BARAZA
Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wamekabidhi
msaada wa madawati 500 kwa serikali ili kusaidia upungufu wa madawati
katika shule za msingi na sekondari.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi madawati, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Abubakar Bin Zuberi amesema kuwa katika msaada hawaangalii suala la dini
kinachoangaliwa ni watakaolia madawati hayo ni watanzania.
Mufti
Zuberi amesema kuwa wamechangia katika kusaidia serikali kauli mbiu ya
elimu bure katika kuweza kusaidia watanzania wapate elimu.
Amesema
kuwa wataendelea kushawishi waislaam katika kuendelea kuchangia elimu
ili watoto wapate elimu iliyo bora kwa kuwa serikali pekee yake haiwezi
kutatua changamoto zote za elimu.
Mwenyekiti
wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa amepeleka msaada huo katika bakwata
ikiwa ni kuonyesha umoja na jinsi ya kusaidia serikali katika upande wa
elimu.
Amesema
kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna
watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka
kuweza kuchangia madawati 1000.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza kwa
niaba ya Waziri Mkuu amesema kuwa msaada wa madawati hayo ni mkubwa
kutokana na changamoto iliyopo mbele yao.
Amesema
kuwa idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza kuandikishwa umeongezeka
kutokana na mpango wa elimu bure hivyo serikali kupata madawati ni
jambo la furaha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia madawati
kutokana na mahitaji kuwa makubwa.
0 comments:
Post a Comment