Sunday 6 September 2015

Magufuli: Nikiwa Rais Nitachukua Mashamba Yasiyotumika

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kunyang’any’a mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo. 
 
Alisema hayo alipozungumza na wananchi wa wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro jana.

Dk Magufuli alisema akiwa rais, kuna mambo mengi anaweza kufanya, kukabiliana na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na mojawapo ni kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi, unaosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.

Alisema kuna watu wanamiliki maelfu ya eka za ardhi bila kulima na kwamba atanyang’any’a mashamba hayo ambayo yamehodhiwa na watu hao bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo. 
 
Akihutubia maelfu ya wananchi, pia Dk Magufuli alisema kuwa anajivunia uzoefu wa marais wastaafu wa Awamu ya Pili mpaka Awamu ya Nne na wa Zanzibar, kwamba ndio atakaowafuata kwa ushauri akikwama popote.

Alisema hiyo ni moja ya tofauti kubwa kati yake na wagombea wengine wa urais. 
 
“Nitaingia Ikulu nikiwa na washauri wazuri, nikikwama mahali nitakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, nikikwama nitaenda kwa mzee Benjamin Mkapa, nikikwama tena nakwenda kwa mzee Ali Hasan Mwinyi.

“Wako wengi, upo ushauri nitauchukua kutoka kwa mzee Salmin Amour (Rais Mstaafu wa Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein na kwa Amani Abeid Karume,” alisema. 
 
Kutokana na fursa hiyo ya kiuongozi aliyonayo ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Dk Magufuli aliomba Watanzania wote bila kujali vyama vya siasa, makabila wala dini kumpa kura kwa wingi kwa kuwa atakuwa na washauri wazuri wenye uzoefu.

Alisema wagombea wengine, akiwemo wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa, hawataweza kupata ushauri wa washauri hao kama ilivyo rahisi kwake.

Kutokana na uhakika huo wa washauri wazoefu, Dk Magufuli alisema ndio maana baadhi ya wagombea hao wanaweza kuja na ahadi za uongo, ikiwemo ya kuondoa nyumba za tembe na za nyasi.

Aliwataka wananchi kuwapima wagombea hao katika ahadi zao, kwa kuwa baadhi walikuwepo ndani ya Serikali kwa muda mrefu, lakini walishindwa kuondoa nyumba hizo katika majimbo walikotokea.

Dk Magufuli alisema yeye hataahidi kuondoa nyumba hizo, bali anaahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi wanaofanya kazi wajenge nyumba bora.

Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana.

Alisema atataka kila anayefanya kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia kukabiliana na mahitaji ya maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora kutokana na kushushwa kwa bei za bidhaa za ujenzi. 
 
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao.
Share:

Dr. Slaa Aishambulia CHADEMA Kwa Mara ya Pili.......Asisitiza Kuwa Lowassa ni Fisadi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani kwa mara nyingine na kujibu watu waliojitokeza kuponda hotuba yake, aliyoitoa hivi karibuni kuwa hawana hoja zaidi ya kumtukana.

Akizungumza kupitia kituo kimoja cha Televisheni jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema madai yote, yaliyotolewa juu yake na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa Chadema na vyama vinavyounda Ukawa, baada ya hotuba aliyoitoa, hayana msingi wowote na kwamba ni kuishiwa hoja, ndio maana walimtukana badala ya kujibu hoja.

“Nashukuru hoja zangu zote hawajazijibu, sasa wanapiga tu propaganda, hata Rostam Aziz alijaribu kujibu, lakini akatukana tu kama alivyonitukana mwaka 2007 badala ya kujibu hoja na mimi nasema ufisadi ni hoja,” alisema Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema hawezi kumpeleka mahakamani Rostam ambaye ni kada wa CCM, ambaye amemtaka Dk Slaa ampeleke mahakamani kama anao ushahidi kuwa anaunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Slaa amesema yuko tayari kutoa ushahidi wake pale Jamhuri itakapomfungulia mashitaka. “Wale ambao hawaelewi taratibu za kesi, kuna kesi za madai ambapo mtu binafsi anafungua kesi na kesi za jinai ambazo mtu binafsi hawezi kufungua ila Jamhuri, kesi za Jamhuri mtu huwezi kufungua, wewe ni shahidi… mimi nikiitwa nitakwenda kutoa ushahidi dhidi ya Rostam Aziz,” alisema Dk Slaa.

Aidha, alisema ni kweli vijana wanataka mabadiliko na ni hoja ya msingi na pia wakulima ambao hawafaidiki na kilimo chao, wanataka mabadiliko, vivyo hivyo kwa makundi mengine.
 
 “Nimesema mimi Lowassa hafai, leo, lini ameanza kuwa rafiki wa masikini?

"Lini ameanza kuwa safi?Watanzania waache ushabiki usiofaa wapime kwa vigezo, ushabiki usio na tija utatuangamiza,” alisema Dk Slaa, akijibu hoja mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya hotuba yake hiyo, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutangaza kuachana na mambo ya siasa na kubaki mshauri wa wananchi.

Akijibu shutuma dhidi yake baada ya kutuhumiwa kutoa habari za upotoshaji juu ya maaskofu, Slaa alisema alichokieleza siku ile anatangaza kujiengua kwenye siasa ni alichoambiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwamba maaskofu 30 kati ya 34 walihongwa.

“Tatizo halikuwa fedha bali askofu anaona sifa mimi kumuunga mkono mtu ambaye alitumia fedha kununua maaskofu, na Watanzania nawaomba mtulie msikurupuke na maneno bila kuyachambua, taifa linaangamia kwa sababu ya ushabiki usio na tija, nimeshtushwa na kauli yake, kiongozi anayepaswa kukemea rushwa, maovu… baba askofu piga magoti Mungu wako atazame dhamira yako,” alisema.

Dk Slaa alisema yeye ana uwezo wa kupambanua siasa na mambo mengine na kwamba ni kweli alikutana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe katika Hoteli ya Serena na hiyo ni katika kupata taarifa alizozihitaji kwa ajili ya kazi yake ya utafiti na kwamba Mwakyembe ni chanzo cha taarifa cha kwanza na kwamba hakufanya kwa siri.

Akizungumzia picha yake ambayo ilizunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha yeye akiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema picha hiyo ni wakati wa mkutano wa vyama vya siasa na Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipokuja kwenye ziara ya kikazi Februari mwaka huu.

“Kwenye picha hizo ambazo zinatuonesha mimi, Mwigulu na Profesa Lipumba tukimpokea Rais wa Ujerumani alipotembelea Tanzania, leo ndio zinaletwa kuonesha eti haya ndiyo mazungumzo ya kumng’oa Slaa, naomba niwaambie warudi nyuma waangalie hizo picha ni za lini hazina uhusiano na mimi kujiondoa,” alisema Dk Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema kuwa kuna propaganda nyingine ambayo imetumika ambapo watu wametuma pia picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye ndege, ikisemekana kwamba ametoroka nchini baada ya hotuba, sio kweli.

Alikiri kusafiri lakini sio kwa kutoroka, kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu na kwamba amekuwa akipiga picha na watu kwenye ndege na kwamba picha hiyo ni ya safari ambayo alishasafiri na kurudi.

“Magazeti na mitandao wanasema Dk Slaa hayuko nchini, lakini nadhani sasa Watanzania wanaona sasa niko hapa studio Dar es Salaam na siko Marekani,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa uongo huo unaonesha ni aina gani za siasa zilizopo hapa nchini.

Alisema hoja ya wapi amepata fedha kwenda Serengeti na kuishi hotelini ni hafifu. “Nilikwenda Marekani na kukaa kwa zaidi ya miezi 12 na kutembelea majimbo 13 na sikulipiwa na mtu yoyote zaidi ya chama changu kulipia shilingi 500,000 kwa mshauri aliyeandaa nyaraka ya kunisaidia katika ziara hiyo, mbona hawakuniuliza nimepata wapi fedha hizo?”
Share:

Lembeli Aanika MAOVU Yaliyofichwa Wakati wa Operesheni Tokomeza

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameishambulia serikali ya CCM na kueleza kwamba serikali hiyo haiwezi kuwapatia wananchi maendeleo kutokana na kuwa na mfumo mbovu wa kiutawala.

Mbali na hilo Lembeli alisema serikali ya CCM ndiyo serikali pekee yenye mfumo kandamizi, viongozi wake ni walaghai wakubwa na imekuwa na mfumo mchafu wa kulindana mafisadi kwa mafisadi huku wananchi wa kawaida wakiendelea kutaabika.

Lembeli ambaye awali alikuwa mbunge wa CCM jimbo la Kahama na baadaye kutimkia Chadema, alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chadema zilizofanyika katika viwanja vya Freeman Mbowe ambapo uwanja huo ulijengwa na mbunge anayemaliza muda wake na kutetea jimbo hilo Prof Kulikoyela Kahigi.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo alitonesha vidonda vya wafugaji wa jimbo hilo kwa kueleza kwamba serikali imekalia ripoti ya uchunguzi wa Tume iliyoundwa na bunge kwa ajili ya Operesheni tokomeza.

Alisema sababu kubwa ya serikali kushindwa kuweka hadharani taarifa hiyo ambayo Lembeli alikuwa mwenyekiti ni kutokana na vitendo vingi vilivyofanywa vilikuwa vikihusisha vigogo wa serikali na ndiyo maana kuna hali ya kulindana licha ya kuwa wapo watu ambao wamepata vilema na wengine kupoteza maisha.

Alisema katika taarifa hiyo kuna mambo mengi ya kutisha ambayo yalifanywa na watumishi wa serikali ikiwa ni pamoja na kudhalilisha utu wa mtu, mauaji pamoja na uharibifu wa mali za wananchi hususan wafugaji.

“Ndugu zangu wana Bukombe kuna msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata, sasa mtungi ni CCM na kata ni mimi (Lembeli) mimi nimetoka CCM baada ya kuona kwamba hakuna chama dharimu, kandamizaji, kinachotumia migogo ya wanyonge masikini kujinufaisha.

“Sijaona chama chenye viongozi ambao wanalinda ufisadi wa kutisha, wizi wa kutisha pamoja na watu ambao hata upeo wa kufikiri umekwisha bali wamekuwa watu wa kupokea vitisho vya hali ya juu na hatima yake wanatugeuza kuwa wapumbavu na malofa,” amesema Lembeli.

Akizungumzia ahadi za mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Lembeli amesema kwamba mgombea huyo kwa sasa amekuwa akiwalaghai wasukuma kwa madai kwamba atawapatia maendeleo pale tu atakapochaguliwa.

Amesema kauli hiyo ni ya uongo na unafiki kamwe Dk. Magufuli awezi hata kuwatetea wasukuma wenzake.

“Nawapa mifano miwili tu wakati Dk. Magufuli akiwa waziri wa mafugo aliwasaidia nini wafugaji wakati mifugo ikiteketea na kukosekana kwa soko.

“Mbali na hilo alipochaguliwa kuwa waziri wa mifugo na uvuvi ni nani ambaye alikuwa akichoma kokolo za wavuvi kwa madai hazifahi, alikuwa wapi kushika nyavu hizo zikiwa madukani na kuzipiga marufuku wakati huo huo aliendelea kuchoma nyavu hizo, hapo kweli ana nia ya kuwakomboa watanzania hususani wakulima na wafugaji,” alihoji Lembeli.
Share:

MKUTANO WA MAGUFULI IFAKARA MOROGORO

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

COMMONWEALTH Scholarships tenable in the UK for 2015

Share:

MKUTANO WA LOWASSA TABORA(PICHA)

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 06 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Saturday 5 September 2015

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 05/9/2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY




Share:

Friday 4 September 2015

MKUTANO WA LOWASSA MPANDA-KATAVI-RUKWA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Share:

MKUTANO WA CCM DODOMA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Sukuhu Hassan, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni Dodoma mjini leo.
 Kijana akiwa na bango wakati akienda mkutano wa  kampeni za CCM Dodoma mjini leo
 Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika leo Dodoma mjini
 Mgombea wa ubunge jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Dodoma mjini leo
 Maelfu ya wanannchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Sukuhu Hassan alipowalisi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo
 Maelfu ya wanannchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Sukuhu Hassan alipowalisi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo
 Wagombea Ubunge Livingstone Lusinde (Mtera) na Anthony Mavunde (Dodoma mjini) wakishiriki kucheza muziki jukwani wakai wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo Dodoma mjini leo na kuhutubiwa na mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan
 Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa wakati wa mkutano wa kampeii za CCm uliofanyika leo Dodoma mjini
 Wagombea Udiwani Dodoma mjini wakiwa  kwenye mkutano wa kampeniwa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia uliofanyika leo
 Mgombea Ubunge Dodoma mjini,  Anthony Mavunde akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Dodoma mjini


 Kinkundi cha Hapa Kazi kutoka Tanga wakitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika leo, jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kibakwe , Dk. Simba Chawene akiomba kura kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo hilo leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia (kushoto) akishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la Hapa Kazi, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika, jimbo la Kibakwe mkoani dodoma leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa kampeni katika jimbo la Kibakwe mkoani dodoma leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kibakwe, Dk. Simba Chawene katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo hilo leo. Kushoto ni Mama Mariam Simbachawene.
 Msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia ukiwa umeuziwa na wananchi wakati akienda jimbo la Mtera leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,  akimnadi Mgombea Ubunge wa Ubunge jimbo la Mtera Livingstone Lusinde katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
 Mgombea Mwenza wa Urais tikati ya CCM, Mama Samia akiwahutubia wananchi wa jimbo la Mtera katika mkutnao wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo
Maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni katika jimbo la Mtera leo
Share:

POLISI WAMTIA MBARONI TAPELI SUGU..ANATEPELI WASTAAFU NCHI NZIMA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la David Makali maarufu kama Peter Mabula amekamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani kwa kuwatapeli wastaafu nchini.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime aliwaambia waandishi wa habari kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatapeli wastaafu kwa kujifanya yeye ni mtumishi wa Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

“Mtuhumiwa pia amekuwa akijifanya ni mtumishi wa Mfuko wa pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni wa PSPF na Mtumishi wa ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Afya na kufanikiwa kuwaibia fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika mikoa mbalimbali.
“Wanachofanya watu hawa hupiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani pamoja na namba za akaunti zao za simu,” amesema Kamanda Misime.
Amesema kwa njia hiyo matapeli hao wamefanikiwa kupata orodha ya wastaafu kutoka katika mikoa takriban 15 hususan kutoka kwenye idara ya afya.
“Wakishapata orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu, humpigia mstaafu na kujitambulisha anatokea wizarani na kwamba anashughulikia wastaafu ambao inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonesha naye amepunjwa milioni fulani,” amesema Kamanda Misime.
Amesema watuhumiwa hao hutumia mwanya huo kuwatapeli fedha wastaafu kwamba watume fedha ili wawasaidie waweze kupata fedha zao walizopunjwa na baada ya mstaafu husika kutuma hizo fedha, mtu huyo anakuwa hapatikani tena katika simu.
Kamanda Misime amewatahadharisha wastaafu kutokubaliana na watu wa aina hiyo na idara mbalimbali zichukue tahadhari na kila mara wahakikishe kinachohitajika kinatoka katika idara husika na kwa mtu sahihi.
Share:

New AUDIO | PNC - Wale Wale | Download/Listen

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/nr55e6a6ht6o/PNC_-_Wale_Wale.mp3?d=1
Share:

New AUDIO | Msaga sumu - Lowassa | Download/Listen

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

New AUDIO | Msaga sumu - Lowassa | Download/Listen

DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/5h9o26dzol1c/Msaga_sumu_-_Lowassa.mp3?d=1
Share:

New AUDIO | Linex Ft. Baraka Da Prince - Because of You | Download/Listen

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
http://old.hulkshare.com/dl/gcb8728frs3k/Linex_Ft._Baraka_Da_Prince_-_Because_of__You.mp3?d=1
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBER TAREHE 04.9.2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Thursday 3 September 2015

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBER TAREHE 3/9/2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY.
Share:

Wednesday 2 September 2015

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 2 SEPTEMBER 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger