Saturday 27 February 2016

SCHORASHIP:China scholarship opportunities for 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ministry of Energy and Minerals

1. INTRODUCTION
Applications are invited from committed, motivated and qualified Tanzanians to apply for postgraduate studies in the one of China’s best Oil and Gas Universities – the China University of Geosciences (Wuhan).
Sponsorship will be in the fields of oil and gas. The scholarships will be processed in collaboration with the Embassy of China in Tanzania and will be awarded to the best twenty two (22) candidates.
2. ELIGIBILITY
a) Applicants must be holders of Bachelor’s degree in Earth Sciences or Engineering from recognized universities;
b)Master’s Degree and Ph.D. applicants should not be older than 35 and 40 years respectively;
c)Applicants will be required to pay for a ticket to China; other costs will be paid by the Government of China including return ticket; and
d)Applicant once awarded scholarship, will not be allowed to decline for any reasons.
 >>Read More>>
Share:

Mawaziri ‘Waliombip’ Magufuli Hadharani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MAWAZIRI watano wamewekwa hadharani kuwa ndio hawakujaza Tamko la Rasilimali na Madeni na Hati ya Ahadi ya Uadilifu na kurejesha fomu hizo katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana asubuhi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema Rais John Magufuli, aliagiza mawaziri hao watekeleze wajibu huo kabla ya saa 12.00 jioni, vinginevyo watakuwa wamejiondoa wenyewe katika nafasi zao.

“Rais ameelekeza mawaziri popote walipo warudi na kutekeleza hilo na ofisi yangu itasimamia kwa karibu kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni na Hati ya Ahadi ya Uadilifu. “Wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili, atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Majaliwa alisema Rais ameelekeza mawaziri hao watajwe ili popote walipo wajue na kurejea kuzijaza fomu hizo.

Kutokana na maelekezo hayo, Majaliwa aliwataja mawaziri hao kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, ambao hawajarudisha fomu zote mbili za Tamko la Rasilimali na Madeni na Hati ya Ahadi ya Uadilifu.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga ambaye alikuwa hajarejesha Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ambaye alikuwa hajarudisha Tamko la Rasilimali na Madeni.

Waziri Mkuu alisema Naibu Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira), Luhaga Mpina, yeye alikuwa hajarejesha fomu zote mbili za Tamko la Rasilimali na Madeni na Hati ya Ahadi ya Uadilifu.

Aliweka msisitizao kuwa kiongozi yeyote wa umma, anatakiwa kujaza fomu ya kutamka mali na madeni kwa viongozi wa umma na kuhaidi uadilifu uliotukuka na sheria hiyo itaendelea kufanyiwa kazi kwa wote wanoendelea kuteuliwa.

Akizungumzia suala la mawaziri waliokuwa safari ambao pengine wangeshindwa kuwasilisha fomu hizo, Majaliwa alisema cha muhimu agizo limetolewa na sababu nyingine zitaangaliwa kama zina msingi.

Alisema kama mawaziri hao wako nje ya nchi, ni lazima Rais anajua kwani ndiye anayetoa kibali na ikiwa wako mikoani ambako hawataweza kufika mpaka jana jioni, Waziri Mkuu anafahamu hivyo wataangalia sababu hizo.

Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya mawaziri na naibu mawaziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu juzi, alikabidhiwa majina ya mawaziri hao.

Akifafanua Majaliwa alisema kila kiongozi anawajibika kutoa tamko la mali na madeni ndani ya siku 30 baada ya kuteuliwa, mwisho wa kutumia wadhifa husika na kila mwisho wa mwaka.

Alisema mawaziri walikabidhiwa fomu hizo walipoteuliwa na viongozi wengine wameendelea kujazafomu hizo na kurudisha kwa Kamishna.

Akizungumza juzi katika mafunzo hayo, Kamishna wa Maadili Jaji mstaafu Salome Kaganda, alisema ofisi yake ilikuwa imepokea fomu za matamko ya mali kutoka kwa baadhi ya mawaziri na baadhi yao walikuwa hawajajaza fomu hizo wala za ahadi ya uadilifu.

Alisema Sheria ya Maadili inamtaka kila kiongozi, kuwajibika kuwasilisha tamko la mali kwa sekretarieti hiyo na jukumu la chombo hicho cha kusimamia maadili ya viongozi, ni kupokea fomu za tamko la kiongozi wa umma za rasilimali, maslahi na madeni.

Jukumu linguine alitaja kuwa ni kupokea, kuchambua na kuchunguza malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa maadili unaodaiwa kufanywa na viongozi wa umma na kuandaa na kutunza daftari la rasilimali, maslahi na madeni ya viongozi hao.

Alisema sekretarieti hiyo ina wajibu wa kuratibu vikao vya Baraza la Maadili kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma na kuwasilisha kwa Rais taarifa hizo za uchunguzi.

Kwa mujibu wa jaji Kaganda, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995, inatamka maadili yanayotakiwa kuzingatiwa na kila kiongozi kuwa ni uadilifu, haki na uwajibikaji ambazo ni sifa muhimu za kiongozi bora.

Jaji Kaganda alisema kwa kuzingatia misingi na miongozo hiyo, katika sheria hiyo mawaziri na wakuu wa mikoa wamewekewa kifungu maalumu kinachobainisha maadili wanayopaswa kuyatekeleza.
Share:

RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Gianni Infantino

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-Uefa, Gianni Infantino amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Soka duniani-Fifa.

Infantino alishinda awamu ya pilii ya uchaguzi huo uliofanyika Uswisi kwa kura 88 kati ya kura 207 akifuatiwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain aliyepata 85.

Mwanafalme wa Jordan Ali Bin Hussein alipata kura 27 na mgombea kutoka Ufaransa Jerome Champagne alipata kura saba.

Infantino mwenye umri wa miaka 45 anashika nafasi hiyo kumrithi Sepp Blatter aliyesimamishwa kushiriki shughuli zozote za soka kwa miaka minane adhabu ambayo ilipunguzwa kuwa miaka sita pamoja na Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini kwa tuhuma za rushwa.

"Ndugu zangu, siwezi kuelezea hasia zangu kwa wakati huu," Infantino alisema wakati akizungumza baada ya kuchaguliwa. "Tutarejesha hadhi na heshima ya Fifa. Watu watatupongeza, watawapongeza ninyi kwa mabadiliko tutakayofanya.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARY 27 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

VIDEO_NAY WA MITEGO-SHIKA ADABU YAKO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tokeo la picha la shika adabu yako video 
Huku audio ya wimbo Shika Adabu yako wake Nay wamitego, ykizidi kufanya poa kabisa, hatimaye Nay amekuletea Official Video ya wimbo huwo.
Bofya hapa chini kuutazama 
Share:

VIDEO:MWANAFUNZI WA SAUT MWANZA AKIPIGWA MAWE,BAADA YA KUNG'ANG'ANIA SIMU YA MPENZI WAKE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
marehemu akiwa na mpenzi wake aliemsababishia kifo
Share:

Friday 26 February 2016

Video:UKAWA/CHADEMA WAONGELEA KUHUSU UCHAGUZI WA MEYA LEO DAR FEB 27 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Kesho February 27  Dar es salaam inategemea kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji,  Vyama mbalimbali vimejiandaa kwa uchaguzi huo. Leo Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu ameongea na waandishi wa habari na kusema..
Uchaguzi kesho unafanyika, tunatoa rai kwa mamlaka zote zinazohusika kusimamia uchaguzi huu, miezi miwili tumekuwa tukivutana katika jambo hili, Kuna taarifa kwamba wapo wanaotaka kuharibu uchaguzi huu.’
Njama zozote za kufanya figisufigisu hatutazivumilia, tunahaki za kuwatumikia Watanzania na tunaomba kesho uchaguzi ufanyike kwa amani, hatutarajii kuliona Jeshi la Polisi kwamaana uchaguzi utakuwa ni wa amani‘ ;-Salum Mwalimu
Unaweza kuicheki full stori kwenye hii video hapa chini…

Share:

GARI LA NAY WA MITEGO LAVUNJWA VIOO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Gari la Nay 
Mkali wa muziki wa Bongo fleva na hit song ya Shika adabu yako Nay wa Mitego, amekutwa na majanga ya kuvunjiwa kioo cha gari usiku huu na kumsababishia ashindwe kuachia rasmi Video ya wimbo wake huwo.
Share:

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI BENKI YA ACCESS MBAGALA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MAJAMBAZI WATATU WAUAWA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI BENKI YA ACCESS MBAGALA Benki ya Access tawi la Mbagala Rangi Tatu kumetokea tukio la ujambazi -Majambazi watatu wameuawa na polisi baada ya kuzidiwa nguvu. CHANZO:JMF

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu





Benki ya Access tawi la Mbagala Rangi Tatu kumetokea tukio la ujambazi
-Majambazi watatu wameuawa na polisi baada ya kuzidiwa nguvu.

CHANZO:JMF
Share:

BREAKING NEWS:CHUO KIKUU ST.JOSEPH ARUSHA CHAFUTWA RASMI NA TCU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.Tunapenda kuuarifu umma kwamba, Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha ni mojawapo ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ambacho kilianza kudahili wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka wa masomo 2013/2014.

2.Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.
 

3.Kwa muda mrefu na kwa wakati tofauti kumekuwapo na matukio ya migogoro baina ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Kampasi ya Arusha na wanafunzi. 
Kwa kipindi hiki chote Tume imekuwa ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo kwa uongozi wa chuo kurekebisha kasoro zinazosababisha migogoro chuoni hapo.
Kwa sehemu kubwa migogoro hiyo imekuwa ikitokana na matatizo ya ubora, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu kama zilivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu. 
Hata hivyo jitihada za Tume ya Vyuo Vikuu kukitaka Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa katika Kampasi hii inakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na Tume hazikupewa uzito stahiki na uongozi wa chuo.
 

4.Hivi sasa Kampasi ya Arusha ina jumla ya wanafunzi 1557 wanaosoma programu za masomo ya ualimu wa sayansi zifuatazo:
5.Kutokana na yaliyobainishwa hapo awali, tunapenda kuuarifu umma kwamba, Tume imejiridhisha kuwa Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuendelea kutoa elimu ya chuo kikuu. 
Kwa kuzingatia ukweli kwamba wanafunzi ndio waathirika wakuu wa matatizo yaliyopo kwenye Kampasi hii, Tume imeamua kama ifuatavyo:
 

a)Imefuta kibali kilichoanzisha Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) na kuidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote waliokuwa wanasoma katika Kampasi hiyo ya Arusha kwa gharama za Chuo Kikuu cha SJUIT. Orodha ya majina yao na vyuo watakavyopangiwa itatangazwa na kuwekwa katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu hivi punde.
 

b)Imefuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi. Na kwamba, wanafunzi wanaoendelea na masomo katika programu hii watahamishiwa katika Kampasi ya Luguruni, Dar es Salaam, na watalazimika kwanza kuhitimu katika ngazi ya Stashada (Diploma) kama ilivyokuwa imeidhinishwa na Tume hapo awali. Utaratibu wa uhamisho wa wanafunzi wa programu hii utatangazwa hivi punde na kuwekwa katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu.
 

c) Imeidhinisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao hawakuweza kupata udahili katika vyuo vikuu vingine, kutoka katika kundi la wapatao 500 waliofukuzwa chuoni kutokana na migogoro iliyojitokeza katika Kampasi ya Arusha mwezi Juni, 2015 kuendelea na masomo katika vyuo watakavyopangiwa baada ya taratibu za uchambuzi wa taarifa zao kukamilika. Orodha ya majina yao na vyuo watakavyopangiwa itatangazwa na kuwekwa katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu hivi punde.
 

6.Kufuatia uamuzi huu, wanafunzi wote wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Kampasi ya Arusha wanaarifiwa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo vikuu vingine vinavyofundisha programu za masomo zinazofanana na masomo wanayosoma hivi sasa chini ya utaratibu na masharti yafuatayo:
 

 i)Wanafunzi wote wanapaswa kuondoka chuoni mara moja baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi mali na vifaa vingine vya chuo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
 

 ii)Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo watakavyopangiwa wakati wa kufunguliwa kwa muhula (semester) wa pili. Tarehe halisi ya kuanza kwa muhula wa pili kwa kila chuo watakachopangiwa itatangazwa na kuwekwa kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
 

 iii)Wanafunzi wanaosoma shahada ya miaka mitatu ya ualimu wa sayansi katika masomo yafuatayo watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM):

     a)Bachelor of Science in Education with Mathematics & Chemistry;

   b)Bachelor of Science in Education with Physics & Chemistry, na

   c)Bachelor of Science in Education with Physics & Computer Science.
 

 iv)Wanafunzi wanaosoma shahada ya miaka mitatu ya ualimu wa sayansi na Kompyuta (Bachelor of Science in Education with Mathematics & Computer Science) watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU):
 

 v)Wanafunzi wanaosoma shahada ya miaka mitatu ya ualimu wa sayansi katika masomo yafuatayo watahamishiwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge (MWECAU):

  a)Bachelor of Science in Education with Physics & Mathematics; na

  b)Bachelor of Science in Education with Biology & Chemistry.

vi)Orodha ya wanafunzi waliohamishwa na majina ya vyuo vikuu walivyohamishiwa itatangazwa na kuwekwa kwenye tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu hivi punde.
 

 vii)Wanafunzi wote waliohamishwa ambao hawakukamilisha mitihani yao ya mwisho wa muhula wa kwanza, au hawakufanya kabisa mitihani hiyo, watatakiwa kufanya mitihani hiyo katika vyuo vikuu watavyohamishiwa kwa utaratibu maalum utakaondaliwa na chuo husika.
 viii) Kila mwanafunzi anawajibika kutunza kumbukumbu zake zote muhimu za maendeleo ya kitaalama kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ikiwa ni pamoja na matokeo ya mitihani aliyokwishafanya.
 

ix)Wanafunzi wote ambao ni wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mikopo yao itahamishiwa katika vyuo wakapokuwa wamehamishiwa.
 

7.Kampasi nyingine za Chuo Kikuu cha SJUIT (Luguruni na Boko – Dar es Salaam; na Makambako – Njombe) zitaendelea na masomo kama kawaida.
 

8.Kwa taarifa hii, vyuo vikuu vyote nchini vinakumbushwa kufuata sheria na kuzingatia utoaji wa elimu inayokidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. Tume haitasita kuchukua hatua stahiki kwa chuo kikuu chochote kitakachobainika kutoa elimu isiyokidhi viwango vya ubora kwa kisingizio cha aina yoyote.
 

Imetolewa na

PROF. YUNUS D. MGAYA
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 
26 Februari 2016
Share:

MPYA:HII NDIO LIST YA VYUO BORA TANZANIA 2016

Share:

MPYA:HIVI HAPA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU KIDATO CHA PILI(FTSEE),NNE(CSEE) NA SITA(ACSEE) 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MFUMO WA KUTUNUKU MATOKEO YA UPIMAJI/MITIHANI YA TAIFA


Share:

BREAKING NEWSSerikali yatoa muda mpaka saa 12 jioni kwa mawaziri wasiopeleka tamko la mali

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari:Rais John Pombe Magufuli ametoa muda mpaka leo jioni kwa Mawaziri wanne na Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu kwa Sekrtariati ya maadili kwa ajili ya kuanisha mali na madeni wanayodaiwa ambapo wamepewa muda mpaka saa 12 wawe wamesharejesha fomu hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja majina mawaziri hao kuwa ni
Agustine Mahiga
Charles Kitwanga,
January Makamba,
Joyce Ndali Chako na Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.
by ITV

Share:

TANZIA:MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU SUA Bsc.IRRIGATION AND WATER RESOURCE ENGINEERING AMEKUTWA KAFARIKI KATIKA PORI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ipatapo jana mida ya saa 9 jioni nilipata meseja ikisema  kwamba kuna mwanafunzi kakapotea ni mwaka wa kwanza kozi ya irrigation engineering-sua,wenzako wanaekaa nae room walisema kwamba mwenzao alikuwa ni mgonjwa hivyo siku hiyo aliondoka tangu asubuhi na laiacha simu yake ndani na wakidhani ameenda sehemu ya karibu,hadi kufikia mida ya jioni alikuwa hajarudi.
Leo mida ya mchana huu nimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa hostel zao Mr.hatibu Kilenga ambae amesema kwamba;

"Kwa masikitiko makubwa  napenda kuwajulisha ndugu wana SUA wanafunzi wote ,waafanyakazi na watu wote kwamba leo asubuhimajira ya saa tano asubuhi baada ya heka heka za kumtafuta ndugu yetu YEREMIA MBENDULE,hatimae tumemkuta katika pori la uwanja wa suaakiwa tayari amefariki dunia,tukiwa na polisi tunampeleka marehemu hospitali ya mkoa wa morogoro kwa taratibu nyingine.
Namshukuru Rais wa chuo Mr.Ndunguru,makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mr.Salim na wanafunzi wote kwa ujumla kwa jitihada za kumtafuta mpendwa wetu"
Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!AMEN

Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza kozi ya Bsc.irrigation and resource engineering na jumatatu alikuwa anajiandaa kuanza mtihani wake wa mwiho wa muhula.

Uongozi wa MASWAYETUBLOG unapenda kutoa pole kwa familia ya marehemu.
Share:

Vigogo Watatu Wa Mradi wa Mabasi ya (DART) Wafikishwa Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo, wamepandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5.

Mbali na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na kusomewa mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Walisomewa mashitaka na wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jackline Nyantori akisaidiwa na Estazia Wilson na Stellah Mafuru.

Nyantori alidai kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi 2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5.

Katika mashitaka yanayomkabili Mwakatobe, inadaiwa Juni 29, 2005 katika ofisi za kodi Ilala, Dar es Salaam, alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), wakati akiwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2004 na ya 2005 ya kampuni yake ya Yukan Business, jambo lililosababisha alipe kodi ndogo.

Awali, Wakili Nyantole alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amewasilisha hati ya kuruhusu mahakama hiyo, kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi hivyo washitakiwa wataruhusiwa kujibu mashitaka yao.

Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Takukuru ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hawana pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa.

Hakimu Mwijage alisema Asteria, Katale na Kugesha watapata dhamana endapo kila mmoja atakuwa na mdhamini mmoja anayefanyakazi serikalini au kwenye taasisi inayofahamika, atakayesaini hati ya Sh milioni 15. Pia kila mshitakiwa awasilishe Sh milioni 15 au hati isiyohamishika yenye thamani ya Sh milioni 15.

Kwa upande wa Mwakatobe, dhamana yake ipo wazi endapo atapata mdhamini mmoja mwenye barua kutoka taasisi inayofahamika, asaini hati ya Sh milioni tano.

Wote waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti. Asteria na Katale wametakiwa kuwasilisha hati hizo Machi 3 mwaka huu. Kesi itatajwa tena Machi 9 mwaka huu.
Share:

Basi La Mashimba Express La Kahama- Mwanza Lapata ajali Kuua Watu Wanne

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Watu wanne wamefariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo  katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu  Mkoani Shinyanga

Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ilisababishwa  na  gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu  wawili  waliokuwa  katika  gari  hilo  akiwemo  dereva  walifariki  dunia  papo hapo

Mganga mfawidhi wa hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo  walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.

Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger