Friday 30 October 2015

JOINING INSTUCTIONS VECTOR CONTROL TRAINING CENTRE 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

ADVANCED DIPLOMA IN VECTOR CONTROL (IN SERVICE) VECTOR CONTROL TRAINING CENTRE 2015/2016

KINDLY CLICK HERE TO DOWNLOAD 
Share:

JOINING INSTRUCTIONS ADVANCED DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (IN SERVICE)-MBEYA 2015/2016

Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS YA BUGANDO-AMO TRAINING 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
ADVANCED DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (AMO) IN SERVICE  AMO TRAINING CENTRE - BUGANDO

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS

Share:

DOWNLOAD JOINING INTSRUCTIONS ZA DIPLOMA MUHIMBILI 2015/2016

Share:

Updated List Of Third Batch Selected Students To Join KIU For 2015/2016

Share:

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU MWENGE 4TH BATCH 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2015/2016 academic year. Registration shall begin on wednesday, 28th October, 2015 followed by Orentation on Friday 30th October, 2015  and lectures shall begin on Monday, 2nd November, 2015.
Click Here to view the selected canditates.
Click Here to view Pre-Orientation Information.
Click Here to download Medical Form.
Share:

Picha 10 kutoka ndani ya Ikulu Rais JK alivyomkaribisha Dk. Magufuli.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Ni siku ambayo tayari historia imeandikwa kwenye vichwa vya Habari za Siasa Tanzania ambapo Dk. John Pombe Joseph Magufuli ametangazwa kuywa mshindi wa kiti cha Urais kwenye Uchaguzi mkuu uliofanyika October 25 2015.
unnamed ii
Rais JK na Dk. Magufuli ndani ya Ikulu baada ya matokeo ya Urais kutangazwa October 29 2015
Kwa maana hiyo Dk. Magufuli anakuwa Rais anayekuja kubadili nafasi ya Rais Jakaya Kikwete na kuwa Rais wa awamu ya tano Tanzania.
Dk. Magufuli amealikwa ndani ya Ikulu Dar es Salaam Tanzania na Rais Kikwete na kupongezwa kwa ushindi huo… hapa ninazo picha kutoka ndani ya Ikulu hiyo.
unnamed iii
Dk. John Magufuli.
unnamed iv
Rais JK, Mama Salma Kikwete kwa pamoja wakimpongeza Dk. John Magufuli.
unnamed ix unnamed v unnamed vi unnamed VII unnamed viii unnamed x unnamed XII
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCTOBER 30 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday 29 October 2015

ANGALIA HAPA ADA ZA CHUO KIKUU ST.FRANCIS IFAKARA MWAKA WA MASOMO 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

FEE STRUCTURE FOR VARIOUS PROGRAMMES IN ACADEMIC YEAR 2015 - 2016

Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU TIA DAR NA MBEYA CAMPUS 2ND BATCH 2015/2016

Share:

DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZWA RAIS MTEULE AWAMU YA TANO 2015-2020

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
post-feature-image

RAIS NI MAGUFULI: TUME

Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA CHETI NA DIPLOMA-NACTE 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Habari yenu wadau wa blog hii pendwa ya MAASWAYETU BLOG Leo tena tunaweletea Joining instructions za kozi mbalimbali certificates na diploma kwa mwaka wa masomo 2015/16

Tunajua wengi mnazisubiria hizi form kwa hamu sana na mnataka mjue gharama za mafunzo kwa chuo ulichochaguliwa.

Share:

TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KUBADILISHWA KWA TAREHE YA KURIPOTI CHUONI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
slide2
Chuo Kikuu cha Dodoma kinasikitika kuwatangazia Wanafunzi wote kuwa, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Chuo tarehe za kufungua Chuo zimebadilishwa.
·        Kwa wanafuzi wapya, Chuo kitafunguliwa tarehe 14 Novemba 2015 badala ya tarehe 31 Oktoba 2015
·     Kwa Wanafunzi wanaondelea, Chuo kitafunguliwa tarehe 21 Novemba 2015 badala ya tarehe 7 Novemba 2015 iliyokuwa imetangazwa awali. 
·        Mitihani ya marudio (Suplimentary Examinations) itafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2015.
Wanafunzi wote mnatakiwa kukamilisha malipo ya ada na malipo mengine kabla ya kuripoti Chuoni. Wanafunzi watakaoshindwa kukamilisha malipo hayo hawatapokelewa Chuoni.
Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na Ofisi ya Mahusiano
29 Oktoba 2015

Share:

Wednesday 28 October 2015

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SEKOMU 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Loans Allocations Of Continuing Students
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA ST.JOHN UNIVERSITY 4TH BATCH 2015/2016

Share:

ANGALIA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALIMBALI VYA AFYA 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Habari yenu,
Kama kawaida yetu MASWAYETU blog tunanendelea kukuletea huduma karibu zaidi,Kutokana na NACTE kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya afya 2015/2016 pia unatakiwa kufanya confirmation ya uchaguzi ulipochaguliwa usipofanya hivyo nafasi yako itapotea.

Kwa hiyo MASWAYETU BLOG INATOA HUDUMA IFUATAYO,

1.TUMA JINA ALKO KAMILI KWENDA NAMBA 0768260834 mfano:PAUL  LUGANDA(AFYA SELECTION OCTOBER 2015/2016)

2.HUDUMA HII UTASAIDIA KUFANYIWA CONFIRMATION YA CHUO
   ULICHOCHAGULIWA.


3.HUDUMA HII UTATOZWA TSHS 1000 TU AMBAYO UTAITUMA KWA MPESA KWENDA NAMBA 0768260834 AU TIGO PESA 0652740927
4.UTAJIBIWA NDANI YA DK MOJA TU.
Share:

Mambo 20 yaliyotamkwa na Edward Lowassa (UKAWA) na January Makamba ( CCM) leo Oct 28.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
1: Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo, katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi, majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe.
———-
2: Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi, kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya.
———-
3: Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa, bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura, hata hivyo tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI
4: CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi, tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru uliofanyika kwa uwazi na kwa amani na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa.
———-
5: Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.
———-
MALALAMIKO YA UKAWA
6: Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na waandishi wa habari jana, tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume, hata hivyo matokeo ya Ubunge wanayakubali na kule wanakoshinda, wanayasheherekea.
———-
7: Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile, hata fomu ya matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura, zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: urais, ubunge na udiwani.
———–
8: Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura. Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume, wasimamizi na taratibu zote.
————
9: Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho aliyonayo mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli atakapotangazwa mshindi.
————-
10: Kwetu sisi CCM, kuchagua wagombea bora na kuwanadi na kutengeneza sera bora na kuzinadi, pamoja na rekodi yetu katika uongozi wa nchi, ndio njia zetu pekee za ushawishi. Katika uchaguzi huu, wananchi wamefanya maamuzi yao kwa uhuru na utashi, ikiwemo kuwaangusha mawaziri sita ambao tuliwasimamisha kama wagombea wetu katika majimbo mbalimbali nguvu na utashi wa wananchi umejidhihirisha katika uchaguzi huu.
————–
11: Mchakato wa uchaguzi sasa unakaribia kufikia ukingoni, tutawapata madiwani, wabunge na Rais, tunapaswa kuendelea na maisha na tuwape nafasi watutumikie. Jitihada tunazoziona sasa za viongozi wa UKAWA za kuendeleza siasa za uchaguzi kwenye mitaa ya miji yetu kwa njia za vurugu na maandamano hazikubaliki hata kidogo.
————–
12: Tunalaani kitendo cha wafuasi wa UKAWA kuchoma ofisi za CCM katika Wilaya ya Mbozi. Amani ya nchi hii ina thamani kuliko hitaji la madaraka la mtu yoyote. Wenzetu wa UKAWA wana haki ya kulalamika lakini hawana haki ya kuiingiza nchi yetu machafukoni kwa kuwakusanya vijana na kuwaingiza mitaani wafanye vurugu na kuhatarisha maisha, kuharibu mali na kusimamisha shughuli za watu wengine. tunawaomba Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida huku kila mmoja akitambua wajibu wake wa kuilinda amani ya nchi yetu.


MAMBO 8 YALIYOSEMWA NA EDWARD LOWASSA

1: ‘Hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu ya Rais, Wabunge na Madiwani yanayoendelea kutangazwa nchini na tume ya taifa ya uchaguzi, hii ni sababu upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo haya umevurugwa kwa makusudi na Watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na wa chama cha Mapinduzi’

2: ‘Katika maeneo mengi matokeo yalikotangazwa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais hakifanani wala kwendana na matakwa halisi ya Wananchi, matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM John Pombe Magufuli’

3: ‘Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM… kwa aibu sana, maeneo mengine kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa, mfano Jimbo la Mkoani na Mtambile Pemba, Makunduchi, Chambani, Kilindi na kwengineko ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa sio kura za uchaguzi mkuu wa Rais bali mzimu wa uchaguzi’

4: ‘Katika maeneo mengine likiwemo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyopo mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi yanatofautiana na yale yaliyokusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo, hali kama hii ipo kwenye majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA, NCCR na C.U.F ama wamekua na nguvu kubwa au wameibuka Washindi’

5: ‘Uko ushahidi wa wazi katika majimbo yote Wagombea wa UKAWA wameshinda, tume imechelewa kutangaza matokeo ya Urais kwa sababu zinazothibitishwa kuwepo mikakati ya hila, matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada ya jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabu kura na kuwakamata Wataalamu wetu waliokua wakipokea matokeo ya nchi nzima ambako tulikua tukiongoza kwa maeneo mbalimbali’

6: ‘Tunaamini kwa dhati kwamba uvamizi huo ulifanyika kwa makusudi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa na NEC, tunapenda kuwataarifu na Jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati huo uvamizi umefanyika kura zetu za Urais zilionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60 kabla hawajatunyang’anya documents zetu, computer zetu’

7: ‘Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na Watendaji wa NEC, mimi Edward Lowassa na mgombea mwenza, tunautangazia Umma wa Watanzania na Jumuiya ya kimataifa kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC, tunataka wasitishe mara moja na kuanza upya kuhakiki, kinachofanywa na NEC hapa ndicho kinachofanywa Zanzibar, zinafanyika juhudi za kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa ushindi wa Maalim Seif’

8: ‘Tunaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na amani na mshikamano, tunachosema sisi utaratibu umekosewa wasitishe na wasipositisha tutachukua hatua ambazo tutazitangaza baada ya kamati kuu ya chama chetu kukutana leo’
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger