Tuesday 3 May 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY TAREHE 3.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Monday 2 May 2016

New Audio: Harmonize & Raymond - Penzi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

LEICESTER CITY NEW CHAMPIONS ENGLISH PREMIER LEAGUE .2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

TCU: List of Qualified and Disqualified SJUIT Students as at 2nd May 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
List of Qualified and Disqualified SJUIT Students as at 2nd May 2016
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY TAREHE 2.5.2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Sunday 1 May 2016

Sherehe za Mei Mosi : Rais Magufuli Ashusha Kodi ya Mapato Ya Mshahara (PAYE) Kutoka Asilimia 11 Hadi 9 ;

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli  ametangaza kushusha kodi ya mapato ya Mshahara ( Pay as you Earn -PAYE  )  kutoka asilimia 11 iliyopo sasa hadi asilimia 9.
Rais amesema ameamua kuchukua umamuzi huo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwapunguzia mizigo wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na kuwapunguzia kodi ya mapato ya mishahara.

Kuhusu kuwaongezea mishahara, Rais Magufuli ameomba wafanyakazi wamvumilie kwa kuwa hivi sasa yuko kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuziba mianya yote ya Rushwa.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka waajiri wote nchini kuwapa wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kupeleka makato yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa
Share:

Serikali Yaendelea Kuhakiki Madeni ya Walimu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dakta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, jana tarehe 30, Aprili, 2016, kwamba serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwaajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo

Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa  20.125bn, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.

Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi 600m badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya

Dakta Mpango alisema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yao na watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.
Share:

Auawa na Mdogo wake Baada ya Kumfumania Akifanya Mapenzi na Mkewe

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkazi wa Mahembo Manyanda Manyilizu (40) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mdogo wake baada ya kumfumania akiwa na mkewe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.

“Manyilizu alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema Kisusi.

Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.

Katika tukio jingine, watu wawili wameuawa kwa kupigwa mawe na marungu kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi.

Kisusi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Shimba wilayani Kahama.

Kisusi alisema watu hao walituhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kumvamia Mchongaraji Ndalawa (65), akiwa amelala nyumbani kwake wakimtaka awape fedha.

“Alivyosema hana walimkata kwa panga kichwani, ndipo wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua,” alisema.

Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri.
Share:

Wabunge wa CCM Wakataa Bunge Kuonyeshwa LIVE,Wapinzani Waamua Kujirekodi Kwa Simu Zao

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wabunge wa CCM jana waliibuka kidedea walipowazidi wenzao wa upinzani kwa kura za sauti “Siyooooo” kuikataa hoja ya kutaka matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja ‘live’ na televisheni. 

Hiyo ilitokea jana wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utumishi na Utawala Bora) na kuzua mvutano mkali uliosababisha bajeti hiyo ipitishwe kwa utaratibu wa wabunge kutohoji kitu chochote (guillotine).

Wakati hoja yao hiyo ikipingwa kila kona, tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, wabunge hao wa upinzani sasa wamebuni mbinu mpya ya kujirekodi wenyewe wakati wakichangia mijadala mbalimbali bungeni na kurusha sauti zao kwenye mitandao ya kijamii na kupeleka sauti hizo kwenye redio zilizopo katika maeneo ya majimbo yao.

Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Salehe ndiye aliyeibua hoja hiyo akitaka kushika mshahara wa waziri kwa maelezo kuwa kuzuia Bunge kurushwa ‘live’ ni kinyume na utawala bora na haki ya kupata habari.

Hoja hiyo iliungwa mkono na  Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, Masoud Abdalla Salim (Mtambale-CUF), Rose Kamili (Viti Maalumu -Chadema), Ester Matiko (Tarime Mjini – Chadema) na Mussa Mbarouk (Tanga Mjini - CUF).

Wabunge wa CCM waliopewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuchangia hoja hiyo ni Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Kangi Lugola (Mwibara), Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) pamoja na Waziri Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.

Ilivyokuwa  Bungeni
 Baada ya Salehe kutaka ufafanuzi wa kina huku akisisitiza kuwa uamuzi huo unakiuka Katiba ya nchi na haki ya kupata habari, Kairuki alisema kwa mujibu wa Ibara ya 18 na 100 ya Katiba zinazozungumzia uhuru wa kupata habari, uamuzi huo ni sahihi na hakuna mwananchi aliyenyimwa taarifa.

Maelezo hayo yalipingwa na Salehe, safari hii akifafanua kuwa matangazo ya Bunge yanarekodiwa kwa saa saba na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) kwa saa moja tu, huku wabunge wa upinzani wakiondolewa na kuonyeshwa wa CCM pekee.

Alitaka vyombo vya habari vya elektroniki kuruhusiwa kurekodi shughuli za Bunge na kurusha maudhui wanayoyataka, badala ya kupewa video na studio ya Bunge ambayo huondoa michango na hoja za wapinzani.

Mchungaji Msigwa, Masoud Abdallah, Kamili, Matiko waliungana na Salehe na kusisitiza kuwa nchi nyingi barani Afrika zinarusha ‘live’ matangazo ya Bunge huku wakihoji sababu za TBC kurusha moja kwa moja harusi na kushindwa kuonyesha shughuli za Bunge.

Mbarouk alikwenda mbali akitaka Bunge kuanza shughuli zake usiku ili kuendana na utetezi wa Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuwa usiku wananchi wengi wanakuwa majumbani mwao hivyo wanapata nafasi nzuri ya kufuatilia Bunge.

Matiko: Juzi Rais John Magufuli kazindua Daraja la Kigamboni, TBC ilikata matangazo ya Bunge ili kuonyesha uzinduzi huo. Yaani ya kwenu mnataka yaonyeshwe ila haya ya Bunge yasionekane. Mnakiuka demokrasia.

Ghasia: Demokrasia siyo Bunge kuonyeshwa ‘live’. Wakulima na wafugaji hawawezi kuona Bunge asubuhi ndiyo maana yanarushwa usiku. 

Serukamba: Mbona wabunge wa Chadema wanaonyeshwa katika matangazo ya TBC. Hoja kwamba maagizo ya Serikali hayatawafikia watendaji si kweli.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju alisema wapinzani hawajiamini na hawaaminiki huku akiwataka wasome ibara ya 100 ya Katiba; “Bunge kuonyeshwa au kutoonyeshwa hakuongezi kitu jimboni. Wanaozungumza ni wabunge siyo televisheni.”

Akihitimisha hoja, Kairuki alipinga maelezo ya Salehe na kutoa mfano wa nchi ambazo matangazo ya Bunge hayarushwi moja kwa moja.

Kutokana na mvutano huo Chenge aliwahoji wabunge wanaoafiki hoja ya Salehe waseme “ndiyooo”, wapinzani pekee wakasema ndiyoo, aliposema wasioafiki waseme siyo, wabunge wa CCM kutokana na wingi waliitikia kwa sauti kubwa siyoooo, na Chenge akasema anadhani wasioafiki wameshinda. 

Wapinzani  Waamua Kujirekodi kwa simu
Kwa zaidi ya mara tano,wabunge wa upinzani wameshuhudiwa wakijirekodi ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kutumia simu zao za mkononi, wanapotoka nje huulizana kama wameshatumia video na sauti hizo katika mitandao ya kijamii.

Juzi, Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utawala Bora) alirusha sauti yake katika mitandao ya kijamii na kusema hiyo ni moja ya njia ya kuwafanya wananchi wajue kinachoendelea bungeni.
Share:

Serikali kutumia shilingi bilioni 59.5 kuwezesha vijiji nchi nzima

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017

Dokta Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016, kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

Alisema kuwa fedha hizo zimewekwa kwenye mfuko wa Hazina, ili kuwawezesha wadau na taasisi zitakazo husika  kupanga utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha hizo.

“Fedha hizi zitaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu” aliongeza Waziri Mpango

Akizungumza kuhusu mikopo ya wanawake na vijana, Dokta Mpango, alisema kuwa serikali, kupitia Ofisi hiyo ya Waziri  Mkuu, imepanga kutumia shilingi 1bn kuendeleza ujuzi kwa vijana wasio na ajira na shilingi 1.955bn kuwainua wanawake kiuchumi

Alifafanua kuwa halmashauri za wilaya, miji na majiji zitaendelea na utaratibu wao wa kutenga asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kutoa mikopo kwa vijana na asilimia nyingine 5 kwaajili ya kuwawezesha wanawake katika maeneo yao.
Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Viongozi Wa Mtandao Wa Vyama Vya Wazee Tanzania

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Share:

Serikali Yaokoa Sh. Bilioni 15.4 za Mishahara HEWA Machi hadi Aprili 24

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali imetangaza kuokoa kiasi cha Sh15.4 bilioni katika kipindi cha kuanzia Machi hadi Aprili 24 ambacho kingelipwa kwa watumishi hewa 8,236 ambao wamebainika hadi sasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Angela Kairuki aliliambia Bunge jana kuwa kazi ya kuwasaka watumishi hewa bado inaendelea nchini kote.

Alisema watumishi hao wamebainika katika maeneo mbalimbali na kati yao 1,614 ni wa Serikali Kuu na 6,624 wa Serikali za Mitaa.

Waziri alisema kuwapo kwa watumishi hewa kumewafukuzisha kazi maofisa 56 na taratibu za kuwafungulia kesi mahakamani zinaendelea ikiwamo kutakiwa kulipa hasara yote ambayo waliisababisha.

Alisema mapambano dhidi ya watumishi hewa ni endelevu ili kukomesha tabia hiyo inayolitia hasara taifa.

“Mheshimiwa Rais alitangaza siku za hivi karibu na mtaona nami natangaza leo idadi ikiwa juu kuliko aliyotangaza Rais na vyombo vingine vitaendelea kutangaza maana tuko kwenye kazi kila siku,” alisema Kairuki.

Alitaja changamoto kubwa katika wizara yake ni kuwa ni tofauti ya mishahara kwa wafanyakazi ambayo inaonekana ni kubwa kati ya mtu wa chini na wa juu yake, jambo alilosema Rais ameamua kulisimamia ili kulipunguza.

“Tofauti ya mishahara ni kubwa, kuna baadhi ya maeneo mtu anatakiwa kupokea mshahara wa miezi 50 au 30 ili aweze kumfikia mwenzake mwenye mshahara mmoja tu,” alisema Kairuki.

Kuhusu suala la ajira, alisema katika mwaka wa fedha wa 2016/17, Serikali imepanga kuajiri watumishi 71,496 kuanzia mwezi huu na akawataka waajiri kuacha kuwahamisha watumishi endapo hakuna fedha za kuwalipa.
Share:

Tume ya Pamoja Kufuatilia Ziara ya Rais Magufuli Nchini Rwanda

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. 
 
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. 
 
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
 
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika. 
 
Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka. 
 
Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
 
Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.
 
Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia  (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori  (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
 
Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
 
Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Gisenyi, Rwanda
30 Aprili, 2016
Share:

Dk Philip Mpango: Serikali ya Kikwete haikukomba fedha Hazina

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amesema Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete haikukomba fedha katika Hazina kama ambavyo baadhi ya wabunge wamedai, hata Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), lilifanya tathmini na kutoa taarifa safi.

Dk Mpango alieleza hayo bungeni jana mjini Dodoma, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mjadala wa wizara mbili zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walisema Serikali ya Awamu ya Nne, ilikomba fedha zote Hazina na kusababisha Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, kukuta Hazina haina fedha.

Akijibu hoja hiyo, alisema hakuna ushahidi ulioitia hatiani Serikali ya Awamu wa Nne kuhusu kukomba fedha Hazina na kwamba IMF na wadau wengine wa kimataifa, walifanya tathmini huru ya bajeti na mwenendo wa uchumi nchini na taarifa yao ya mwisho waliitoa Desemba mwaka 2015.

Katika ripoti hiyo hakuna mahali ilipoonesha nchi ilikuwa na hali mbaya ya fedha na kwamba kwa kudhihirisha hilo, vigezo vya kimataifa vilionesha bayana kuwa Deni la Taifa ni himilivu na nchi bado inakopesheka na imeendelea kulipa mishahara watumishi wake pamoja na madeni mengine bila kutetereka.

Alisema Serikali iliendelea kulipa madeni mengi na hakuna kilicholegalega, huku ikiendelea pia kugharimia shughuli za mihimili yote, ikiwemo Bunge, usalama wa nchi na kuendelea kulipa madai ya makandarasi na watoa huduma wengine.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imerithi mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali za awamu zilizopita, ikiwemo uchumi imara, umeme uliosambazwa maeneo mengi vijijini na miundombinu
Share:

Wafungwa Wanaosubiri Kunyongwa Magerezani Wafikia 465

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
IDADI ya Watanzania wanaosubiri kunyongwa imekuwa ikiongezeka na hadi sasa imefikia 465 kutokana na hukumu ya kifo kutotekelezwa tangu mwaka 1994. 

Ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Morogoro juzi, imebainisha kuwa hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais ili kutekelezwa hadi Oktoba 2015 kulipofanyika Uchaguzi Mkuu ambao Rais Magufuli aliibuka mshindi.

Ripoti hiyo ya Mpango wa Kujitathmini Kuhusu Hali ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (UPR), unaotekelezwa kwa mara ya pili nchini, imeonesha kuwa kuna mahabusu 465 wanaosubiri adhabu ya kifo, kati yao wanaume ni 445 na wanawake ni 20.

Wanaharakati 
Akiwasilisha ripoti hiyo, Ofisa Uchunguzi Mkuu wa Tume hiyo, Philemon Mponezya, alisema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, inaitaka Serikali kufuta adhabu hiyo kwa kuwa haitekelezeki lakini baadhi ya asasi hasa zinazohusika na haki za walemavu wa ngozi, zinapinga kufutwa kwa adhabu hiyo.

Baadhi ya asasi zinazopinga kufutwa kwa hukumu ya kifo ni taasisi ya Under The Same Sun (UTSS), ambayo inasema katika utafiti waliofanya, wahusika wanataka hukumu hiyo hasa inayohusu watu walioua albino, itekelezwe mpaka hapo mauaji hayo yatakapokoma.

Hata hivyo, Mponezya alisema watetezi wengi wa haki za binadamu wanataka adhabu hiyo ifutwe kwa kuwa ni kinyume cha haki za binadamu na kwa Tanzania, imekuwa mbaya zaidi kwa kuwa baadhi ya wahukumiwa wamesubiri zaidi miaka 20 bila hukumu dhidi yao kutekelezwa, jambo linalowaathiri kisaikolojia.

“Tume inasisitiza Serikali iangalie upya hukumu hii na kuiondoa kwa sababu ya utekelezaji wake. Tangu mwaka 1994 hadi leo watu 465 wanasubiri adhabu hiyo, hakuna aliyenyongwa. Kila mlango unapogongwa unahisi ni wewe kumbe la, tunadhani iondolewe maana haitekelezwi,” alisema Mponezya.

Wananchi wagawanyika 
Tume hiyo ilikiri kwamba, Tanzania imeshindwa kutekeleza adhabu hiyo kwa miaka mingi kutokana na Serikali kueleza kuwa jamii imegawanyika kuhusu hukumu hiyo. 

Wapo wanaotaka ifutwe lakini wengi wanataka iendelee kutekelezwa kutokana na ongezeko la mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina na albino.

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mark Mulumbo, alipotakiwa kufafanua kuhusu mtazamo wa kisheria na kiserikali kuhusu utekelezaji wa adhabu hiyo katika mafunzo hayo, alikiri kwamba tafiti zilizofanywa nchini zimeonesha kuwa, kuna mgawanyiko kwa wananchi kuhusu adhabu hiyo.

“Tume kadhaa zilizoundwa kupata maoni ya wananchi, zilitoa matokeo kuwa wananchi wengi bado hawataki adhabu iondolewe, wanataka iendelee kuwapo, sasa Serikali inafanya kazi kwa matakwa ya wananchi, si vinginevyo,” alisema Mulumbo.

Akifafanua zaidi, alisema hata katika mchakato wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hali hiyo ilijitokeza kwamba Watanzania wengi hawaoni kama muda ni mwafaka kufuta adhabu hiyo. 

Marais 
Kuhusu marais kushindwa kusaini hukumu hiyo, Mulumbo alisema upo mtazamo wa aina mbili kuhusu jambo hilo; wa kiimani na kisheria.

Alisema pamoja na kwamba nchi haina dini, marais wote waliowahi kuchaguliwa mpaka wa Awamu ya Tano, wana imani za kidini. 

“Siwasemei kwamba imani zao ni sababu, lakini huenda ni sababu.Ila kisheria rais hahukumiwi akisaini hukumu hiyo, sasa hilo mimi siwezi kulisemea ila sheria zinaweza kuangaliwa zaidi, ili zimpe rais nafasi ya kumpa mhusika kifungo cha maisha. 

“Lakini hapo napo kuna mtazamo mwingine, maana kuna hoja kwamba kwa nini aliyeua na kupatikana na hatia afungwe maisha. Je, iko wapi haki ya aliyeuawa?” Alifafanua Mulumbo kwa mtazamo wake.

Wanaoipenda 
Mwanasheria wa UTSS aliyewasilisha mada katika mafunzo hayo, Perpetua Senkoro, ambaye pia ana ulemavu wa ngozi, alisema  kwamba, utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwa walemavu wa ngozi (albino) kuhusu hukumu hiyo, umeonesha jamii inataka iendelee kuwapo, na itekelezwe.

Senkoro alisema wana imani sawa na wanaharakati wenzao wa haki za binadamu kuwa dhana ya hukumu ni kumfanya mkosaji abadilike na hukumu ya kifo haitoi nafasi ya kubadilika, lakini kwao kutokana na namna wanavyouliwa kwa imani za kishirikina, hilo si suala la tabia bali ni imani na hivyo muuaji hawezi kubadilika, wanaona heri iendelee kuwapo na itekelezwe.

“Wengi wa jamii yetu wanataka hukumu iendelee kuwapo mpaka hapo mauaji kwa albino yatakapokoma na itekelezwe. Wauaji wa albino wanaua kwa imani si tabia, wanatumwa na watu wenye fedha, kiungo kinauzwa Dola za Marekani 2,000, tena tunaona wanaokamatwa ni vidagaa, bado mapapa hatuyaoni, tunaomba Serikali (ya Magufuli) iwatafute vigogo na tuone hukumu hii ikitekelezwa ili kumaliza imani hizi zinazowanyima haki baadhi yetu ya kuishi,” alisema Senkoro.

Pamoja na Tanzania kuridhia mapendekezo kadha wa kadha ya haki za binadamu, bado Mei 9 hadi 12 mwaka huu, katika mkutano wa Geneva, Uswisi itaulizwa utekelezaji wa mapendekezo mengine na msimamo wa nchi kuhusu kufuta adhabu ya kifo.

Mkutano huo utahudhuriwa na asasi mbalimbali za utetezi wa haki za binadamu nchini, viongozi wa serikali pamoja na tume za haki za binadamu, ambapo nchi zaidi ya 190 zinatarajiwa kushiriki.

Ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, imeonesha kuwa idadi ya watu waliouawa mwaka 2015 katika utekelezaji wa hukumu ya kifo ni kubwa zaidi tangu mwaka 1990.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 1,634 waliuawa mwaka jana sawa na asimilia 50 ya waliouawa mwaka 2014. Aidha takwimu hizo hazihusu utekelezaji wa hukumu hiyo nchini China, ambako takwimu za adhabu hiyo huwa siri ingawa zinatajwa kuwa kubwa. 

Nchi zinazotajwa kutekeleza zaidi hukumu hiyo mwaka jana ni Iran, Pakistan na Saudi Arabia ambako asilimia 90 adhabu hiyo ilitekelezwa.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY TAREHE 1.5.2016 (MEI MOSI-SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger