhili katika fursa yako. Na nilipokea barua pepe nyingi na ujumbe mfupi wa maandishi kwamba wanasubiri kwa hamu. Basi bila shaka siku uliyoingojea kwa hamu ndiyo hii. Kaa mkao wa kulisha ubongo kisha twende sawa ili niweze kukata kiu yako.

Enzi za utoto ndiko kulikonifanya niweze kujua ukweli juu ya jambo hili. Unajua ni kwanini? Wakati tupo wadogo pale kijini kwetu palikuwa na kanisa ambako watoto wengi tulikuwa tunapenda kwenda zaidi hasa pale walipokuwa wanakuja wazungu. Wengi tulikuwa tunapenda kwenda katika kipindi hicho wakija wageni hao kwa sababu walikuwa wanakuja na vitu vizuri kwa ajili yetu na kuweza kutugawia watoto wote ambao tulikuwepo siku hiyo. Walikuwa wanatugawia vitu kama saa, nguo, baiskeli na vitu vingine vingi ambavyo wakati huo vilikuwa vinatuvutia sana.

Nafikiri kwa kisa hicho kama utakuwa miongoni wa waliokuwa wanapata zawadi hizo nitakuwa nimekukumbusha mbali sana. Lakini kwa kipindi hicho hakuna aliyejali kwamba wale wazungu wamepajuaje kanisani petu pale kijijini zaidi ya kufurahia zawadi zao! na wakati hawajawai kufika hata siku moja katika bara letu hili! Kadri nilivyozidi kukua nikazidi kufanya uchunguzi ambao ulikata kiu yangu, naamini pia utakata kiu yako. Kumbe ukweli ni kwamba kuna njia ambazo huwa zinatumika mpaka kuweza kuwapata wafadhili ambao wapo nje ya nchi na wakaweza kukusaidia katika kutekeleza jambo lako.

Jambo ambalo huzingatiwa zaidi katika kupata wafadhili , wao huangalia mtu ambaye amekwisha kuanza kulitekeleza jambo lake kwa kiwango fulani. Kama nilivyokueleza mfano wa kanisa hapo juu ili wawaze kukufadhili ni lazima uwe umeshalianzisha kanisa hilo. Usiwatafute wafadhili kwa kupiga ‘stori’ tu bila kuwa na kitu maana kuna usemi unasema mwenye nacho huongozewa. Je, unataka kufahamu ni njia zipi za kutumia ili kuwapata wafadhili?
Zifuatazo ndizo njia za kupata wafadhili katika mradi wako;

1. Intaneti/wavuti (website)
Hii ndio njia ya kwanza ambayo kiukweli itakufanya ambayo hata wewe ukiweza kuitumia leo utakwenda kunufaika zaidi. Ikumbukwe ya kwamba kuitumia intaneti vizuri ni pesa mkononi ambayo itakufanya utengeneze pesa zaidi. Namna ya kutumia njia hii ni kwamba, ingia ‘google’ ile sehemu ya kuandika jambo ambalo unalihitaji, kisha andika jambo lako. Kwa mfano unacho kituo cha kulelea watoto yatima na unataka kupata hao wafadhiri.

Unaweza kuandika hivi (Organization supporting orphan children) baada ya hapo, ‘google’ itafunguaka kurasa mbalimbali zenye matokea zaidi hata ya elfu tano. Tuliza akili yako na uanze kufungua moja baada ya nyingine. Ukifungua nenda sehemu ya ‘home ya page’ hiyo kisha tafuta sehemu ya ‘contact page’ , baada ya kuipata sehemu hiyo zichukue namba zao za mawasiliano na uanze kuwasiliana nao watu hao. Huenda pia wakawa hawajaweka namba ya zao za simu au e-mail zao ila kukawa na sehemu ya wewe kujaza taarifa zao zijaze kisha utaona ni jinsi gani mtakavyoweza kuwasiliana nao.

2. Kujitolea na kujipendekeza.
Baada ya kutembelea hizo kurasa zao anza sasa na kujitolea na kujipendekeza kwa kutuma mawazo yako chanya, tuma picha mbalimbali za huku afrika ikiwemo vivutio tulivyonavyo, tuma shughuli unazofanya kama ni kilimo, biashara na vitu vingine baada ya hapo anza kutuma picha za jambo lako ambalo unalitaka ufadhili kama ni kituo cha kulelea watoto yatima tuma majengo yake kama tayari kimeanza kutoa huduma tuma picha mbalimbali.

Kufanya hivi kutawafanya wafadhili hao waweze kupenda kuja kukutembelea na kuona hivyo vitu vya utalii vilivyomo katika nchi yako. Hakikisha ya kwamba huwaombi fedha wafadhili hao mwanzoni tu mwa mawasiliano yenu maana watakuona wewe ni tapeli.

3. Jifunze kwa watu ambao tayari wana wafadhili.
Kwa kuwa kuna watu tayari wamekwisha wapata wafadhili ni muda wako muafaka wa kuwauliza waliwapata vipi wafadhili hao? Kufanya hivyo kutakufanya uweze kuwapa wafadhili katika jambo lako. Pia kama utakuwa hajaweza kuwapata wafadhili wa kutoka ya nje unaweza kujua namna ya kuwapata wafadhili wa ndani ya nchi ambao nao wana mchango mkubwa katika kukufanikisha jambo lako kwa muda sahihi. Kuwa ni mtu wa kutaka kujifunza zaidi kwa kufuatalia mwenyewe kwa ndani kuliko kusikia tu.
Share:

Norway yatangaza mapambano dhidi ya ugaidi

Norway imetangaza kuwepo kwa mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi baada ya kugundua bomu lililotengenezwa nyumbani kwenye mji mkuu Oslo siku ya Jumamosi.
Kwa sasa imedhibitika kuwa ilipangwa kufanywa kwa shambulizi mjini hapo kama ilivyokuwa kwa miji ya nchi nyingine mfano Stockholm, St Petersburg na London iliyoteak siku za hivi karibuni.
Kijana wa miaka 17 raia wa Urusi amekamatwa akihusishwa na tukio hilo.

Mwanasheria wa kijana huyo anasema kuwa hizo ni njama tu, Vyombo vya dola vinasema kuwa wamefanya mahojiano na kijana huyo na amekiri kuliunga mkono kundi la IS.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL TAEHE 10.4.2017

Share:

Thursday 6 April 2017

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRIL TAREHE 6.4.2017

Share:

Wednesday 5 April 2017

VIDEO | Bahati x Rayvanny - Nikumbushe | Watch/Download


Bahati x Rayvanny - Nikumbushe
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO SUA AWAMU YA 11 2016/2017

Image result for SUANET.AC.TZ 

Batch 11 Addition Loan Allocations for SUA Students Receiving loan from HESLB

Click link to Download >>Batch 11 Addition Loan Allocations for SUA Students Receiving loan from HESLB
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL TAREHE 5.4.2017

Share:

MADIWANI DODOMA WAMNG'OA MEYA,HAWANA IMANI NAYE


Jafari Mwanyemba
***
MADIWANI wa Manispaa ya Dodoma wamemwondoa Meya wao, Jafari Mwanyemba kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye kutokana na kumtuhumu kuhusika na tuhuma mbalimbali zikiwamo za ubadhirifu wa fedha.
Kura hizo zilipigwa mjini hapa kwenye Mkutano Maalumu wa Madiwani wa kujadili tuhuma dhidi ya Meya Mwanyemba.
Kati ya madiwani wa manispaa hiyo 56, 47 ndio walipiga kura ya kutokuwa na imani naye dhidi ya kura nne zilizodai kuwa na imani naye, wakati kura moja iliharibika na madiwani wanane hawakupiga kura.
Akitangaza matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa, Godwin Kunambi alisema kuanzia saa 8.30 adhuhuri hiyo, Mwanyemba si Meya wa Manispaa ya Dodoma na kutokana na kanuni za manispaa, Naibu Meya Jumanne Ngede ndiye atakayekuwa akiongoza hadi uchaguzi wa kuziba nafasi utakapofanyika miezi miwili kuanzia sasa.
Alisema kutokana na kanuni za halmashauri hiyo namba 4 (8), baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa kurudisha ripoti kwa mkurugenzi katika kipindi cha siku 14, alitakiwa kuwasilisha kwenye mkutano maalumu wa madiwani kwa uamuzi wa tuhuma dhidi ya meya huyo ambapo madiwani wameamua kumng’oa kwa kupigia kura.
Kutokana na kupigwa kura ya kumng’oa, kanuni za halmashauri zinamruhusu aliyekuwa Meya wa Manispaa ndani ya mwezi mmoja kukata.
Share:

Tuesday 4 April 2017

Rais Magufuli amteua Prof. Kitila A. Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji

[​IMG]
Share:

NAFASI ZA MASOMO CHUO KIKUU SAUT MWANZA KWA DIGRII MWAKA WA MASOMO 2017/2018


SAUT
Formal application for admission is made on an Application form.
The forms are available below for downloading. Please click on the links provided below. Download the application form, fill-out the hard copy accordingly. Attach copies of Academic Certificates/Transcripts, and together with a non-refundable, non-creditable application fee of Tshs 20,000.00 (For Tanzanian) or US$25 (For Foreigner) should accompany the application and
Share:

NAFASI ZA MASOMO NGAZI YA CHETI CHUO KIKUU MUM -MOROGORO 2017/2018

Image result for MUM.AC.TZ 

KUSOMA TANGAZO
>>BONYEZA HAPA<<
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger