Wednesday, 19 January 2022

COMORO YAICHAPA 3-2 GHANA NA KUITUPA NJE AFCONTIMU ya taifa ya Comoro imeitupa Ghana nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa mabao 3-2 katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku wa Jumanne Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.

Mabao ya Comoro yalifungwa na El Fardou Mohamed Ben Nabouhane dakika ya nne na Ahmed Mogni mawili, dakika ya 61 na 85, wakati ya Ghana iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Andre Ayew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25, yalifungwa na Richmond Boakye dakika ya 64 na Alexander Djiku dakika ya 77.
Share:

CHELSEA YAZIDI KUPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA EPL YATOKA SARE YA 1-1 NA BRIGHTONTIMU ya Chelsea imetoa sare ya 1-1 na wenyeji, Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa The AMEX, Falmer, East Sussex.

Hakim Ziyech alianza kuwafungia wageni dakika ya 28, kabla ya Adam Webster kuwasawazishia wenyeji dakika ya 60 na sare hiyo ya nane ya msimu inazidi kuiondolea Chelsea matumaini ya ubingwa sasa kikosi cha kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kikiachwa pointi 12 na mabingwa watetezi, Manchester City.

Chelsea inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 23 nafasi ya tatu, nyuma ya Liverpool pointi 45 za mechi 21 na Man City pointi 56 za mechi 22, wakati Brighton imefikisha pointi 29 katika mechi ya 21 nafasi ya tisa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 19,2022
Share:

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI NA KUTOWEKA NA MWILI WA MAREHEMU


Kaburi la mtoto Christian Samson lililofukuliwa
***
Mwili wa mtoto Christian Samson (1), aliyezikwa siku ya Jumapili katika makaburi ya kitongoji cha Kipondoda wilayani Manyoni mkoani Singida, umefukuliwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana licha ya ndugu kuutafuta bila mafanikio.

Simanzi na huzuni zilitawala katika makaburi hayo hii ikiwa sio mara ya kwanza vitendo hivyo vya ufukuaji wa makaburi kujitokeza, na mara hii imejitokeza hali isiyokuwa ya kawaida kwa kuwa mwili marehemu umetafutwa kwa zaidi ya saa nne huku jitihada hizo zikishindikana.

Kufuatia hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Rahabu Mwagisa, na kuzungumzia vitendo hivyo huku akisisitiza suala la maombi kuwa ni la muhimu na jeshi la polisi linafuatilia ili kuwabaini waliohusika na kitendo hicho.

Chanzo - EATV
Share:

AWAMU YA SITA YANG'ARISHA SINGIDA MASHARIKI


............................................

ZOEZI la Uchimbaji wa visima virefu katika Jimbo la Singida Mashariki linaendelea ambapo kwa sasa ni zamu ya Kijiji Cha Mbwanjiki Kata ya Ikungi.

Kazi hiyo inafanywa na Mkandarasi M/s Target na ameshachimba mita zipatazo 152 na kupelekea maji mengi kupatikana na hivyo kufanya visima vilivyokamilika kuchimbwa kufikia vinne katika vijiji vya Kimbwi, Ujaire na Msule.

Mradi huo wa visima unatarajiwa kukamilishwa kwenye vijiji vya Mapando, Damankia na Mang'onyi ambapo baada ya kupatikana vyanzo vya maji hatua inayofuata ni kujenga miundombinu ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Matokeo hayo ni jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyoahidi kusogeza huduma za maji karibu na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),iliyoahidi kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

Kwa sasa wilaya ya Ikungi inatoa maji safi na salama kwa asilimia 58 lakini baada ya kukamilika kwa miradi hii upatikanaji wa maji utafikia asilimia 73.

Akizungumza na mtandao huu Mbunge wa Jimbo hilo Miraji Mtaturu ameishukuru serikali kwa kutenga fedha Ili kutekeleza miradi hiyo ya maji.

"Tunamshukuru Rais wetu Mh Samia Suluhu Hassan kwa kusimama imara kuitekeleza Ilani tuliyoinadi wakati wa kampeni,hii ni hatua kubwa inayoleta matumaini na uhakika wa wananchi wetu kupata maji,kweli anaposema Kazi Iendelee anamaanisha kwa vitendo,"alisema Mtaturu.
Share:

Tuesday, 18 January 2022

RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI WAWILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement), Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Mcha anachukua nafasi ya Bw. Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.

Uteuzi huu umeanza tarehe 5 Desemba, 2021.

Aidha, Mhe. Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

Balozi Mushy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Januari, 2022.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Share:

KIUNGO MNIGERIA ASEPA SIMBA
KIUNGO, Udoh Utop jana Jumapili aliondoka rasmi nchini ambapo alikuja kwa ajili ya majaribio ndani ya Simba na kurejea kwao nchini Nigeria.


Udoh alikuja nchini sambamba na winga mwenye uraia wa Ivory Coast, Cheick Mounkoro na Sharaf Shiboub waliofanya majaribio na Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupata mkataba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Udoh Utop alisema kuwa tayari ameshaondoka kurejea kwao nchini Nigeria ambapo kuna ofa nyingine amezipata, lakini kama kuna timu itakuwa ipo tayari kumsajili kutoka Tanzania yupo tayari kujiunga nayo.


“Tayari safari yangu imeiva na leo (jana) Jumapili nitaondoka kuelekea Nigeria ambapo ni nyumbani, kuna ofa nimepata kutoka timu nyingine sehemu mbalimbali nakwenda kuziangalia baada ya kushindwa kusajiliwa na Simba.


“Kuhusu Tanzania nimependa mazingira yake na soka lake hivyo kama kutakuwa na timu yoyote kutoka Tanzania itanihitaji basi nipo tayari kujiunga nayo,” alisema kiungo huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 18,2022

Magazetini leo Jumanne January 18 2022

Share:

Monday, 17 January 2022

BODI YA FILAMU KUENDELEZA FURSA ZA KUWAINUA WASANII- WAZIRI MCHENGERWA


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa maelekezo ya kuendeleza utendaji bora kwa Taasisi za Bodi ya Filamu, BASATA na COSOTA wakati alipofanya ziara katika Taasisi hizo katika majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini Dar es Salaam. Akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hassan Abbas, Naibu Katibu Mkuu Mhe. Said Othman Yakubu na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akielezea kuhusu umuhimu wa Haki za Wasanii wakati Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa alipozitembelea Taasisi za Bodi ya Filamu, BASATA na COSOTA zilizopo katika majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini Dar es Salaam.


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo akielezea majukumu na utendaji wa Bodi hiyo wakati Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa alipozitembelea Taasisi za Bodi ya Filamu, BASATA na COSOTA zilizopo katika majengo ya Utumishi, Kivukoni jijini Dar es Salaam.

...........................................................................

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuendelea kuwajengea uwezo Wadau mbalimbali wa Tasnia ya Filamu kwa lengo la kuhakikisha Wadau hao wanakuwa na uwezo wa kutoa kazi zenye viwango bora.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea na kujifunza majukumu ya Taasisi zilizopo katika Wizara hiyo ikiwemo Bodi ya Filamu Jumatatu Januari 17, 2022 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Watendaji wa Bodi ya Filamu Waziri ameitaka Bodi hiyo kuendelea kutoa elimu na kuwajengea uwezo Wadau wa Filamu ili waweze kutoa Filamu za Kitanzania zenye ubora mzuri na uhalisia zitakazoweza kutangaza fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi, hivyo kuongeza pato la Taifa.

“Tuendelee kutafuta fursa za kuwainua na kunyanyua kazi za Tasnia yetu ya Filamu ili waweze kunufaika na kufaidika na kazi zetu jambo litakalowezesha kuijenga zaidi Tasnia ya Filamu,” amesema Waziri

Aidha, Waziri amesisitiza Bodi kufuatilia utekelezaji wa uanzishaji wa Jumba Changamani ambalo litakuwa maalum katika utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza itakayowasaidia Wasanii kuandaa Filamu kwa urahisi na zenye viwango bora zaidi.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas amesisitiza Taasisi za Wizara hiyo ikiwemo Bodi ya Filamu kufanya kazi kwa malengo ya kulinda na kutetea maslahi ya Wanatasnia wa Filamu ili kuwawezesha kunufaika na kazi zao za Filamu na Michezo ya kuigiza.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Dkt. Kiagho Kilonzo akiwasilisha utendaji wa Tasnia ya Filamu pamoja na majukumu ya Bodi hiyo amesema Tasnia hiyo hadi kufikia mwaka 2021 imekuwa ikichangia katika kutoa ajira takribani 30,000 zinazotokana na shughuli za utayarishaji wa Filamu.

Ameongeza kuwa Bodi hiyo tayari iko katika hatua za kuwa na Kanzidata yenye taarifa za Wanatasnia wa Filamu kwa lengo la kutambua taarifa za Wanatasnia wa Filamu kwa urahisi na usahihi zaidi.

Dkt. Kilonzo amesema Bodi hiyo tayari inaendelea kuandaa mfumo wa Kidijitali utakaosaidia kutoa huduma kwa Wanatasnia wa Filamu kwa urahisi bila kufika Ofisini hapo. Aidha mfumo huo utarahisisha utoaji wa huduma kwa Wanatasnia katika maeneo yao na kuwapunguzia gharama pamoja na kuwapa uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger